Jela ni nusu ya jehanamu hata kama watetezi wa haki za binadamu wanapambania kuwepo na maisha bora huko jela, ila ni kubaya aisee. Kudhoofika kwa afya kupo labda uwe mtumia bangi uvute utoe mawazo ukubaliane na milo ya huko. Kuna wengine wananenepa na kuwa na afya nzuri kuliko walivyokuwa uraiani. Inategemea na mtu alikuwa anakulaje alipokuwa uraiani, wengine wakifika huko wanakula kwa uhakika uji na ugali hata kama ni mara moja kwa siku uhakika wa kula upo. Changamoto ni kwa watumiaji wa dawa tiba kutokana na maradhi waliyo nayo inayowalazimu kula mlo kamili wenye virutubisho vyote. Kule jela ishu ya kula bado sana, wanalishwa kama wanyama wafugwao ndani wasiokuwa na uhuru wa kula watakavyo.