Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Sisi uonevu umezidi,yaani ukigundua kitu halafu hujasoma wasomi lazima wakuwekee zengwe.
Ila ushauri wangu Kwa wagunduzi wanapogundua kitu wakitupie moja Kwa moja kwenye mitandao ya jamii
Nalog off
Mkuu
Autodidact ni watu wenye uwezo wa kujifunza vitu wa pekee yao (self-taught), kuna watu wamejaliwa kipaji hichi cha kujifunza wao pekee yao. Watu hawa hua hawahitaji mwalimu awasimamie au kuwafunza vitu ili waelewe bali wanachohitaji ni kujua is where to find right material for them to read…Watu hawa ukilazimisha wafundishwe na mwalimu kamwe hawawezi kuelewa, wataishia kufeli tu.

Mara nyingi watu wenye low latent Inhibition ndio hua na hali hii pia ya Autodidactism, wanasayansi wengi hawakupita vyuoni bali walitumia LLI yao kujifunza vitu na kugundua mambo mengi mapya..!

Baadhi ya watu maarufu ambao walikua ni autodidact ni galileo, Da vinci, Euclid, Socrates, Plato, Pythogras, nk.. zaidi unaweza kutizama orodha hapa

Hebu niambie ni chuo gani alisomea Archimedes,Da Vinci nk.
Basi tu waafrika tumelaanika kwa matendo yetu
 
Mimi jameni Nina waswasi na huu weusi wetu... Haiwezkan kila shida zetu! Kutengwa! Uchawi(kuna mtu uchiz aliupatia eapoti alkuw anaend ulaya scholarship) had Leo anaokot makopo pale mnaz mmoja. Umaskin w kutupwa alaf tuna 60 year tok uhur na bado mpaka Leo tunalaum wazungu [emoji28]
Tusbirin kufa tu tutengenezew mpak elimu na historia yetu wenyew.. watu weusi dah! Mi siamin Kam wamisri hao w miaka hiyo ni weusi mkuu
 
Hapo kwenye maandishi umenena vyema.
Hope hata Yale mapango yetu ya Tanzania yakiyochorwa maandishi na picha ambazo watz tumeshindwa kuyatafsiri yana maana ndani yake.

Kuna Yale maandishi/michoro ya kule kondoa sijui Kolo pana Elimu ya kale pale.
Yes pamoja na kusoma sayansi but napenda historia nimefatilia maandishi yakale ktk vitabu vya zamani Sana nimebahatika kupata kalamu za kizamani zipatazo 100+
 
Mbona jibu ni simple, empire zina raise and fall. zikifa zinaacha baadhi ya alama zake. Hizi alama ni kama majengo monument : pyramid, great wall, hanging garden, aztec, na utamaduni. Katika utamaduni na ustaarabu wa kijiongoza hapa ugiriki ndipo utakapo mwona. Demokrasia ilizaliwa athen, olympic tornament zilianza huko kwao katika milima mount olympia.
Na inapoanguka empire moja nyingine inasimama it just a circle ulimwengu unapitia we have to accept. Alipotoka ugiriki alikuja Rome alikaa ambaye alikop tamaduni karibia zote za ugiriki kasoro jeshi.
 
Yamewakuta..yaliyotukutta sisi kutoka kwa wazungu...
 
Hii kwako mr Da'Vinci na kwa wengine wenye mitazamo eti wamisri walikuwa weusi tii. sijui ni misingi gani mnabase your claim. Nadhani mnatumia misingi ya ubara na urangi, eti kwa kuwa misri ipo pamoja na bara la Afrika, eti kama njia ya kuonyeaha mtu mweusi nae yumo. Si sawa kufanya hivyo tafuta ukweli na ukweli atakuweka huru.
Mimi napinga kuwa wamisri wa kale walikuwa weusi kwa kutumia kanuni za kigeographia. Yatupasa kujua watu katika sayari yetu hapo kale walikuwa wametenganishwa kwa namna mbalimbali: kuna bahari,kuna mito, kuna mabonde ya ufa, kuna milima, na pia kuna majangwa. Hili la mwisho jangwa watu huwa hawazingatii kabisa lakini sisi waafrika rangi nyeusi twapaswa kujua the great sahara desert kama moja wapo wa ukinzani uliotukinga na maendeleo kwa miaka mingi hapo nyuma.
Ukitazama ramani yako chini ya jangwa la sahara ndio kuna watu weusi juu yake kuna watu rangi nyeupe. Ukiuliza kwa nini ni kwa sababu ilikuwa haiwezekani enzi hizo weupe kushuka chini na weusi kwenda juuu. In short wamisri wenyewe walishindwa kufwatilia chanzo cha mto nile kutokana na ukakasi uliletwa na jangwa. Imagine wamisri wangefika Victoria si wangetuabudu kama miungu wao na kutupa ujuzi wao wote. Mbali na kuwa kizuizi kikuu pia ilipelekea kusini kutokupata farasi na farasi ndio ilikuwa yaendesha uchumi kipindi hicho. Sasa tunapata taabu sana kwa sababu kuna baadhi ya stage wafrika weusi hatujapitia katika maendeleo yetu.
 
