Wagombea wengi wazuri wanakwamishwa na gharama za Uchaguzi

Wagombea wengi wazuri wanakwamishwa na gharama za Uchaguzi

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,973
Reaction score
6,750
Ndugu wajumbe,

Leo napendekeza tujadili hili suala gharama za Uchaguzi jinsi linavyosababisha viongozi wazuri na wenye maono makubwa kukosa nafasi za uongozi hata wa kata.

Hili ni jambo ambalo linaleta ubaguzi,na wakati mwingine linasababisha rushwa wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Ukitazama katika kura za maoni za CCM utaona namna ambavyo watu walitumia gharama kubwa kununua kura.

Swali langu ni Je, katika Uchaguzi Mkuu ujao watanzania watapata viongozi bora hasa kwa sababu ya umaskini unaosababisha wengi wa viongozi wazuri kushindwa kumudu kampeni? Je, wagombea wafanyeje ili kupata Fedha kwa ajili ya kampeni ambazo hazitakuwa na masharti wala hazitwafanya wawe na madeni makubwa?

Je, wananchi wana mtazamo gani kwa wagombea wasiokuwa na Pesa za kufanya kampeni za kisasa?Watawaunga mikono kama wa na sera nzuri?

Tujadili hapa katika lengo la kujenga bila kujali tofauti zetu za kiitikadi
 
Back
Top Bottom