Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Habarini wadau.
Kuna maambukizi ya ule ugonjwa wa macho mekundu almaarufu kama red eyes, ambao husababisha macho kuwasha, kuuma, kuwa mekundu sana, kuvimba na kutoa uchafu mwingi sana wa tongo tongo.
Ni ugonjwa unaosambaa kwa kasi sana endapo tahadhari hazitachukuliwa mapema kutoka kwa walio ambukizwa kuwaelekea ambao hawajaambukizwa.
Ugonjwa huu unasambaswa sana kwa njia ya vimelea au Virusi kutoka kwa mgonjwa anaposhika macho yake na kuwapakaza wengine kwa njia ya kuwagusa aidha machoni direct (hii ni kwa watoto sana sana maeneo yao ya michezo), au mgonjwa kujigusa machoni wakati akijifikicha na kushika sehemu mbali mbali kama vitasa vya milango, siti za daladala na mabomba ya abiria waliosimama na kujishikiza, vijiko, sahani, vikombe au glass, remote , na hata arm rest za viti wanaposhika na kupakaza wale Viruses, kushikana mikono wakati wa salam na kadhalika.
Kitu kinacho nikwaza katika kipindi hiki cha maambukizi ni changamoto ya watu ambao tayari wameambukizwa inakuta wanajichanganya maeneo ya mkusanyiko na miwani yao myeusi kama paka wa kichawi wakishika vitu, pesa, na mazingira kwa ujumla jambo linalopelekea kusambaa kwa Virusi hawa wabaya kwa kasi kubwa.
Imagine pesa inashikwa na mikono michafu mingapi ya watu wenye red eyes wasio na ustaarabu wa kunawa mikono yao na sabuni ili kupunguza maambukizi.
Unakuta jitu linafikicha macho halafu linashika vyombo, milango, pesa, na kusababisha Virusi kusambaa kwa kasi.
Kwann usitulie nyumbani japo hata siku mbili au tatu ujiuguze upone ndipo kujichanganya na watu, au kama ni lazima sana kutoka why usichukue tahadhari ya kubeba sanitizer mfukoni au kwenye pochi, na kusanitize mikono yako kila baada ya masaa kadhaa ili kupunguzo carriage load ya Virusi kwenye viganja na vidole vyako before haujasambazia wengine popote walipo?
Kwann usiwe na subira na afya yako at least upone kwanza kabla haujawasambazia wengine?
Tahadhari ni muhimu ili kuwalinda wengine, mtu una mgahawa unaruhusu vipi muhudumu au mpishi aje kazini na anaumwa red eyes kwann usimpe 'paid leave' hadi apone ndipo aje kazini?
Mtu anahudumia watu huku kavaa miwani myeusi, macho yamevimba na machafu yanatia kinyaa hata kutazama. Why unaendelea kukaa eneo la kazi badala ya kujiuguza at least upate nafuu.
Aisee nimechefukwa sana leo. Nimekuna na watu wenye red eyes sehemu 4 tofauti na pote huko wanashika shika vitu na pesa. Nimechefukwa sana aisee.