ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Mgombea Urais wa CHADEMA mwaka huu amekuwa akipinga jitihada za serikali kusambaza umeme, maji vijijini na mijini, kuboresha huduma za afya, elimu na ofisi za umma, kuimarisha miundombinu na huduma za usafiri wa majini, anga na nchi kavu.
Kutokana na kauli za mgombea huyo wa Urais, wagombea wa Ubunge wa CHADEMA wamekosa ahadi za kuwapa wapiga kura. Yale yote yanayopingwa na mgombea wa chama chao, ndio kero za wapiga kura wa Ubunge na Udiwani.
Kila wanapopita wanajikuta wanalazimika kuahidi kuboresha huduma za afya, lakini kwa vile chama chao kinapinga, wananchi wanashindwa kuwaelewa. Wakijaribu kuahidi kuboresha elimu wanajikuta katika hali hiyohiyo ya kukosa hoja mbadala.
Kwa hali iliyopo huku mitaani, wabunge wengi wa CHADEMA watashindwa kurudi bungeni. Vilevile, chadema itashindwa kupata wabunge kwenye majimbo mengine yasiyokuwa na wabunge wa CHADEMA.
Imeshakuwa bayana kuwa kitendo cha mgombea Urais wa Chadema kuacha kunadi ilani ya chama chake na kujiamulia kupinga maendeleo kitakigharimu chama hicho.