Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Ahsante kwa kunijuza!
Ila ningependa kuuliza pia, historia inaonyesha kwamba upasuaji ulianzia misri, maana vifaa vya upasuaji vimegunduliwa huko!
Je wao walitumia nini wakati wa kufanya upasuaji?? Au ndio ilikua live bila ganzi, Ningependa kujua historia ya upasuaji maana sifahamu sana maswala ya utabibu
 
Ahsante kwa historia mkuu sky

😅😅😅Mashanuo, sijasikia hili neno siku nyingi. Utakua Typical mswahili
PS. Naomba kujuzwa kwanini Mashanuo hayo yawe ushahidi wa weusi wa Wamisri... There's some pieces I can't put together
Moja ya ushahidi mmoja wapo ni mashanuo ya mbao za mpingo waliyoyumia ambayo mpaka leo yapo katika majumba ya makumbusho Cairo.

View attachment 2126837
 
Ahsante kwa historia mkuu sky

😅😅😅Mashanuo, sijasikia hili neno siku nyingi. Utakua Typical mswahili
PS. Naomba kujuzwa kwanini Mashanuo hayo yawe ushahidi wa weusi wa Wamisri... There's some pieces I can't put together
Nyinyi mliozaliwa baada ya utawala wa Mzee Ruksa hamjui maisha tuliyoishi baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza miezi kumi na nane ya kufunga mikanda. Hii ilikuwa ni baada ya Vita ya Kagera.
 
Nyinyi mliozaliwa baada ya utawala wa Mzee Ruksa hamjui maisha tuliyoishi baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza miezi kumi na nane ya kufunga mikanda. Hii ilikuwa ni baada ya Vita ya Kagera.
Aisee nimezaliwa muhula wa kwanza wa mzee rukhsa ukiwa unaishia,wakati utawala wake unaisha nilikua kama 6yrs hivi. So Kwakweli sijui ningependa unielezee hiyo miezi 18 ya kufunga mkanda ilikua ya kufanya nini! Na kwanini??
 
Aisee nimezaliwa muhula wa kwanza wa mzee rukhsa ukiwa unaishia,wakati utawala wake unaisha nilikua kama 6yrs hivi. So Kwakweli sijui ningependa unielezee hiyo miezi 18 ya kufunga mkanda ilikua ya kufanya nini! Na kwanini??
HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA:

Nyerere ahaha kutafuta marafiki na silaha.

#Sehemu #ya - 8

Jana tuliona Mwalimu Nyerere alivyoanzisha kambi za mafunzo ya kijeshi kwa Waganda huko Tarime mkoani Mara.Kambi ile likuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wapiganaji 1,200,pia aliwataka Waganda wengine wakiwemo Robert Serumaga,Roger Makasa na Andrew Adimola wa chama cha Ugandan Redemption and Reconciliation Union.

Serumaga ambaye alikuwa mwandishi aliukimbia utawala wa Idi Amin mwaka 1977.Adimola alikuwa waziri kabla hajakimbia, mwingine ni Aleker Ejalu.

Nyerere aliwasihi wote hawa wahamasishe wapiganaji.

Sasa endelea........

Hadi ilipofika Krismasi mwaka 1978,zaidi ya wafuasi 50 wa watu hawa wakawa wamewasili.Wiki chache baadaye wakawasili wengine zaidi ya 100 tayari kwa mafunzo.
Januari 1979 Serumaga na Ejalu walimwambia Nyerere kuwa katika miji ya Kampala na Jinja kuna maelfu ya wanajeshi wanaompinga Idi Amin na kwamba wakipata msaada kidogo tu wataasi.

Nyerere alikubaliana nao,akaruhusu Waganda 200 wapelekwe Uganda kwa kazi hiyo,50 kwa ajili ya Serumaga na Ejalu na 150 kwa ajili ya Tito Okello. Lakini walipokaribia ufukwe wa Ziwa Victoria upande wa Uganda baadhi ya mashua zao zilizama,baadhi walifanikiwa kurejea Mwanza.

Muda mfupi baadaye Ejalu na Serumaga wakatuma mashua za doria ziwani,lakini walipowasili karibu na mji wa Jinja wote walikamatwa na kuuawa.
Baada ya matukio haya,kambi ya mafunzo ya Tarime ikafungwa rasmi.

