Wageni rasmi wenye tija

Wageni rasmi wenye tija

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nimejaribu kuhudhuria sherehe mbali mbali kwa miaka kadhaa; sherehe za mashule, vyuo, mambo ya ujenzi n.k

Na katika hizo sherehe nimeona tofauti kubwa kwa wale wageni rasmi, wanaopewa nafasi hizo.

Katika risala, huwa kuna kipengele cha kuelezea changamoto walizonazo, na zinazoitaji utatuzi. Na changamoto nyingi, huwa ni rasilimali fedha. Wanaweza kusema, tunaitaji kumalizia jengo letu; ambalo mpaka sasa linahitaji milioni 200 ili liweze kukamilika.

Sasa hapa, ndipo wageni rasmi wanapo tofautiana. Kwa wale wageni rasmi walio ajiriwa, wakiwemo na wana siasa; wengi huishia kutoa ahadi, au watasema; tutajaribu kulifanyia kazi kwenye sera au tutatafuta wadau mbali mbali n.k

Ila kwa mgeni rasmi mfanyabiashara, yeye huenda moja kwa moja kwenye utatuzi, atasema; hilo jengo niachie mimi nitalimaliza ndani ya mwezi mmoja n.k

Sasa kwa wale wanaoanda, sherehe mbali mbali inabidi wawe makini na wageni rasmi wanao waalika, ili kuweza kutatua changamoto zao.​
 
Back
Top Bottom