Waha /Abaha ni Wanyarwanda?

Waha /Abaha ni Wanyarwanda?

Then what next? Mbona Wangoni wametokea Africa ya kusini, wayao Malawi na Msumbiji, Wamakonde Msumbiji... Au hao Waha wanahitajika kwao na wao wanakataa kwenda?

Hili swali iulize serikali ya rwanda
 
Neno Ha kwa kiha lina maana ya hapa hapa. Waha au Abhaha ni neno linalotumika kutambulisha koo na kabila la waha. Tafsiri hii ilitokana na majibu ya wazawa wa Buha(Bhuha) walipoulizwa na wageni wa kikoloni kuhusu asili yao, walijibu... "Twebwe tul'abhaaha" ....Hili ni jibu utakalokutana nalo kutoka kwa muha halisi hata vijijini kwenye ardhi yao.

Kabila la waha ni kubwa lenye eneo kubwa linakaribia eneo lote la Rwanda na Burundi ukiziunganisha pamoja.

Bhuha ni himaya ambayo haikuendeleza uwepo wake baada ya waha wengi kuondoka kwa wingi kwenda manamba kwenye mashamba ya katani huko Morogoro na Tanga lakini baadaye Uganda.
Himaya ya hii ilijumuisha Bhuha ya kaskazini ambapo kuna Buyungu na Muhambwe wakati Bhuha ya kusini ilijumuisha Heru chini na juu ambayo ndio Kasulu ya sasa na Buhigwe, Bugoye ambayo ndio ujiji ya sasa na Uvinza.

Dhana ya kuwa waha ni wahutu haina ukweli wowote kwa kuwa chimbuko la waha ni koo tofauti na wahutu au watusi. Ukizungumza kiha cha Bhuha ukiwa sehemu yoyote ndani ya Burundi hueleweki moja kwa moja zaidi ya kupata picha ya kile unachowasilisha kupitia maneno yanayofanana lakini yenye maana tofauti. Ukiwa Rwanda ni hivyo hivyo kuelewa muha anasema nini kwa mnyarwanda ni shughuli pevu.

Big up kwa ufafanuzi mzuri
 
Huu ni wehu flani wa kupenda superior race
Wazenji wote wanadhani waarabu
Waha wengi husema wao watusi

Wanasema watusi ni sawa!!!

Kuna wahamiaji wengi wa kitusi wanaishi kwa baadhi ya wilaya , ambao kiasili ni watusi ila si waha na wamejipa uha kwasababu tanzania haitambui kabila kama watusi kama ni kabila la watanzania ila n wahamiaji na wakimbizi!!

Wilaya kama Manyovu wamejaa huko watusi
 
warundi pia wanaongea lugha ileile ya rwanda. hivyo inawezekana ni kweli, watu wote wa burundi, rwanda, kigoma ni walewale tu ila hiyo haimaanishi kwamba ni wanyarwanda, kwasababu makabila yote ya mipakani yapo pande zote mbili za nchi zilizoko mipakani. hao wameru wa arusha na wamasai hata kenya wapo hivyo hivyo, hao kina mwita hata kenya wapo kwa majina na tamaduni hizo hizo, hao wajaluo, hao wahaya na uganda wanaendana vilevile, hao wanyasa wa malawi na wanyasa wa tanzania ni wale wale hadi kuna kipindi wanyasa wa malawi walikuwa wanataka kujitoa malawi wawe watanzania kwa sababu wanatengwa, wamakonde wapo msumbiji na mtwara, na wayao pia, wazigua wapo tanga na kenya pia. wachaga na wakenya wametenganishwa na mlima tu. kwahiyo kama yeye anasema kigoma ni rwanda hata sisi tuna haki kusema Rwanda ilikuwa Tanzania na tunaweza kuichukua kama vipi.
Kiha kinashabiana kihangaza na kirundi...sio kinyarwanda labda neno moja moja
Ila kinyambo na kinyankole kinashahabiana na kinyarwanda somehow
 
Kama ulizani umesikia yote !! si kweli
View attachment 2810568
Chanzo: Chronicles Rw

UCHAMBUZI!
Taarifa au Tetesi si hii ina ikweli kiasi gani??
Tuanze hapa

Karne ya 18 Pwani ya tanganika ilitawaliwa na mportugue ambaye alitawala pwan yote na baadae muarabu wa oman akamfurusha na kuikalia pwani ya tanganyika! hata hivo ukomo wake haukuhusisha maeneo ya ndani ya Tanganyika

Ujerumani ndio mkoloni wa kwanza kukalia eneo hili na kuliita Koloni la ujerumani
View attachment 2810796

Katika utawala wa mjerumani Rwanda na burundi zilikua Eneo la Tanganyika lililoitwa British East Africa kama inavoonikana kwenye raman.
Baada ya Vita ya kwanza Ujerumani ilipokonywa maeneo yake hivo Uingereza ilichukua eneo ambalo ujerumani mwaka 1920 ililikalia lakini haikuhusisha Rwanda na Burundi.

