Uchaguzi 2020 Wagombea waonywa kutoheshimu matokeo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Umoja wa Wapigakura Tanzania (UWAKUTA), umewatahadharisha wagombea wa urais, ubunge na udiwani kutoka vyama vyote vya siasa kuwa ni lazima watii na kuheshimu uamuzi wa wapigakura katika matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mratibu wa UWAKUTA, Peter Mpeleka, alisema jana kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya wagombea wa udiwani, ubunge na urais kuingilia uamuzi wa wapigakura kwa kubeza matokeo.

Mpaka sasa, alisema umoja huo umeshatembelea maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wapigakura kuhusu umuhimu wa kushiriki kwa wingi, kuwachagua wagombea wa nafasi mbalimbali wanaowataka kwa ajili ya maendeleo yao.

Mpeleka alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kulalamikia matokeo bila sababu za msingi, hivyo kusababisha taharuki kwa wapigakura na wananchi kwa ajili ya mstakabali wa amani ya nchi yao.

Alisema umoja huo unashirikiana na vyombo vya dola, kuhakikisha wanawatia nguvuni baadhi ya watu, ambao wamekuwa na tabia ya kuwahadaa wapigakura kwa kununua shahada zao za kupigia kura katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa nchi.

Mpekeka pia, alivitaka vyombo vya dola kulinda usalama wa wapigakura kwa lengo la kuhakikisha wanakwenda katika vituo vya kupigia kura na kutimiza wajibu wao wa kuwachagua viongozi wanaowataka, bila ya bugudha yoyote.

Alisema, vyombo vya dola visije vikajiingiza katika kuwanyanyasa wapigakura kwa namna yoyote ile na kuwa jukumu lao ni kuhakikisha wanalinda usalama wa wapiga kura katika maeneo ya vituo vya kupigia kura.
 
Hawana la maana.
 
Kwa iyo kama tume sio huru na ina uwezo wa kutangaza yeyote imtakayo kwa masrahi yao kwa iyo alieibiwa kura akae kimya na alizike?? Kwa dhuruma aliyofanyiwa sio nyie acheni kuiogopa serkal cha msingi na cha secondary tunataka Katiba mpya ili mfumo wa kufanya au kuendesha mambo ubadikike na uwe wazi kisheria ili ikitokea kiongoz au mtu amekosea awajibishwe kwa mjibu wa sheria tulizoweka sio mambo ya nchi yenye watu million karibu 60 yaamuliwe na mtu mmoja yy ni nani??!!!

Tunataka tume iwe huru na sio mambo za kuteuana ili ubebwe na uliowateua ndio maana hawataki Katiba mpya maana hii ya sasa inawabeba watawala na sio sisi wanyenchi wa kawaida. Embu angalia wakuu na wasimamizi wengi wa taasisi na mamlaka mbali mbali niwa kuteuliwa na sio wa kuchagiliwa na wanyenchi, wakuu wa walaya, wa mikoa, wawaziri, makatibu, wakurugenzi wa halimashaur, majaji, takukuru, mpka tume ya uchaguzi nao wanateuliw na rais haya niambie sasa hapo haki wa kutangaza mpinzani akishinda unapata wapi!!??
 
Back
Top Bottom