Waha /Abaha ni Wanyarwanda?

kwasababu wako karibu na nchi yenye machafuko ! Lakin huwezi kusikia tukiwambia wajaruo ni watu wa kenya au wamakonde ni watu wa msumbiji.

Ni rahisi kumtolea mtu mfano mbaya kuliko mzuri hasa kwene malumbano
Wajaluo Sudan ndiyo wengi na ndy walipotokea na kuja uganda kenya tanzania

Ova
 
Kweli kabisa. Kuna sehemu moja nilitembelea pale Tabora inaitwa Ulyankulu , eneo karibia lote wamejaa warundi. Wengi wamezaliwa hapo wamekulia hapo. Mpaka Sasa wamekuwa watanzania, lakini asili yao ni Burundi.
Dar tu kuna sehemu inaitwa msigani
Kuna warundi kibao wanajifanya wahaa....mrundi asilia akiongea
Tu kama mjanja una uzoefu nao utawajuwa tu

Ova
 
Hebu waachane na vihistoria walio watanzania ni watanzania wasijaribu kabisa .na India iongelee moo?
 
Mkuu, si kweli. Labda,si mzuri sana kwenye hayo mambo ya Historia,ila WAHA wapo. Ukiachilia mbali makabila ya kikoloni ya wahutu na watutsi,makabila hayo ndo yanayotambulika. Kuhusu wametoka wapi ndo sijui. Kama ramani yako ilivyo, kama Rwanda na Burundi miaka hiyo zilikuwa part ya Tanganyika,basi itakuwa ile hama hama ya watu. Maana mpaka mtu awe wa kabila fulani,ni kwamba kuna chimbuko.
Na kama si hivyo, nachosikiaga mie na nahisi ndo chanzo cha huyo Vincent Karega kuyatamka hivo,enzi za ufalme,kuna maeneo ya Tanzania,Uganda na DRC yalikuwa ya Rwanda. Kabla wakoloni hawajakata mipaka.
-Kama ikiwa hivyo,basi kuna uwezekano mkubwa wa kabila hilo kusheya badhi ya vitu na Rwanda.
-Kagera,makabila ya wanyambo,ukweli ni kwamba chimbuko na kuzaliana kuko hukooo.

-Uganda ukisikia wanyankole,walibaki tu huko baada ya mipaka kukatwa.
-DRC, M23 unayosikia, mzizi ni huo huo

Wanaojua haya mambo watujuze zaidi
 
Kagame kama anataka wahaya wenzake aseme ila ardhi tuliyoipigania kutoka kwa wabaganda na kumwaga damu za watanganyika pamoja na wapemba asijaribu kutamka kama ni eneo lake.
 
Lete hoja na viambatanishi si kuongea kutoka hewani mkuu

Ni ujinga kushangaa muingiliano wa makabila ya Mipakani. Hujui kuna wamakonde, wamasai, waluo, wamaasai, wanyasa, wangoni TZ na nchi za jirani? Hujui kuna wasambaa Tanga na Comoro?

Their language is a Bantu language,[5] and is called the Ha language, also called Kiha, Ikiha or Giha. It is closely related to the Kirundi and Kinyarwanda spoken in neighbouring Burundi and Rwanda, and belongs to the Niger-Congo family of languages

Google is free.
 
Neno Ha kwa kiha lina maana ya hapa hapa. Waha au Abhaha ni neno linalotumika kutambulisha koo na kabila la waha. Tafsiri hii ilitokana na majibu ya wazawa wa Buha(Bhuha) walipoulizwa na wageni wa kikoloni kuhusu asili yao, walijibu... "Twebwe tul'abhaaha" ....Hili ni jibu utakalokutana nalo kutoka kwa muha halisi hata vijijini kwenye ardhi yao.

Kabila la waha ni kubwa lenye eneo kubwa linakaribia eneo lote la Rwanda na Burundi ukiziunganisha pamoja.

Bhuha ni himaya ambayo haikuendeleza uwepo wake baada ya waha wengi kuondoka kwa wingi kwenda manamba kwenye mashamba ya katani huko Morogoro na Tanga lakini baadaye Uganda.
Himaya ilijumuisha Bhuha ya kaskazini ambapo kuna Buyungu na Muhambwe wakati Bhuha ya kusini ilijumuisha Heru chini na juu ambayo ndio Kasulu ya sasa na Buhigwe, Bugoye ambayo ndio ujiji ya sasa na Uvinza.

Dhana ya kuwa waha ni wahutu haina ukweli wowote kwa kuwa chimbuko la waha ni koo tofauti na wahutu au watusi. Ukizungumza kiha cha Bhuha ukiwa sehemu yoyote ndani ya Burundi hueleweki moja kwa moja zaidi ya kupata picha ya kile unachowasilisha kupitia maneno yanayofanana lakini yenye maana tofauti. Ukiwa Rwanda ni hivyo hivyo kuelewa muha anasema nini kwa mnyarwanda ni shughuli pevu.
 
Then what next? Mbona Wangoni wametokea Africa ya kusini, wayao Malawi na Msumbiji, Wamakonde Msumbiji... Au hao Waha wanahitajika kwao na wao wanakataa kwenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…