Wanajeshi wa ugiriki (Sparta) walijulikana kama Hoplites, ambapo hoplites walikua wanajeshi wenye ngao ya duara,mkuki na upanga mfupi wa chuma. Kwenye vita walikua wanatumia mfumo wa vita unaofahamika kama phalanx ambapo hoplites alikua anasima mbele ya mwenzake kisha anatumia ngao yake kujilinda na kumlinda mwenzake kama likitokea shambulio la mbele. Kama phalnx ikivunjika au adui akishambulia kutoka upande wa kushoto au kulia basi inakua hatarii zaidi kwa Hoplites
Mwanzoni mwa karne ya 5 BC nchi ya Persia ilikua inafanya uvamizi nchini ugiriki ,lakini jeshi lile la vile vimiji zaidi ya mia vilivyoungana kijeshi viliirudisha nyuma jeshi la Persian lilipotaka kuvamia katika vita inayojulikana kama Battle of Marathon ilikua mwaka 490 B.C chini ya mfalme Darius I wa Persia . Miaka kumi baadae mtoto wa Darius aitwae Xerxes I (519-465 B.C.), kwa mara ya pili alianzisha uvamizi nchini Ugiriki.
Chini ya mfalme Xerxes I, jeshi la Persian lilivamia ugiriki kupitia pwani ya mashariki akishirikiana na jeshi la maji la Persian lililokua linapita pwani. Ili kufika sehemu walipokua wanaeleka katika eneo linaloitwa Attica ambapo pia attica ilikua ni mji unaoongoozwa na Athens, Jeshi la Persia ilitakiwa lipite sehemu moja ya pwani inayoitwa Thermopylae (au “Hot Gates,” ilijulikana hivo kwakua ilikua karibu na chemichemi ya sulfur). Katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 480 B.C., Leonidas alikua anaongoza jeshi la wat 6,000 mpaka 7,000 kutoka miji mbalimbali iliyopo ugiriki ukijumuisha na wanajeshi 300 kutoka katika mji wake wa Sparta Aliongoza jeshi hilo kuziwia jeshi la Persia kupita ile sehemu inayoitwa Thermopylae.
Wananchi wa Sparta walikua na miungu yao walioiabudu, kulikua kuna mtu ambae alikua kama nabii wao ambae alikua anawapa maagizo wananchi kutoka kwa miungu hiyo. Kabla ya kwenda vitani Leonidas alienda kuonana na huyo nabii ili ampe maono kuhusu vita hiyo anayokwenda kupambana, nabii alimkataza kua asiiende atapoteza maisha ya wengi ni bora ajislimishe kwa jeshi la Persia, leonida alikata kata kata kua hataweza kujisalimiisha lazima akawaziwie pale kwenye hot gate, walimsihi sana na kumshauri lakini alikataa na kuituna miungo yake
Leonidas aliongoza jeshi lake hadi pale hotgate akiamini kua jeshi la Persia lazima lipitie pale alipambana nao na kuwaua wanajeshi wengi wa Persia kisha akajenga ukuta kwa kutumia maiti za wale wanajeshi.
Leonidas akiwa hajui kumbe jeshi lingine lilipita njia inayopita milimani hivyo wakatokezea nyuma ya jeshi la leonida, baada ya kugundua hilo makamanda walimshauri kua ni bora wajisalimishe maana washazungukwa ila Leonidas alikataa kabisa akasema sharia ya nchi ya Sparta hairuhusu kujisalimisha ni bora afe pale. Makamanda kutoka ile miji mbalimbali walichkua majeshi yao na kumuacha Leonidas akiwa na wanajeshi 300 tu!
Akiwa na wanajeshi 300 tu Leonidas alipambana na jeshi la zaidi ya watu 15000, mwisho alizidiiwa na kuuwawa..walimkata kichwa .