Uchaguzi 2020 Wagombea wa Ubunge wa NCCR na ACT-Wazalendo wajiunga CCM

Uchaguzi 2020 Wagombea wa Ubunge wa NCCR na ACT-Wazalendo wajiunga CCM

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wagombea wawili wa Ubunge katika Jimbo la Serengeti mkoani Mara wameacha kuendelea na kinyang’anyiro cha kupambania kupata ubunge wa Jimbo hilo na kuhamia CCM.

Mmoja wa wagombea hao ni Daniel Daudi ambaye alikuwa anagombea kupitia, NCCR-Mageuzi na Amosi Roswe aliyekuwa anagombea kwa tiketi ya ACT-Wazalendo.

Jimbo la Serengeti lilikuwa chini ya Marwa Ryoba ambaye alihamia CCM kutokea CHADEMA. Aidha kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu CCM imemsimamisha Jeresabi Mkimi.

ACT-NCCR.jpg
 
Haya si ni matakataka! Wamepima upepo wakaona watapata kura 2 kila mmoja! heri kujitoa kapata hizo hela kidogo walizowapa!
 
Waache waende watakako, nayo ni demokrasia.
 
Mgombea wa CHADEMA katika jimbo hilo anaitwa nani?

Mkuu Analogia Malenga naomba unijibu maana wewehuwahutupi ushirikiano hapa jukwaani hasa hasa member wa upinzani.
 
Mbona kama nasikia mzee baba alijichanganya huko akamuombea kura wa chadema
 
Ok shukrani mkuu, vipi anaundugu na na marehemu Mtahaba?
Hapana. Hawana uhusiano wowote, ni majina tu. Huyu mdada kwao ni eneo linaloitwa Ngoreme wilaya ya Serengeti. Mtahaba ni Mhaya wa Kagera.
 
Daniel Daud huyo ni msaka tonge hana lolote awali alikuwa CUF amehamia NCCR Mageuzi then CCM baada ya kuona hawezi toboa kwa chadema mbuzi wa mayai tu huyo hapa Serengeti ccm hamtoboi saizi chadema imesimama tulieni tuwaoneshe hao hawana uwezo hata kidogo hata wakihamia ccm wamefata maslahi yao tuulize watoto wa town wenye mji wetu tunajua mbunge wetu na diwani ni nani
 
Muulizeni mkurugenzi yule mama na chandi walivotaka kudhurumu haki ya chadema 2015 kilicho wakuta
 
Daniel daud huyo ni msaka tonge hana lolote awali alikua cuf amehamia Nccr then ccm baada ya kuona hawezi toboa kwa chadema mbuzi wa mayai tu huyo hapa Serengeti ccm hamtoboi saizi chadema imesimama tulieni tuwaoneshe hao hawana uwezo hata kidogo hata wakihamia ccm wamefata maslahi yao tuulize watoto wa town wenye mji wetu tunajua mbunge wetu na diwani ni nani
Na tume inajua nani
 
Na tume inajua nani
Serengeti hatupangiwagi tuna amuaga sisi sisi haki ikidhurumiwa kwanza tuna zingira halimashauli nzima tuna wahi kwa mkurugenzi tuna zingira kwa lolote tunafanya hatudhurumiwagi haki Serengeti tukiamua tunaemtaka ndie atuongoze no story maamuzi yapo kwa wana Serengeti na sio maagizo kutoka juu
 
Back
Top Bottom