beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Umoja wa Wapigakura Tanzania (UWAKUTA), umewatahadharisha wagombea wa urais, ubunge na udiwani kutoka vyama vyote vya siasa kuwa ni lazima watii na kuheshimu uamuzi wa wapigakura katika matokeo ya uchaguzi.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mratibu wa UWAKUTA, Peter Mpeleka, alisema jana kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya wagombea wa udiwani, ubunge na urais kuingilia uamuzi wa wapigakura kwa kubeza matokeo.
Mpaka sasa, alisema umoja huo umeshatembelea maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wapigakura kuhusu umuhimu wa kushiriki kwa wingi, kuwachagua wagombea wa nafasi mbalimbali wanaowataka kwa ajili ya maendeleo yao.
Mpeleka alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kulalamikia matokeo bila sababu za msingi, hivyo kusababisha taharuki kwa wapigakura na wananchi kwa ajili ya mstakabali wa amani ya nchi yao.
Alisema umoja huo unashirikiana na vyombo vya dola, kuhakikisha wanawatia nguvuni baadhi ya watu, ambao wamekuwa na tabia ya kuwahadaa wapigakura kwa kununua shahada zao za kupigia kura katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa nchi.
Mpekeka pia, alivitaka vyombo vya dola kulinda usalama wa wapigakura kwa lengo la kuhakikisha wanakwenda katika vituo vya kupigia kura na kutimiza wajibu wao wa kuwachagua viongozi wanaowataka, bila ya bugudha yoyote.
Alisema, vyombo vya dola visije vikajiingiza katika kuwanyanyasa wapigakura kwa namna yoyote ile na kuwa jukumu lao ni kuhakikisha wanalinda usalama wa wapiga kura katika maeneo ya vituo vya kupigia kura.