DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
WAKATI zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa wagombea wa katika uchaguzi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (SRT), likifungwa rasmi Julai 18 saa 10:00 jioni, jumla ya wagombea 20 wamejitosa kuwania nafasi mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Julai 21, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi SRT, Leonard Thadeo, alisema rasmi zoezi la uchukuaji na urejeshaji lilifunguliwa rasmi Juni 16 na kuhitimishwa rasmi Julai 18 kama ambavyo Katiba ya shirikisho inavyoelekeza.
Thadeo, alisema baada ya hapo leo Julai 21 wameanza kuzichakata fomu hizo, kabla ya Julai 25 kuweka had had any majina ya watakaoitwa kwenye usaili utakaofanyika Agosti 1.
"Tumeona leo tuwataarifu wadau kinachoendelea maana kumekuwa na maswali mbalimbali, tangazo la nafas i za kugombea uongozi wa Shirikisho la Riadha lilitolewa Juni 16, ikiwa si chini ya mwezi mmoja kama ambavyo katiba inaelekeza na Julai 18 ilikuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha...
"Hivyo leo tumeanza zoezi la kuzichakata ambapo jumla ya wagombea 20 wamejitokeza kwenye nafasi mbalimbali," alisema Thadeo na kuongeza zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu lilikuwa la wazi na wagombea walikuwa na fursa ya kuzipata fomu kwa ya e mail, sanduku la posta, kwa njia ya mitandao au kufika ofisini mwenyewe.
Mwenyekiti huyo, aliwataja waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais kuwa ni Angelus Likwembe, Juma Ikangaa, Rogath Stephen, William Kallaghe, Nsolo Mlozina Silas Isangi.
Nafasi ya Makamu wa Rais wagombea ni wawili ambao ni Baraka Sulus na Jackson Ndaweka huku
nafasi ya Mwakilishi wa Wanawake ni Noela Mafuru na Lwiza John.
Wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Christina Paga, Sylivia Rushokana, Shenya Imori, Alfredo Shahanga, Tullo Chambo, Michael Washa, Ibrahim Adam, Andrew Rhobi, Tabu Mwandu na Joshua Kayombo.
Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania, unatarajiwa kufanyika Agosti 16 jijini Mwanza.