Wewe umegundua nini mpaka sasa?
 
Nyie endeleeni kusema nani kagundua na hajagundua,, Alafu mbona siwaelewi mara tusimtukuze mzungu,, wakati vitu vyote unavyotumia ametengeneza White people,, white people atabaka kuwa hivyo hivyo na black people mtabaki na akili zetu nyeusi tiii kama rami au oili chafu,,
 
Maelezo yako mazuri kuna point ndani yake ila bado hujaonyesha ni vipi wamisri enzi hizo hawakua weusi.
Nipe facts mkuu zinazoonyesha wamisri walikua weupe...
Ahsante kwa hoja yako mkuu
 
Hakua smart... Ila kwenye top ten ya watu maarufu yeye ni namba mbili baada ya Yesu.
Kwhy alikuwa average au foolish?
Tuachane Na Hayo sehem Gani hapa Kigoma naweza kupata watoto wa Congo Na Rwanda niwe najisevia?Nataka kuoa huku Na Sina rafiki
 
Maelezo yako mazuri kuna point ndani yake ila bado hujaonyesha ni vipi wamisri enzi hizo hawakua weusi.
Nipe facts mkuu zinazoonyesha wamisri walikua weupe...
Ahsante kwa hoja yako mkuu
Watu weusi ni watu gani? Watu wote wa Afrika siyo jamii moja, kuna jamii nyingi tofauti ambazo hazina uhusiano wa kinasaba.
 

Kwa maana hiyo wewe hata Socrates na Aristotle hukuwahi kuwasikia?

duuuu aisee kazi Ipo Plato ni mwanafalsafa mgiriki aliishi miaka mingi nyuma kabla ya Yesu na sio Ponsio Pilato mrumi ndugu!
Wayahudi tangu walipodai watawaliwe na wafalme ukirejea 1sam 8:1-9,Mungu aliruhusu wafalme wawatawale wakianzia na Saul, Daud na baadaye Sulemani.Hawa wote walianza kazi zao vizuri lakini polepole mwishoni mwa kazi zao hawakuweza kuendelea kuyashika maagizo ya Bwana na hivyo wakalifanya taifa zima kupotea njia.Mambo kama haya ndiyo hatimaye yanawapeleka waisrael utumwani mnamo mwaka 587 KK.

Ilipofika mwaka 63 KK nchi ya wayahudi ikiwa chini ya utawala wa Aristobulus II, ilitekwa na warumi waliokuwa wakiongozwa na Pompey.Warumi hawa waliitawala nchi ya wayahudi kutoka Roma.Wafalme walioitwa Makaisari walikaa Roma na nchi zote walizoziteka walizigawa katika mikoa ambayo iliwekwa chini ya magavana. Hawa magavana waliweka wafalme wa kienyeji. Kumbe, hawa wafalme wa kienyeji walitawala chini ya gavana wa kirumi.Ni kama kwa mfano jinsi wakoloni hapa nchini kwetu walivyoteua machifu kuongoza badala yao enzi za ukoloni.Hapa naweza kukutajia magavana wachache kati ya wengi wanaojulikana kama Ponsio Pilato,Titus,Felix,Festus n.k
Kumbe jina Herode ni jina la ukoo uliotawala nchi ya Palestina kwa muda wa miaka 47 kabla ya Kristo na miaka 79 baada ya kuzaliwa Kristo.Hawa niliowataja walikuwa wafalme wa kienyeji waliowekwa kutawala badala ya Warumi na kwa kweli hao ndio waliotumia jina Herode.

Pia, watawala hawa yaani maherode, walitoka katika shina moja yaani baba yao alikuwa anaitwa Antipater mtawala wa Idumea, kusini mwa nchi ya Palestina ambaye alikuwa amechaguliwa na Warumi kutawala eneo hilo. Huyu alipata kuzaa mtoto mmoja anayejulikana kama Herode Mkubwa.Huyu Herode Mkubwa,alipewa nafasi ya kutoka katika nchi yake kuja Palestina kwa Wayahudi na kutawala katika mkoa wa Galilaya baada ya kifo cha baba yake na ingawa mwenyewe hakuwa myahudi akatawala tangu mwaka 37-4KK.Wayahudi hawakumpenda mtu huyu kutokana na sababu mbili kuu. Kwanza ni kwa sababu hakuwa myahudi hivyo walijisikia vibaya kutawaliwa na mtu ambaye hakutoka katika taifa lao. Sababu ya pili ya kutompenda ni kwamba Herode huyu alikuwa ni katili sana.

