Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mgombea Uenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, amekuwa wa kwanza kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa juu wa chama hicho.
Lissu amewasili katika viwanja vya ukumbi huo saa 10:15 asubuhi, akiwa ndani ya gari jeusi Land Cruiser lenye namba za usajili T216 DHH.
Soma: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
Baada ya kufika, alipokelewa kwa shangwe na wafuasi wake waliokuwa wameshika mabango huku wakiimba, "Lissu! Lissu!"
Wafuasi hao pia wamesukuma gari lake hadi eneo la maegesho kabla ya mgombea huyo kuingia ukumbini.
Mgombea uenyekiti CHADEMA ngazi ya taifa Odero Charles Odero akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani city sehemu ambayo ndipo utqkapofanyika uchaguzi huo siku ya leo tarehe 21January 2024.
Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Chadema, Ezekia Wenje akiingia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi leo Januari 21, 2025.