Hivo hakuna mahala sehemu yeyote ya tanganyika ishawai kuwa sehemu ya rwanda au burundi ila RWANDA NA BURUNDI zilikua sehemu ya tanganyika wakati wa utawala wa ujerumani mwaka tajwa hapo juu.

WAHA
Ni kabila la kibantu linalopatikana Tanzania wanaongea lugha ya Kiha ambacho kina husiana au kukalibiana na kirundi.

Mji mashuhuli kwenye historia ya waha ni ujiji lakini pia Kasuru.

Kiufupi Waha wanapatikana Tanzania kiasili ingawa kilugha wanaweza kuwa wanaingiliana na taifa jirani.
Rwanda na Burundi hamna Kabila la waha hivo hawana kitovu chochote au chimbuko la hizo nchi labda tu kwa kuhamia na kuomba uraia
View attachment 2811177
View attachment 2811180
Kuna kiongozi mmoja alishupalia sera ya majimboism huenda mpango wake mbele ya safari ilikuwa ni kuanzisha Ha teritory
Screenshot_20231114_020845_Samsung Internet.jpg
 
Kama ulizani umesikia yote !! si kweli
View attachment 2810568
Chanzo: Chronicles Rw

UCHAMBUZI!
Taarifa au Tetesi si hii ina ikweli kiasi gani??
Tuanze hapa

Karne ya 18 Pwani ya tanganika ilitawaliwa na mportugue ambaye alitawala pwan yote na baadae muarabu wa oman akamfurusha na kuikalia pwani ya tanganyika! hata hivo ukomo wake haukuhusisha maeneo ya ndani ya Tanganyika

Ujerumani ndio mkoloni wa kwanza kukalia eneo hili na kuliita Koloni la ujerumani
View attachment 2810796

Katika utawala wa mjerumani Rwanda na burundi zilikua Eneo la Tanganyika lililoitwa British East Africa kama inavoonikana kwenye raman.
Baada ya Vita ya kwanza Ujerumani ilipokonywa maeneo yake hivo Uingereza ilichukua eneo ambalo ujerumani mwaka 1920 ililikalia lakini haikuhusisha Rwanda na Burundi.

Hivo hakuna mahala sehemu yeyote ya tanganyika ishawai kuwa sehemu ya rwanda au burundi ila RWANDA NA BURUNDI zilikua sehemu ya tanganyika wakati wa utawala wa ujerumani mwaka tajwa hapo juu.

WAHA
Ni kabila la kibantu linalopatikana Tanzania wanaongea lugha ya Kiha ambacho kina husiana au kukalibiana na kirundi.

Mji mashuhuli kwenye historia ya waha ni ujiji lakini pia Kasuru.

Kiufupi Waha wanapatikana Tanzania kiasili ingawa kilugha wanaweza kuwa wanaingiliana na taifa jirani.
Rwanda na Burundi hamna Kabila la waha hivo hawana kitovu chochote au chimbuko la hizo nchi labda tu kwa kuhamia na kuomba uraia
View attachment 2811177
View attachment 2811180
Neno uraia limeanza kutumika baada ya Uhuru hivyo Waliokuwa wanaishi Tanganyika Walitangaziwa kuwa Wao ni Watanganyika na kama hutaki ondoka Tanganyika wao wakabaki Tanganyika hivyo ni Watanganyika hivyo basi sass tumeungana na Zanzabar hivyo wao ni Watanzania hivyo acha Upuuzi hatuangalii kabila bali ulipozaliwa
 
Me kama Muha wa kigoma naomba Paul Kagame atuchukue tu[emoji855],,CCM wakitoka madarakan aturudishe TZ.
Siyo mpaka uchukuliwe unaweza kwenda tu, halafu kipindi cha operesheni kimbunga ulikuwa wapi kwani, siungeenda tu.
 
Back
Top Bottom