Kwa upande wa uchumi wa nchi, bidhaa zilianza kupaa bei.Hii ilitokana na kuongezeka kwa kodi ili kulipia mahitaji ya vita.Novemba 15, 1978, jarida la Africa Contemporary Record 1978-1979 lilimnukuu Waziri wa Fedha wa Tanzania, Edwin Mtei akitangaza kuwa vita vimeifanya Serikali kuongeza kodi kwa bidhaa za walaji.

Vita ilipoanza kupamba moto,Tanzania ilianza kuwatafuta marafiki na washirika wake,lakini ikaonekana kusingekuwa na msaada mkubwa kutoka kwao.Rafiki wa kwanza ambaye Tanzania ilimwona alikuwa ni Jamhuri ya Watu wa China (RPC).

Kwa mujibu wa kitabu cha "Routledge Handbook of Chinese Security" kilichohaririwa na Lowell Dittmer na Maochun Yu, mwaka 1963 kiongozi wa China, Mao Zedong alianzisha falsafa mpya ya kimkakati aliyoiita “mapinduzi ya dunia”.

Nadharia yake akaiita “Two Middle Areas” (liangge zhongjian didai) ambayo aliamini kuwa katikati ya mataifa mawili makubwa Marekani na Urusi kulikuwa na maeneo mawili makubwa katikati yake. Eneo la kwanza lilikuwa ni baadhi ya nchi za bara la Asia,Afrika na Amerika ya Kilatini ambazo ama zilikuwa tayari zimejipatia uhuru au zilikuwa katika harakati ya kujipatia uhuru.

Kwa kufuata falsafa hiyo, mwaka 1964 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhou Enlai aliitembelea Tanzania. China ilitoa misaada na mafunzo ya kijeshi.Hadi mwishoni mwa 1978, wakati Vita vya Kagera ilipoanza na kupamba moto, Tanzania ilikuwa imeshapokea misaada na zana mbalimbali za kivita kutoka China.

Katika ukurasa wa 42 wa kitabu hicho, waandishi Dittmer na Maochun Yu wanaandika kuwa katika bara la Afrika, nchi ambayo Mao aliipa ‘kipaumbele cha juu’ ni Tanzania,na kuanzia mwaka 1964 Tanzania ilipewa msaada wa silaha mbalimbali vikiwamo vifaru, ndege vita na mfumo kamili wa usalama.

Kitabu cha China into Africa: Trade, Aid, and Influence kilichohaririwa na Robert I. Rotberg (chapa ya mwaka 2008) katika ukurasa wake wa 159 kinasema “...Zana za kivita kutoka China kwenda Afrika tangu 1966 hadi 1977 ilikuwa ni pamoja na boti za doria, vifaru na ndege za kivita aina ya MiG-17, MiG-19 na MiG-21 kwa ajili ya Tanzania.

Katika ukurasa wa 110 wa kitabu chake, Arms for Africa: Military Assistance and Foreign Policy in the Developing World, mwandishi Bruce Arlinghaus ameandika “China ilitoa (kwa Tanzania) asilimia 60 ya mahitaji yote ya kijeshi.

Pamoja na historia yote hiyo ya urafiki kati ya Tanzania na China tangu 1964 hadi 1978, Tanzania ilipoiendea kwa ajili ya msaada wa zana za kivita za kupambana na Idi Amin,Jamhuri ya Watu wa China iliiambia Tanzania kuwa haitajihusisha kwa namna yoyote na mgogoro kati ya Tanzania na Uganda.
Zaidi ya hilo,
China iliishauri Tanzania ikae mezani na Uganda kumaliza mgogoro huo.

Kilichofanywa na Serikali ya China ni kuwasilisha tu zana za vita zilizokuwa zimenunuliwa kabla vita haijazuka lakini hakuna silaha za ziada ambazo China ilitoa hata vipuri. Jeshi la Wananchi wa Tanzania likaanza kutegemea vipuri kama betri za vifaru kutokana na silaha walizoteka kwa majeshi ya Idi Amin.

Kwa upande wa Uganda, zana za kijeshi ambazo ilikuwa ikizipata kutoka Urusi hazikuendelea tena kutolewa.Kufikia katikati ya mwaka 1978 Serikali ya Idi Amin ilikuwa inazidi kutengwa.

“Kati ya 1975 na 1978 Uganda ilipata zana za kivita kutoka Urusi, Libya, Iraq, Uswisi na Libya,” kinasema kitabu cha Arms and Warfare: Escalation, De- escalation and Negotiation (chapa ya 1994) cha Michael Brzoska na Frederic Pearson.

