Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Mkuu ukiachana na imani(Si kwamba nakejeri) Yesu alikuwa na uwezo gani mpaka wewe kumchukulia moja ya Watu wenye akili Zaidi.
Yesu anamzidi hata Isaac Newton kweli.
Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe.

kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hzamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watu wote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.
 
Wapo, ila siku hizi hawana promo tena, kila zama na zama zake...
 
Heshima yako mkuu!
Kwa historia ulipaswa upewe PHD ya heshima ila nashangaa wamempatia mh Kasheku Musukuma wanawaacha watu wanaostahili.
 
Zaid ya biblia ni kitabu gani nisome niweze kupata hii historia ya kale mkuu?
 



Alikuwa mtu mweusi ..
Egyptian wote walikuwa blacks
Hadi kina Ramses..
 
Zaid ya biblia ni kitabu gani nisome niweze kupata hii historia ya kale mkuu?
Mkuu huu uzi una mwendelezo wake, nilijikita zaidi kwenye anguko la misri. Ngoja nikutag huko
 
Mkuu ukiachana na imani(Si kwamba nakejeri) Yesu alikuwa na uwezo gani mpaka wewe kumchukulia moja ya Watu wenye akili Zaidi.
Yesu anamzidi hata Isaac Newton kweli.
1.Alitembea Juu ya Maji.
2.Alimfufua Lazaro.
3.Alilisha watu elfu tano kwa Samaki wawili na Mikate Mitano na Mabaki ya samaki na mikate yakajaza vikapu 12.
4.Aliponya Vipofu,wakaona na Viziwi Wakasikia.
5.Aligeuza Maji kuwa Pombe kwenye harusi kule kana.
6.Alipokata roho pazia la hekalu lilipasuka na Wafu wakafufuka.
7.Mwenyewe alifufuka.

Sio isaack Newton tu bali hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuikaribia hiyo CV.
 
Zaid ya biblia ni kitabu gani nisome niweze kupata hii historia ya kale mkuu?
Tembelea Maktaba za Kale hasa middle East utapata vitabu vingi tu mfano injili ya Nicodemu.
Hivi vichache walivikusanya watu wa dini na kuamua kuvitengenezea Kitabu kimoja kiitwacho Biblia.Sio Vitabu vyote vilivyoandika historia ya Yesu viliunganishwa kwenye Biblia.
 
Wachina noma, marcopolo baada ya kurudi kwao akawa anawasimulia kuhusu china nyumba, matumizi ya pesa, icecream na mengine lakini wakawa hawaamini maana ilikuwa ni mbele ya wakati na hawakuwahi sikia vitu kama hivyo
 
Wachina noma, marcopolo baada ya kurudi kwao akawa anawasimulia kuhusu china nyumba, matumizi ya pesa, icecream na mengine lakini wakawa hawaamini maana ilikuwa ni mbele ya wakati na hawakuwahi sikia vitu kama hivyo
Umemtaja Marco Polo umenikumbusha huyu jamaa na Silk road. Wachina wamemtemgenezea muvi nyingi sana..Ila Japan na England naziheshimu sana hizi nchi, ni visiwa tu ila mambo yake noma sana. Sasa hivi ndio wamepunguza makali
 
Asante kwa ufafanuzi Mzuri.
Lakini kulingana na sifa ulizi taja yesu naona mengi alifanya Mazingaombwe (Miujiza) wala hakuna ugunduzi alio ufanya. Maana angefanya ugunduzi mpaka sasa alichokuwa akifanya angeacha walau Formula ili na wengine wakifanye.

Je, kama yesu alifanya hayo yote na hakuna alio waachia urithi (kuendeleza) miujiza hiyo nitakuwa ninakosea kusema alikuwa Mbinafsi? NB: si kwamba nakufuru ila ni mawazo tu.

Hitimisho kulingana na Miujiza ya Yesu hatolinganishwa na watu wasio na miujiza kama akina Galilei Galileo, Newton, Aristottle, Faraday, Archimedes, n.k hivyo alipaswa kushindanishwa na watenda miujiza wenzake kama Ngh'wana Malunde (Wa kabila la kisukuma).
 
Asante, ukiweza pitia kidogo comment #175
Labda utanipa elimu zaidi.
 
Hao wengine kazi zao zinagusa jamii yote ila kwa Yesu hapana umemuweka kishabiki tu hana lolote kwa Yesu ana faida gani kwa watu wasiokuwa na dini au ana faida gani au wanaofata dini ya budha au ana faida gani kwa dini za kigiriki utakuja kuona hana faida kihivyo pia hakuna jambo kubwa alilofanya likagusa dunia nzima huyo hawezi kuwa na akili dunia nzima au genisus maana yake ufalme wake Yesu upo kwa wakristo na waislam tu wayahudi hawamtambui kitu wanaona ana laana ya torati
Ila mtu kama tesla kazi yake inaonekana kila mtu Anajua uwe huna dini au unayo itakugusa tu huyo unaweza sema mtu mwenye akili ila sio huyo Yesu wenu ambaye ufalme wake kwenu wakristo na waislam
 
@Iblis Bin Shetan
 
Opium ndiyo hutengeneza anaesthesia au nusu kaputi anayopewa mgonjwa na kuruhusu tiba ya upasuaji iendelee bila mgonjwa kusikia maumivu.
Ahsante kwa kunijuza!
Ila ningependa kuuliza pia, historia inaonyesha kwamba upasuaji ulianzia misri, maana vifaa vya upasuaji vimegunduliwa huko!
Je wao walitumia nini wakati wa kufanya upasuaji?? Au ndio ilikua live bila ganzi, Ningependa kujua historia ya upasuaji maana sifahamu sana maswala ya utabibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…