Ukatili huu unatokana na ukweli kwamba aliyapata madaraka kwa ujanja. Herode huyu alijua kwamba wengi hawampendi hivyo akajitahidi kuhakikisha kuwa wote wanaompinga anawaangamiza rej Lk 19:27.Tunaambiwa kwamba aliwaua hata ndugu zake na watoto wake mfano akina Antipater, Alexander na Aristobulus walioonekana vinara wa kumpinga. Ukisoma pia Mt 2:16-18 pale wanatajwa watoto mashahidi waliouawa katika harakati za kuhakikisha kwamba mtoto Yesu anauawa pia ingawa hakufanikiwa kumuua Yesu kwani tayari alikuwa ametoroshwa toka Bethlehemu.

Kila mtu anayo mazuri na mapungufu. Herode Mkubwa naye kafanya kitu fulani ambacho kiliwafurahisha Wayahudi pamoja na ukatili wake.Yeye ndiye aliyejenga hekalu la Yerusalemu,hekalu lililokuwa kubwa na zuri kiasi kwamba wayahudi hao hao wakawa wanasema kwamba kama mtu alizaliwa hadi akafa bila kuliona hekalu lile,basi mtu huyo atambue kwamba hakuwahi kuona kitu chochote kizuri hapa duniani.Kumbe huyo ndiye Herode aliyetishia maisha ya Yesu maana hakupenda aje mtu yeyote atakayeitwa mfalme tofauti na yeye.Aliposikia kwamba amezaliwa mtoto ambaye ni mfalme alijua mtoto huyo anataka kurithi ufalme wake hivyo alifanya lolote awezalo ili kuhakikisha anammaliza bila kujua kwamba ufalme wa mtoto Yesu haukuwa wa kidunia.
Herode Mkubwa naye alikuwa na watoto. Kabla ya kifo chake aliacha wosia ulioagiza kwamba nchi aliyoitawala igawiwe kati ya watoto wake watatu yaani Archelaus, Herod Antipas na Philip.

Katika mgao huo, Archelaus akawa mtawala wa Yudea na Samaria na kwa kweli hii ni karibu nusu ya nchi yote ya wayahudi kwani alitawala mikoa miwili. Herode huyu ndiye alikuwa mtawala kipindi kile Yoseph na Maria waliporudi kutoka Misri rej Mt 2:22.Hata hivyo alishindwa kumudu uongozi wa mikoa hiyo na hivyo Warumi wakamtoa na kumweka Pontio Pilato kuwa mtawala badala yao. Mtoto wa pili yaani Herode Antipas alipewa kutawala mkoa wa Galilaya tangu mwaka 4KK-39 BK.Huyu alitawala wakati Yesu alipokuwa akitembea huko na huko kuhubiri Lk 3:1,MK 6:4 Zaidi sana,huyu ndiye Herode aliyekemewa na Yohane Mbatizaji alipomwoa Herodia mke wa kaka yake Philip rej Mt 14:1-5,Mk 6:14-29,ndiye anayeitwa na Yesu mbweha Lk 3:32,na Ndiye aliyekutana na Yesu wakati wa mateso Lk 23:7-12. na mwisho ndiye aliyemuua mtume Yakobo na kumfunga mtume Petro Mdo 12:1-5.
 

Hilo hekalu alilojenga na lile la mfalme Sulemani lipi ni bora zaidi. Naongelea hekalu ambalo Newton alitumia muda mwingi akilifikiria na akifanyia utafiti akizani kuna siri atagundua, hekalu ambalo mpaka leo wayahud wanasali kwenye msingi wake
 
Maelezo yako mazuri kuna point ndani yake ila bado hujaonyesha ni vipi wamisri enzi hizo hawakua weusi.
Nipe facts mkuu zinazoonyesha wamisri walikua weupe...
Ahsante kwa hoja yako mkuu
Watu weusi misri wameingizw nautumwa mkuu.. ndo mana ni minority group pale misri' Kam ulivyo kwao minority in Asia, America n europe' pili, wazawa w misri Kam wangekuwa weusi lazima tuwe n tresi ni Lin hasa muarab aliingia pale na kwa hoja zipi has muarab akatwaa uongoz n uwingi was wat wake kias Cha mzawa kukos madaraka yote mpak kuwa mtumwa
Alaf hizi za michoro kuonekan n pua kubwa sijui au kuonekan miungu yenye rangi nyeus ni hoja zeny dhana ya kuuikweza tu uafrika sabb (north Africa yenyew) tukisem misri weusi lazima tuelezee imekuaje misri na sio north yote!?vip!? na kw nn Libya, Tunisia na moroko Arabs pia!? hao weusi walitolewaje!? .North yote mpak wazawa Afrikan kuw minorities maeneo hayo!?
Toa elimu hiyo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…