Jumatatu ya Novemba 10, 1975 Idi Amin alitishia kuvunja uhusiano na Urusi ndani ya saa 48 ikiwa hangepata alichokitaka kutoka kwao. Alitishia pia kuwa angemfukuza nchini mwake balozi wa Urusi, Andrei Zakharov.

Aliilaumu Urusi kwa kuingilia mambo yake ya ndani. Pia aliilaumu kwa kumnyima vipuri kwa ajili ya ndege zake za kijeshi aina ya MiG-17 na MiG-21.
“Novemba 11, 1975 Idi Amin akatangaza kuwa Urusi imlete balozi wake mwingine ambaye ‘hana ubeberu’ kama aliyekuwapo,” kinaandika kitabu cha Who Influenced Whom: Lessons from the Cold War cha Dale Tatum.
Katika matangazo ya Redio Uganda, Idi Amin alisikika akifoka, “Mimi si kibaraka na sishurutishwi na yeyote.”

Mara baada ya hapo, kinaandika kitabu hicho, “Urusi waliamua kuvunja uhusiano na Uganda, lakini cha kushangaza Urusi iliurejesha uhusiano huo siku nne baadaye Novemba 15, 1978.”

Huu ni ule wakati ambao Idi Amin alikuwa mwenyekiti wa Nchi Huru za Afrika (OAU).
Uganda ilipovamiwa na makomandoo wa Israel katika kile killichoitwa ‘Operation Entebbe’ au kama ilivyojulikana kwa wengine, ‘Operation Thunderbolt’, Jumapili ya Julai 4, 1976 na ndege zake za kijeshi kuharibiwa vibaya, Urusi iliahidi kuimarisha kikosi cha anga cha Jeshi la Uganda na kuwapa ndege nyingine za kivita.

Kwa ahadi hiyo uhusiano kati ya Uganda na Urusi ukaanza kuimarika tena. Marubani wa ndege za jeshi za Uganda walipelekwa mafunzoni Urusi.

Itaendelea............

Copied from Matanga
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Yesu hapo ni lazima awe namba moja, kwa sababu yeye ni Mungu-mtu. Mungu-Mwanadamu.
 
Mkuu Kasomi heshima kwako.
Mungu ni mwema.

Uvumbuzi wote wa kisayansi kwetu Africa ni miujiza.

Aeroplanes, computers, simu za viganjani, internet painkillers, antibiotics, chanjo,n.k n.k.

Yote ni miujiza tu kwetu sawasawa na kufufua wafu au kuponya wagonjwa kwa neno.

Hivyo twaweza mpima Yesu kwenye mzani mmoja na hao Newton, Galileo, etc na kum declare kuwa amewazidi.

Alafu inasemekana ujio wa Yesu ndio ulileta mabadilko kwenye jamii ambayo yaliibua hivyo vipaji vya hao wanasayansi wakuu na hili laweza kuwa sehemu ya jibu la swali la mkuu Da’Vinci yaani Wagiriki walipoteza ubunifu na umaarufu kwa sababu waling’ang’ania upagani wao wakati wenzao wakibadilika na kwenda na Ukristo.
Amini mkuu,

Nimekuelewa vyema kabisa basi hata mimi nasema yesu ndio mkuu wa wote.
 
Opium poppy( Papaver somniferum) ndio raw material ya morphine.
Nimeongezea kidogo tu doctor.
Hivi hiyo uliyotaja ndio ile iliyokua inatumiwa kwenye Game of Thrones inaitwa Milk of poppy
 
Misri inapigiwa chapuo Sana kwenye huu hata kwenda nje swali alilouliza, wagiriki ndio wagunduzi wa mambo mengi ya sayansi mpaka siasa (democracy) ,
Tafiti zinaonyesha serikali (Government) iligunduliwa na wamisri, Je kati ya serikali na Siasa kipi kilianza?
hii ilitokana na utamaduni waliokuwa nao na dini kwani wagunduzi wengi kama sio wote walikuwa wanakaa maisha ya monastery au monks, industrial revolution nafikiri wao hawakujisumbua Sana na mabadiliko hayo ambayo yalianza kushape upya uchumi wa nchi zilizochangamkia hizo revolutions lakini bado wao wakaendelea kutumika kama wasomi wa Ku plan future ya nchi hizo, na hadi Sasa wanatumika
Umenifunza kitu kipya mkuu, Thanks. Ngoja nitafuatilia zaid
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.

