Wafungwa na Mahabusu wenye VVU Nchini wanalishwa Ugali Maharage kila siku

Wafungwa na Mahabusu wenye VVU Nchini wanalishwa Ugali Maharage kila siku

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Taarifa iliyowasilishwa Bungeni kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya #UKIMWI na kueleza kuwa Wafungwa na Mahabusu Tanzania wanapewa aina moja ya Chakula kila Siku.

Kutokana na hilo, Afya za #Wafungwa walioathirika na Virusi vya UKIMWI na wanaotumia Dawa za Kupunguza Makali ya Virusi (ARVs) zimedhoofika kwasababu ya Ukali na Nguvu ya Dawa wanazokunywa.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kamati, idadi ya Wafungwa wenye VVU wanaotumia Dawa Nchini kote ni 888 ambapo Kamati imeshauri Serikali kuhakikisha inatoa Lishe Bora kwa Wafungwa hao.
 
Sio watu wote waliopo jela basi walifanya uhalifu.

Bado uko kwenye hii dunia inawezekana hujaona maajabu ya mtu kufungwa bila hatia, iko siku utaona hilo tena anaweza kuwa jamaa yako wa karibu sana
Nielewe hadi mwisho wa sentence
 
Kwamba huko walipo ni Holiday ?

Vipi wametoa na takwimu ni Watanzania wangapi wanakula milo mitatu, hata huo ugali hawaupati ?
 
Na hapo usiombe uwe na HIV,TYPHD,UTI...
Halafu unazaidi ya 5+yrs unakunywa dawa!!!!

ndo utakapoamini wagonjwa wa ukimwi bado wananyanyapaliwa...
 
Nani aliwaambia wafanye uhalifu, ila hata mtaani kama hutopambana hata huo ugali wa maharagwe hutopata
jela ni kama hospitali, watu hujikuta wamefika bila kutaka wao. Halafu jela hata huna kosa ni tuhuma tu unaweza kufika, kwa hiyo usione waliopo huko wamejitikia wenyewe, ni kama ajali tu, kuepuka ajali ni majaliwa ya Mungu
 
Jela ni nusu ya jehanamu hata kama watetezi wa haki za binadamu wanapambania kuwepo na maisha bora huko jela, ila ni kubaya aisee. Kudhoofika kwa afya kupo labda uwe mtumia bangi uvute utoe mawazo ukubaliane na milo ya huko. Kuna wengine wananenepa na kuwa na afya nzuri kuliko walivyokuwa uraiani. Inategemea na mtu alikuwa anakulaje alipokuwa uraiani, wengine wakifika huko wanakula kwa uhakika uji na ugali hata kama ni mara moja kwa siku uhakika wa kula upo. Changamoto ni kwa watumiaji wa dawa tiba kutokana na maradhi waliyo nayo inayowalazimu kula mlo kamili wenye virutubisho vyote. Kule jela ishu ya kula bado sana, wanalishwa kama wanyama wafugwao ndani wasiokuwa na uhuru wa kula watakavyo.
 
Back
Top Bottom