Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
- Thread starter
- #21
Kalonzo Musyoka atarudi tu kubembeleza ugali Azimio. Ni kivuruge yule. 2013 Raila alimwambia waungane dhidi ya Uhuru akagoma akifikiri Uhuru atampa mfupa (maana pensheni ya U-VP wakati wa PNU) haimtoshi kuendesha chama WIPER na OKA. Raila akamwambia kwani mshahara wa U-VP ulikuwa unapokea shs ngapi? Akataja, Raila akasema anampa taslimu kwa mkupuo mmoja wa miaka mitano ili aje Rainbow, akachukuwa mkwanja na kutokomea, sasa hii ya juzi ya kujiondoa Azimio ni mara ya pili anamsaliti Raila.Naona unaifuatilia siasa za Kenya kwa ukaribu sana.
Ukoo wa Odinga ni Wajamaa wanaoamini kwenye utajiri. Ukoo huu una utajiri mkubwa Kenya (waligoma kuwekeza nje ya nchi). Raila hatafuti urais kuganga njaa bali kuipa Kenya maendeleo ili waishi kwenye nchi nzuri kwa maisha yao yote na vizazi vyao. Babake alikuwa tajiri wa pili Kenya baada ya uhuru akaja kupitwa na Kenneth Matiba aliyekuwa na majority shares kwenye Kenya Breweries.
Kiwanda cha kusindika gesi Kenya ni cha ukoo wa Odinga tena alikizindua Mwl Nyerere wakati uhusiano wa ukoo wa Odinga na Moi ulipozorota. Kaka mkubwa wa Raila Dr. Oburu Oginga alikuwa Jasusi ktk KGB kwa miaka mingi kabla ya kudai kurudi kwao Kenya kwa sababu ni ukoo ambao una uzalendo mkali kwa nchi yao.
Utajiri wa akina Raila ni wa ukoo/urithi siyo wa ufisadi.