Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
acha kuwafananisha hao viumbe wengine na Yesu
 
Wanajeshi wa ugiriki (Sparta) walijulikana kama Hoplites, ambapo hoplites walikua wanajeshi wenye ngao ya duara,mkuki na upanga mfupi wa chuma. Kwenye vita walikua wanatumia mfumo wa vita unaofahamika kama phalanx ambapo hoplites alikua anasima mbele ya mwenzake kisha anatumia ngao yake kujilinda na kumlinda mwenzake kama likitokea shambulio la mbele. Kama phalnx ikivunjika au adui akishambulia kutoka upande wa kushoto au kulia basi inakua hatarii zaidi kwa Hoplites
Mwanzoni mwa karne ya 5 BC nchi ya Persia ilikua inafanya uvamizi nchini ugiriki ,lakini jeshi lile la vile vimiji zaidi ya mia vilivyoungana kijeshi viliirudisha nyuma jeshi la Persian lilipotaka kuvamia katika vita inayojulikana kama Battle of Marathon ilikua mwaka 490 B.C chini ya mfalme Darius I wa Persia . Miaka kumi baadae mtoto wa Darius aitwae Xerxes I (519-465 B.C.), kwa mara ya pili alianzisha uvamizi nchini Ugiriki.

Chini ya mfalme Xerxes I, jeshi la Persian lilivamia ugiriki kupitia pwani ya mashariki akishirikiana na jeshi la maji la Persian lililokua linapita pwani. Ili kufika sehemu walipokua wanaeleka katika eneo linaloitwa Attica ambapo pia attica ilikua ni mji unaoongoozwa na Athens, Jeshi la Persia ilitakiwa lipite sehemu moja ya pwani inayoitwa Thermopylae (au “Hot Gates,” ilijulikana hivo kwakua ilikua karibu na chemichemi ya sulfur). Katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 480 B.C., Leonidas alikua anaongoza jeshi la wat 6,000 mpaka 7,000 kutoka miji mbalimbali iliyopo ugiriki ukijumuisha na wanajeshi 300 kutoka katika mji wake wa Sparta Aliongoza jeshi hilo kuziwia jeshi la Persia kupita ile sehemu inayoitwa Thermopylae.

Wananchi wa Sparta walikua na miungu yao walioiabudu, kulikua kuna mtu ambae alikua kama nabii wao ambae alikua anawapa maagizo wananchi kutoka kwa miungu hiyo. Kabla ya kwenda vitani Leonidas alienda kuonana na huyo nabii ili ampe maono kuhusu vita hiyo anayokwenda kupambana, nabii alimkataza kua asiiende atapoteza maisha ya wengi ni bora ajislimishe kwa jeshi la Persia, leonida alikata kata kata kua hataweza kujisalimiisha lazima akawaziwie pale kwenye hot gate, walimsihi sana na kumshauri lakini alikataa na kuituna miungo yake
Leonidas aliongoza jeshi lake hadi pale hotgate akiamini kua jeshi la Persia lazima lipitie pale alipambana nao na kuwaua wanajeshi wengi wa Persia kisha akajenga ukuta kwa kutumia maiti za wale wanajeshi.

Leonidas akiwa hajui kumbe jeshi lingine lilipita njia inayopita milimani hivyo wakatokezea nyuma ya jeshi la leonida, baada ya kugundua hilo makamanda walimshauri kua ni bora wajisalimishe maana washazungukwa ila Leonidas alikataa kabisa akasema sharia ya nchi ya Sparta hairuhusu kujisalimisha ni bora afe pale. Makamanda kutoka ile miji mbalimbali walichkua majeshi yao na kumuacha Leonidas akiwa na wanajeshi 300 tu!
Akiwa na wanajeshi 300 tu Leonidas alipambana na jeshi la zaidi ya watu 15000, mwisho alizidiiwa na kuuwawa..walimkata kichwa .
Katika movie bora kabisa kwangu ya vita ni 300 ni bonge la movie
 
Katika movie bora kabisa kwangu ya vita ni 300 ni bonge la movie
300 film by Zack Snyder ni story ya kweli kabisa iliyotokea. Ni kama vile ilivyo series ya Spartacus.
Leonidas alikua kiongozi mzuri ila hashauriki Ego yake alishindwa kuimeza. Mwisho kabisa kama angemsikiliza yule mlemavu yasingempata
btw warumi ndio waligundua threesome ila ilikua ya wanaume watupu. Wapuuzi wanapenda sana mapenzi ya jinsia moja
 
Spartacus ile series sio ya kuangalia na wakwe ama watoto kuna ujinga mle hatari ila ni bonge la series kuna ujumbe mkubwa sana mle kwa watu tunaopenda history
 
Nini kiliwakuta waTanzania? Hamna wapambanaji Kama akina kinjikitile,milambo,mkwawa na abushiri? Usiwazungumzie wenzako
Hao si inajulikana wazi jamii waliachana na tamaduni zao kutokana na matokeo ovu ya ile mkutano kule Berlin
 
Spartacus ile series sio ya kuangalia na wakwe ama watoto kuna ujinga mle hatari ila ni bonge la series kuna ujumbe mkubwa sana mle kwa watu tunaopenda history
History ni ya kweli kabisa, ngono zilizomi sio halisi lakini ila mkuu unakaaje na mama mkwe mnaangalia series/muvi tena za kizungu??
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Mkuu ukiachana na imani(Si kwamba nakejeri) Yesu alikuwa na uwezo gani mpaka wewe kumchukulia moja ya Watu wenye akili Zaidi.
Yesu anamzidi hata Isaac Newton kweli.
 
Mkuu ukiachana na imani(Si kwamba nakejeri) Yesu alikuwa na uwezo gani mpaka wewe kumchukulia moja ya Watu wenye akili Zaidi.
Yesu anamzidi hata Isaac Newton kweli.
Kwani hujui Isaac mwenyewe anasanda Kwa Yesu
 
Back
Top Bottom