Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Yaani sawa sawa uulize kua kabla ya kugundulika gravity jiwe lilikua likilishwa juu halirudi chini????
Naam Sasa tupo sambamba...! Kwamba Meli/mitumbwi zilishagunduliwa sema kwa sheria ya " kichaa" Archimedes maboresho ya urahisi katika ufanisi wa Meli yalianzia kwa Kasi..!
 
Eti kawawa
' Development in third world countries, "Kawawa funika kikombe", must be set in such a way that it is understood by citizens in those respective countries.' Alisema Mwalimu alipoona kikombe hakifunikwi huku Wazungu wakiendelea kuminina chai wakati muhusika ameisha tosheka.
====
Kweli Kuna haja ya kufuatilia hili tujue huu usumbufu aliuanzisha nani na kw manufaa yapi!
 
Hivi stori za kawawa nani alizitunga na kwasababu gani?? Eti kawawa alilala chini alishwindwa kujua kitanda kipo ukutani inabidi ubonyeze batan ili kichomoke. Ila nyerere alijua. 😂
Walikua wanatuchukuliaje lakini??

Eureka Eureka.....
Vijiwe vya kahawa havikosi wazee wa fiksi 😂
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.

1. Imhotep
2. Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Huyo namba tatu alikuwa na akili gani zaidi ya kufata mwongozo wa kitabu?
 
Hivi unajua sehemu kama Egypt, Mesopotamia, Crete, Syria, Anatolia, Iran, and the Indus Valley walipata civilization kabla hata ya wagiriki.

Pia wachina waligundua mengi na kusafiri hata kabla ya wengi ambao ndio wamekuwa accredited na ugunduzi huo.

Kwa ufupi ni utamaduni, kukiwa na utamaduni wa kuhoji na watu kupenda kujifunza basi jamii itagundua vitu na kuendelea (Binadamu wanazaliwa wakiwa a Blank Slate) Tabula Rasa ila jamii inayowazunguka ndio inawajengea wawe watu wa aina gani.

Iran ilikuwa imepiga hatua sana, lakini kuingia mambo ya imani all was destroyed in few years. Wachina walikuwa wamesafiri duniani kote tangia zamani ila Mfalme wao kupiga marufuku culture za nje ikawapunguzia kasi.

Kwahio na sisi hizi indoctrination kwamba kila kitu tumepewa au kila kitu kina sababu, hakuna kuhoji wala kutafuta ukweli usishangae miaka milioni moja ijayo tukawa bado tunapiga ramli na kudhani ni Jirani yetu katuloga, au tukiugua ni Mungu amependa.
Egypt walikuwa wanakaa watu gani, black au waliopo sasa
 
Wagiriki walivyokua bado hawajaungana kila Eneo linajitawala walitumia nguvu zaidi kujiimarisha maana wao hawakugopa kufa waliaamini wao ni viumbe special kutoka kwa baba yao wa uumbaji Zeus. Majina mengi ya kigiriki yanaishia na S hata majina ya watu wa mataifai mengine yanaishia S kwakua ni utamaduni uliotokana na wagiriki. Yesu pia jina lake laishia na S yaani Jesus sababu ni kwamba wagiriki wanaamini majina yanayoishia na S yanamaanisha ni mwanaume kutokana na Mungu wao wa kiume Zeus jina lake lainshia na S

Walivyoungana na kua kitu kimoja wakaanza kutumia akili na nguvu ili kujiimarisha zaido kwa kila nyanja wafalme waliwatumia watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri katika kutatua changamoto zinazowakabiri na waliwekea mazingira wezeshi hapa sasa ndio gunduzi zikaanza.
Mfano......

Kipindi fulani ugiriki ilikua ni sherehe ya mavuno hivyo wagiriki walikua wanamsherehekea Mungu wao wa mavuno kuwapatia mavuno mengi. Mfalme kama kiongozi mkuu alitakiwa awepo kwenye sherehe sasa mfalme akampatia dhahabu Muhunzi (Goldsmith) amtengenezee kofia ya kuvaa wakati wa sherehe (Crown), Muhunzi kuona dhahabu kashikwa na tamaa akachakachua dhahabu akaweka dhahabu nusu akaongezea na bronze (shaba) akampelekea mfalme kofia yake.... Mfalme akaangalia kofia akaona hapa kashapigwa cha juu ila hana uhakika.

Akaamua kumuita jamaa mmoja ambae kipindi hicho aliaminika ana akili sana aje amchunguzie kofia yake kama imetengenezwa kwa dhahabu tupu kweli au imechanganywa. Ila akamwambia asiiharibu wakati wa kuichunguza maana hana kofia nyingine...Jamaa huyo ni Archimedes

Archimedes akachukua kofia akaenda maabala kwakwe akachunguza wee akashindwa kupata majibu kichwa kikawaka moto hajui afanye nini.. akamuagiza mfanyakazi wake amuwekee mai ya kuoga bafuni kwenye Jacuzzi.
Akaenda bafuni akavua nguo akaingia kwenye Jacuzzi maji yakamwagika nje aivyoona hivo akatoka nje akikimbia uchi huku anapiga kelele hadi ikulu.

Alipomfikia mfalme akaanza kusema harakaharaa "When a body is totally or partially immersed in a fluid is subjected to an upwards force equal to the weight of the displaced fluid. "

Mfalme akamwambia unamaanisha nini wewe mbona sikuelewi [emoji23][emoji23]
Ndio mzee baba akaanza kumuelezea vizuri sasa... Akachukua vipimo vyake akapima uzito wa dhahabu na Shaba kisha akapima uzito wa Ile kofia ikaonekana muhunzi aliiba dhahabu. Na hapo ndio tukapata Law pedwa ya Archimedes principle na law of floatation inayohusu Density. Kupitia law hizo tumepata Meli mbalimbali..

Sio hivyo tu Archimedes alisaidia san kwenye vita..alikua anatengeneza vifaa vya kivita au anatumia vioo kuunguza meli za maadui wanakuja kuvamia nchi yake.

Sisi huku kama una ujuzi wa kutengeneza Gobole au siraha unanyanganywa na unakomeshwa kabisa uwe mfano wengine wasirudie upuuzi kama huo
Alijuaje akipima dhahabu kiasi gani ndo utakua sawa na uzito wa dhahabu ya kofia.
 
Ile movie ya 300 na ile ya "Rise of an empire" kumbe ni history za kweli? Ngoja nizicheki Tena.
By the way nitafika Athens siku moja
 
Back
Top Bottom