Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima kwenu wanajamvi,
Leo nimeona ni vyema na haki tukawajadili wagombea nafasi ya Rais wa JMT kutokea chama cha CDM.
Nadhani nianze na Mheshimiwa Lissu si kwa bahati mbaya la hasha, nimeanza na Lissu kwasababu ni mgombea pekee mwenye mvuto kwa wananchi lakini pia ni mgombea mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kueleweka kwa wananchi.
Namebahatika kusoma maandiko mbalimbali ya Mhe Lissu tangu akiwa mwanasheria aliyejikita zaidi katika masuala ya mazingira hasa migodi ya dhahabu maeneo ya Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Mwanza na Mara) Mhe Lissu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujenga na kupangilia hoja zake, anaeleweka kwa urahisi kwakuwa kila wakati jambo analolisimamia anakuwa analifahamu ndani nje. Ni aina ya watu ambao hawapendi kubahatisha jambo.
Mhe Lissu si mtu wa kukurupuka hata alipochaguliwa katika nafasi ya ubunge. Bunge letu hasa mawazi na Mwanasheria Mkuu wa Serekali walikumbana na hoja nzito zilizosheheni utafiti wa kutosha. Kwa hakika Bunge la JMT lilikosa mtu mahiri sana na pengo lake mpaka leo sijaona Mbunge angalau mmoja ambaye labda alifikia 50% ya kiwango cha Mh. Lissu. Hii aibu kubwa sana hasa kwa waheshimiwa wabunge waliomaliza muda wao.
Kuna kipindi wananchi walipenda kusikiliza michango ya wabunge mbalimbali kwakuwa waliamini walikuwa wakiwasemea na kuwawakilisha vyema.Michango ya mwisho ya bunge letu la bajeti ilikosa watu aina ya Mh Lissu badala yake tulijikuta tukiambulia michango ya ajabu kutoka kwa wabunge kama Mh Lugola, Mh Msukuma, Mh Lusinde, Mh Silinde, Mh Lijualika na nk ambao badala ya kujadili bajeti ya wananchi walizama zaidi katika kumshambulia KUB Mh Mbowe. Bahati mbaya zaidi hata Mh Job Ndugai naye alijiingiza katika mambo yanayofanana na hayo.
Mh Lissu anatosha kugombea uRais kwa tiketi ya CHADEMA ingawa kushinda ni vigumu sana lakini anaweza kusababisha kupatikana wabunge wengi wa Upinzani.Mh Lissu atahitaji msaada mkubwa sana kutoka chama chake ambacho uchaguzi uliopita kilifanya makosa makubwa ya kuwakaribisha wagombea walioshindwa kupata nafasi za uongozi ndani ya CCM. Kosa la kumkaribisha Mh Lowassa na kumwacha Mh Balozi Dr Slaa kuliondoa identity ya chama kupinga ufisadi. Ajenda hii ilitekwa na Mh Dr Magufuli ingawa utekelezaji umegubikwa na shaka shaka kubwa.
Ningekuwa na mamlaka ndani ya CHADEMA Mh Lissu angepitishwa mapema asubuhi bila kupoteza muda.Nafikiri ni muda muafaka haswa ndani ya CHADEMA kuacha kupoteza muda Mh Lissu anauzika kirahis zaidi ukilinganisha na wagombea wengine hasa katika majira haya yanayo hitaji mtu wa kushindana na Mh Magufuli ambaye katika kipindi cha miaka mitano amehakikisha upinzani haupati nafasi ya kusikika huku yeye binafsi akitumia vyombo vya habari sana.