Wagundua sumu ya kuua VVU mwilini

Wagundua sumu ya kuua VVU mwilini

Mleta uzi kama siyo Muathirika basi atakuwa ni Mzinzi aliyekubuhu..jinsi alivyoiandika Title daah kafurahi kweli.

Kwa hiyo mtu akileta habari za Jangili kuua Tembo naye atakuwa ni Jangili? Acha kunyanyapaa watu, kesho yako hauijui waweza kumbwa na gonjwa baya kuliko ukimwi.
 
Dr.Isokopyomopoko wa JF kasema dawa yeye anayo kama unataka tiba we m-PM.
 
Utaisha, si leo wala kesho lakini UTAISHA! Kuna magonjwa yalitisha kuliko UKIMWI lakini wataalam waliyapatia dawa.

Ila utakuwa umeshatamba vyakutosha kuliko ugonjwa mwingine wowote kwakukaa muda mrefu kabla dawa haijagundulika. Ukimwi noma jamani, endeleeni kutumia every measure ya uupekuka ohoo.
 
Ila utakuwa umeshatamba vyakutosha kuliko ugonjwa mwingine wowote kwakukaa muda mrefu kabla dawa haijagundulika. Ukimwi noma jamani, endeleeni kutumia every measure ya uupekuka ohoo.

Kuna magonjwa yalitisha ndugu yangu, Malaria bado inashika namba moja, Smallpox iliuwa watu zaidi ya 500M ndani ya karne ya ishirini pekee! Kuna BP, kuna Ukoma, magonjwa yapo mengi mno, Ukimwi mbona mtoto mdogo, sema kwa vile umewagusa wazinzi starehe ya wengi ndiyo maana unaonekana kama unatisha, lakini Ugonjwa kama Malari Unatisha kuliko Ukimwi!
 
Mleta uzi kama siyo Muathirika basi atakuwa ni Mzinzi aliyekubuhu..jinsi alivyoiandika Title daah kafurahi kweli.
Acha unyanyapaa wewe, JF ipo kwa lengo lá kuhabarishana na kuelimishina, mleta mada amepost hiyo kitu ili watu wahabirishwe,iweje wewe ufanye kazi ya kubashiri kama marehemu Sheikh Yahya?!
 
Acheni kebehi,kila hatua ni ya kupongezwa maana miaka mingi wataalamu walikuwa hawajapata hata pa kuanzia.Dalili nzuri ni kwamba hata kama si sisi lakini pengine watoto wetu watakuwa free na hili gonjwa.
 
Mleta uzi kama siyo Muathirika basi atakuwa ni Mzinzi aliyekubuhu..jinsi alivyoiandika Title daah kafurahi kweli.


mleta mada alimaliza.siredi yake kwa kusema "SUMU HIYO ITAANGAMIZA VAR MOJA YA VVU-nadhani kwa sasa kuna VAR zaidi ya nne, so.safari bado ni ndefu.....
 
:whoo::whoo:
Dar es Salaam.Timu ya Watafiti katika Chuo Kikuu cha North Carolina nchini Marekani, wamegundua aina ya sumu ambayo ina uwezo wa kuua seli ambazo zimekwishaathiriwa na Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Sumu hiyo iliyopewa jina, 3B3-PE38, inaweza kutumika kutengeneza dawa ambayo ikitumiwa na mtu aliyeathirika kwa VVU, itasaidia kuua virusi.

Watafiti wamebaini pia kuwa dawa hiyo itaweza kusaidia waathirika kutolazimika kutumia dawa za Kupunguza Makali ya Ukimwi (ARVs) maisha yao yote.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kuweza kugundua sumu maalumu ya kuua VVU. Tafiti nyingi zinazoendelea sehemu nyingi duniani ni za kupata chanjo.

Kwa kawaida dawa ni sumu inayoua au kuathiri kiumbe kilichokusudiwa wakati chanjo ni njia ya kuufanya mwili kutengeneza wenyewe kinga dhidi ya vimelea, kulingana na aina ya ugonjwa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa wiki hii na Taasisi ya Tafiti za Kukabili Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID) ya Marekani, inasema ni ugunduzi wa kipekee.

Upekee huo unaoelezwa unatokana na ukweli kuwa kwa sasa dawa zilizopo za ARV zina uwezo wa kuzuia seli nyeupe iliyoshambuliwa isimamishe mvumo wa kuzalisha virusi.

Walivyoendesha utafiti

Utafiti huo uliofadhiliwa na Taasisi ya Afya ya Taifa (NIH) ya Marekani, unaelezwa kuwa panya 40 walitumika katika kutafiti 3B3-PE38.

Walichofanya watafiti hao ni kuwagawa panya kwenye makundi kadhaa na kupewa dozi ya sumu ya 3B3-PE38 kwa viwango na muda tofauti kuanzia wiki mbili hadi nne.

Baadhi walipewa ARV pekee na wengine walipewa pamoja na sumu hiyo ya 3B3-PE38.

Katika utafiti huo, walibaini kwamba wale ambao walitumia ARV pamoja na sumu hiyo, waliweza kupunguza kwa kiwango kikubwa VVU pamoja na seli ambazo tayari zimeathirika.Taarifa za awali zinaelezwa kuwa sumu hiyo inaweza kusaidia kutibu watu walioathirika na mojawapo ya aina ya VVU

we endekeza uzinzi uje ukione.kama sijapiga hela ya jeneza
 
Back
Top Bottom