Kwani Yesu ni binadamu jamani [emoji23][emoji23][emoji3][emoji16] mnatuvuruga si Mungu Huyu au
 
Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe.

kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hzamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watu wote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.
Vyema ukajibu swali kwa fact na mifano kuntu. Kusema tu alivunja rekodi bila kuainisha rekodi zenyewe huutendei haki uzi na muuliza swali kwa ujumla.
 
1.Alitembea Juu ya Maji.
2.Alimfufua Lazaro.
3.Alilisha watu elfu tano kwa Samaki wawili na Mikate Mitano na Mabaki ya samaki na mikate yakajaza vikapu 12.
4.Aliponya Vipofu,wakaona na Viziwi Wakasikia.
5.Aligeuza Maji kuwa Pombe kwenye harusi kule kana.
6.Alipokata roho pazia la hekalu lilipasuka na Wafu wakafufuka.
7.Mwenyewe alifufuka.

Sio isaack Newton tu bali hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuikaribia hiyo CV.
#6 [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Vyema ukajibu swali kwa fact na mifano kuntu. Kusema tu alivunja rekodi bila kuainisha rekodi zenyewe huutendei haki uzi na muuliza swali kwa ujumla.
Inategemea mwenzangu facts unazielewa vipi. Kwa uelewa wangu hayo niliyoongea ndio facts...
 
Wagiriki walivyokua bado hawajaungana kila Eneo linajitawala walitumia nguvu zaidi kujiimarisha maana wao hawakugopa kufa waliaamini wao ni viumbe special kutoka kwa baba yao wa uumbaji Zeus. Majina mengi ya kigiriki yanaishia na S hata majina ya watu wa mataifai mengine yanaishia S kwakua ni utamaduni uliotokana na wagiriki. Yesu pia jina lake laishia na S yaani Jesus sababu ni kwamba wagiriki wanaamini majina yanayoishia na S yanamaanisha ni mwanaume kutokana na Mungu wao wa kiume Zeus jina lake lainshia na S

Walivyoungana na kua kitu kimoja wakaanza kutumia akili na nguvu ili kujiimarisha zaido kwa kila nyanja wafalme waliwatumia watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri katika kutatua changamoto zinazowakabiri na waliwekea mazingira wezeshi hapa sasa ndio gunduzi zikaanza.
Mfano......

Kipindi fulani ugiriki ilikua ni sherehe ya mavuno hivyo wagiriki walikua wanamsherehekea Mungu wao wa mavuno kuwapatia mavuno mengi. Mfalme kama kiongozi mkuu alitakiwa awepo kwenye sherehe sasa mfalme akampatia dhahabu Muhunzi (Goldsmith) amtengenezee kofia ya kuvaa wakati wa sherehe (Crown), Muhunzi kuona dhahabu kashikwa na tamaa akachakachua dhahabu akaweka dhahabu nusu akaongezea na bronze (shaba) akampelekea mfalme kofia yake.... Mfalme akaangalia kofia akaona hapa kashapigwa cha juu ila hana uhakika.

Akaamua kumuita jamaa mmoja ambae kipindi hicho aliaminika ana akili sana aje amchunguzie kofia yake kama imetengenezwa kwa dhahabu tupu kweli au imechanganywa. Ila akamwambia asiiharibu wakati wa kuichunguza maana hana kofia nyingine...Jamaa huyo ni Archimedes

Archimedes akachukua kofia akaenda maabala kwakwe akachunguza wee akashindwa kupata majibu kichwa kikawaka moto hajui afanye nini.. akamuagiza mfanyakazi wake amuwekee mai ya kuoga bafuni kwenye Jacuzzi.
Akaenda bafuni akavua nguo akaingia kwenye Jacuzzi maji yakamwagika nje aivyoona hivo akatoka nje akikimbia uchi huku anapiga kelele hadi ikulu.

Alipomfikia mfalme akaanza kusema harakaharaa "When a body is totally or partially immersed in a fluid is subjected to an upwards force equal to the weight of the displaced fluid. "

Mfalme akamwambia unamaanisha nini wewe mbona sikuelewi [emoji23][emoji23]
Ndio mzee baba akaanza kumuelezea vizuri sasa... Akachukua vipimo vyake akapima uzito wa dhahabu na Shaba kisha akapima uzito wa Ile kofia ikaonekana muhunzi aliiba dhahabu. Na hapo ndio tukapata Law pedwa ya Archimedes principle na law of floatation inayohusu Density. Kupitia law hizo tumepata Meli mbalimbali..

