Waganga wa kienyeji walivyovunja undugu kwenye ukoo wetu

Kama uchawi umeandikwa kwenye vitabu vitakatifu kuwa upo Basi Mwenyezi Mungu hawezi kuishia kuandika tu kuwa uchawi upo Halafu ishindikane kumtambua Mchawi .

Mungu ameandika kitabu gani ?
 
Haya mambo haya hatari
 
Naunga mkono hoja.

Wachawi huwa ni ndugu zako na majirani wanaokujua.
 
Biblia Takatifu.

Biblia ni neno lililotokana na neno la Kigiriki Biblios lenye maana ya mkusanyiko wa vitabu vingi.

biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi tofauti tofauti katika miaka tofauti tofauti. Vikaja kukusanywa pamoja na roman empire na kuwa compressed kiwe kitabu kimoja kikubwa.

JE MUNGU ALIANDIKA BIBLIA LINI NA KWA USHAHIDI GANI ?

Nani alimuona Mungu wakati anaiandika biblia.. na alipomaliza kuiandika Mungu alimkabidhi nani ?
 
Ubishi wa kitoto, tafuta kazi jombaa.
 
Ubishi wa kitoto, tafuta kazi jombaa.

Hoja huwa inabishwa kwa hoja sio kwa matusi.

Mimi nimesoma bible knowledge O level na Divinity A level.

Hunidanganyi chochote kuhusu biblia.

Na hata uislam na Quran yake naujua jua kupitia somo la Anthropology
 
Hoja huwa inabishwa kwa hoja sio kwa matusi.

Mimi nimesoma bible knowledge O level na Divinity A level.

Hunidanganyi chochote kuhusu biblia.

Na hata uislam na Quran yake naujua jua kupitia somo la Anthropology



Kwa hiyo huamini kwamba Biblia ni Maandiko Matakatifu ya Mwenyezi Mungu?

Kumbe tunajadiliana na Pagan?

Sasa kama ni hivyo haina haja ya kuendelea na majadiliano iwapo kumbe kwenye msingi wa imani hupo.

Kama huamini hivyo vitabu vitakatifu kuwa ni maneno ya Mungu Basi hiyo divinity yako ulisoma ili upate credits kwenye matokeo ya mtihani lakini hukuwa na nią ya kujifunza na kupokea Kweli ya Mungu.

Ulisoma kama somo la kawaida la kitaaluma tu basi.
 

Nimekuomba ulete ushahidi kama biblia imeandikwa na Mungu. Umeshindwa kuleta ushahidi
 
Naona afadhali ya uongo wa mganga wa kienyeji.

Mimi familia imetawanywa na mchungaji na waombezi.

Wanasisitiza kuwa kaka yetu ni mchawi kwa kuwa anafanya biashara yenye masharti ya kuua.

Wenye akili fupi wameamini na kujitenga vibaya.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Wapi imeandikwa kwamba Mungu aliandika biblia?
Waandishi wa biblia wamejitaja kwa majina na hakuna sehemu yoyote wamesema Mungu ndo aliandika.
Ila amri kumi ndo Mungu alimpa Mussa.
Acha kuchanganya na Quran ambayo iliandikwa na Allah na akateremshiwa Muhammad.
 
Biblia ipo Injili,Zaburi,Taurati(TORAH),kwa mujibu wa Uislamu,hivyo vitabu vya Mungu,tatizo linakuja kwenye tafsiri kutoka vitabu vya lugha ya asili kuja lugha nyingine,ndi mkanganyiko unakuja hapo.Qur'an ili iwe ni Qur'an,mpaka iwe kwenye lugha ya asili,ikitafsiriwa,inatwa tafsiri ya Qur'an.
 
Poleni sana aisee wachungaji nao janjajanja sikuhizi
 
Unajuaje kama ndugu ni mchawi ?

Diagnosis ya uchawi inafanywa na mashine gani ? Ama kipimo gani ?
watu wa hivi mpaka yamkute mtu unaemfahamu ndio huwa mnaamini. uchawi upo, ndio maana kuna watu huamua kukata mazoea yaliyozidi na watu
 
watu wa hivi mpaka yamkute mtu unaemfahamu ndio huwa mnaamini. uchawi upo, ndio maana kuna watu huamua kukata mazoea yaliyozidi na watu

hakuna uchawi. kukata mazoea na watu ni mbinu tu ya ku avoid problems, hata kwenye elimu ya Human psychology wanafundisha mbinu hiyo.

ukikata mazoea na watu unakuwa na privacy kubwa. hiyo privacy ndio inakuepusha na majanga maana mtu hawezi kuharibu asichokijua. hata mwizi hawezi kuingia kwenye nyumba ambayo haijui ramani yake ndani ikoje, kwenye nyumba wanaishi wangapi na wanatoka saa ngapi na wanarudi saa ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…