Sio hivyo tu Archimedes alisaidia san kwenye vita..alikua anatengeneza vifaa vya kivita au anatumia vioo kuunguza meli za maadui wanakuja kuvamia nchi yake.

Sisi huku kama una ujuzi wa kutengeneza Gobole au siraha unanyanganywa na unakomeshwa kabisa uwe mfano wengine wasirudie upuuzi kama huo
Kuna jamaa niliwahi waona kwenye TV walikamtwa wametengeneza gobole,

Mwengine alitengeneza gari akapigwa stop.

Mwengine kipindi cha uchaguzi ule 2015 alitengeza chopper nae akazinguliwa.

Africa ukiwa na talent unazinguliwa badala ya kiwachukua wale kuwapiga msasa

Models zao zingechukuliwa na kwenda fanyia testing.maabara leo TZ tungekuwa na kiwanda cha silaha kikubwa tungeuza africa nzima na tungekuwa brand riffle zetu

Tungekuwa tuna assemble choppa zetu za jeshi na polisi

Tungekuwa tuna gari zetu safi kabisa hatuna haja kuagiza mitumba inayochafua hewa na kutidhia uhai wa viumbe hai .

Africa TUMEROGWA
 
Kuna jamaa niliwahi waona kwenye TV walikamtwa wametengeneza gobole,

Mwengine alitengeneza gari akapigwa stop.

Mwengine kipindi cha uchaguzi ule 2015 alitengeza chopper nae akazinguliwa.

Africa ukiwa na talent unazinguliwa badala ya kiwachukua wale kuwapiga msasa

Models zao zingechukuliwa na kwenda fanyia testing.maabara leo TZ tungekuwa na kiwanda cha silaha kikubwa tungeuza africa nzima na tungekuwa brand riffle zetu

Tungekuwa tuna assemble choppa zetu za jeshi na polisi

Tungekuwa tuna gari zetu safi kabisa hatuna haja kuagiza mitumba inayochafua hewa na kutidhia uhai wa viumbe hai .

Africa TUMEROGWA
Watawala ndio tatizo
 
Kwanza kabisa sijawataja Waashuru kweye uzi huu nimewataja waajemi tu (Persian yaani iran)
Ahusuhero ni majina ya viongozi wa persian kwa mujibu wa tafsiri mbalimbali kama ilivyokua kwa wamisri Pharaoh na warumi Caesar.


Ahsante kwa kwa mchango ..

Kabisa nakubali. Na alexandar anabaki kua bora kwakua alipewa madini yote na Aristotle.. hapa ndio tutaona elimu na Utawala zinavyosaidia. Alexander aliweza kwa kutumia tactics na Falsafa alizofundishwa na Aristotle.

Unaona hata Marcus aurelius aliweza kuongoza vyema kwakua alichagua Zeno of citium kua mentor wake katika falsafa. Nami nimemchagua Aurelius kuwa mentor wangu wa maisha🙏

Alexander ilikuja kuanguka mikononi mwa Cleopatra ikapelekea kuharibiwa kwa Maktaba ya kwqnza duniani ikiyokua ina urithi wa maarifa mengi ya watu wa misri enzi za utawala wa warumi

Watu wa zamani kweli umri hakujalisha katika kutenda mambo makubwa eg, Yesu, nyerere nk. Dogo angeishi japo miaka 50 Sijui ingekuaje

Kwel kila zama na kitabu chake.. Sikutegemea Rumi na Ugiriki zitakuja kuanguka. Naona na Great Britain nayo ilishasagika japo inajitutumua bado..Ngoja tuone kama USA nae atakuja kuanguka kama wengine au nivipi..


Finally a worth opponent, our battle will be legendary 😆
Wakati mataifa mengine ya ulaya yanajijenga kiuchumi,kisiasa,wagiriki walijisahau walikua busy na kusoma&kuandika history ya dunia,kuja kustuka wamechelewa...
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Umemuweka Yesu kwenye kundi la binadamu alafu umemuweka nafas ya tatu
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
mkuu natafuta ule uzi wako unaelezea king leonidas na watu wake mia tatu
 
Back
Top Bottom