Waha mnalalamikiwa sana na Wahudumu wa Ndege kwa aina hii ya ushamba wenu

Waha mnalalamikiwa sana na Wahudumu wa Ndege kwa aina hii ya ushamba wenu

Ni kweli kabisa Mtani wala hujakosea kwamba Sisi wana Mara ( Musoma ) tunavuta sana Bange / Bangi lakini je umeshawahi kusikia tunalalamikiwa na Watu kama nyie Waha na Wahaya kwa tabia zenu za Kipuuzi katika Jamii? Upo wapi nikuletee angalau ' Vipisi ' viwili tu vya Bangi / Bange uvute ili akili yako ikukae sawa? Na ni hiyo hiyo ' Kitu ' inayowafanya Dada zenu kutupenda na kutung'ang'ania Sisi Wanamume wa Shoka akina Mura.
Mambo yote bana yapo mwisho wa reli, hiyo mipisi yenu tupa kuleee,
 
LOL! Wanalala ghafla na kuanza kuporomosha mashuzi! Ha! haa! haaa!
 
Sijui ni kwanini Watani zangu wengi ni Watu wenye majanga majanga hivi hadi najuta hawa Wazee wetu wa Kale walifikiria nini hadi kutufanya Sisi watu wa Mkoa wa Mara tukawa tukawana na Ujomba na Ushangazi ( Utani ) na haya makabila ya Waha, Wahaya, Wanyiramba, Wanyaturu na Warangi kwani kiukweli wanatutia mno aibu Sisi.

katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa bila ya Wao kujua kuwa waliyekaa nae jirani hapo ni GENTAMYCINE akina Dada fulani mmoja wao akiwa ni Mfanyakazi wa Ndege ile yenye nembo ya Ndege huku mwingine akiwa ni Mfanyakazi wa Ndege moja yenye nembo ya Twiga jana usiku walikuwa wanajadiliana masuala yao ya Kazi ila wote wawili walielezea sana ' changamoto ' zao ambazo huwa wanazipata kutoka kwa abiria hasa wa Kabila la Waha kutoka Mkoani Kigoma.

Zifuatazo ni nukuu mbili tofauti tofauti za hao akina Dada ambao ni Wahudumu wa ndani ya Ndege ya hayo Makampuni mawili maarufu ya Ndege hapa nchini Tanzania na naziweka kama ambavyo nimewasikia mwenywe jana wakitiririka na kuserereka nazo tena kwa hasira kabisa...

Dada wa Shirika la Ndege lenye nembo ya ' Ndege '....." Yaani Shosti nashukuru Mungu Kazi zinaenda tu vizuri na mambo siyo mabaya ila kuna hawa Abiria wa Kigoma hasa wa Kabila hili la Waha sijui kwanini hawastaarabiki kwani wenzao hupanda ndani ya Ndege na Vitabu vya Kujisomea au Magazeti lakini cha kushangaza wao kila wakipanda humu wanapanda na mifuko ya Wali na Samaki halafu Ndege ikishaanza tu kuruka wanaito hiyo mifuko ya Vyakula na kuanza kula wakati Sisi mule huwa tunatoa Vyakula vyetu....."

Dada wa Shirika la Ndege lenye nembo ya ' Twiga '....." Si bora nyie huko Kwenu wakishaingia na hiyo mifuko ya Vyakula wanaitoa na kuanza kula. Huku katika Ndege yetu hawa Waha kiukweli wametuchosha kwani huku wakishaanza kula tu hivyo Vyakula vyao huanza kubishana yaani utakuta mmoja amekaa kule First Class anaanzisha ligi / ubishani na abiria wa Economy huku Chakula kikiwa mdomoni na miba ya Samaki wao wale ikiwadondoka midomoni. Halafu wana tatizo moja sugu sana kwani wakishakula, kushiba na kumaliza ubishani wao ambao ni asili yao hulala ghafla na kuanza Kuwajambia hovyo abiria wengine hali ambayo huwa inatupa sana wakati mgumu Sisi wahudumu....."

Haya naamini kabisa kwamba humu Jamvini JF Watani zangu ' Waha ' mpo wengi hivyo haraka sana naomba mjitokeze kujibu hizi ' Shutuma ' la sivyo hawa Dada zenu tuliwaoa huku Mkoani Mara ( Musoma ) sasa hivi tuwaacha na kuwapa ' talaka ' ili warudi huko Kwenu Mkoani Kigoma mfundishane vizuri ' maadili '. Na hivi mnavyotupenda Wanaume wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) sijui kama tukiwaacha mtapata tena Waume wa Kuwaoa.

Waha na wana Mkoa Kigoma badilikeni upesi!

Nawasilisha.
Kwanza unapaswa kujua kuwa Waha wanathamini sana vyakula vyao, na pili kula, kushiba na kuanza kujamba ni mfumo wa mwili. Sasa hapo hao Dada wanaona vyakula vyao haviliki wanaanza kulalama.
Na Gentamycine kama umemuoa Muha umepata Bahati sana. Waha hawakeketi, wa kwenu wanakeketa, so furahia maisha hayo.
 
Waha wanatuangusha mno wana Kanda ya Ziwa. Hivi mtaingiaje katik Ndege na Vyakula vyenu mmeweka katika mifuko myeusi halafu Ndege ikiwa tu angani mnaanza kula hovyo hovyo hadi ' kuwakera ' abiria wengine? Wabadilike upesi sana.
Hiyo siyo kosa, vyakula vya kwenye ndege ni karoti, nyanya, pilipili hoho na mikate, sasa watu waache kula migebuka na ugali wa Lowe kwa ajili ya madasa nayo, haina maana. Ni kheri mtu aonekane mshamba lakini anafaidi maisha kwa mfumo wake
 
Naona ' Washamba ' mnaoongoza nchini Tanzania sasa mmeamka. Na nilikuwa nawatamani na nawasubirini kwa hamu sana mje humu Jamvini JF niwaseme. Hivi nyie aliyewaambieni kuwa katika Ndege hizi huwa hakuna Vyakula ni nani hadi muwe mnafungisha ' mivyakula ' yetu katika mifuko myeusi na kuja kuifungua Ndege ikiwa angani na kuanza Kula hovyo na mkishiba mnaanza ' Kuwajambia ' abiria wengine hadi mnawakera?

Waha badilikeni upesi mnatuaibisha Sisi Watani zenu wana Mkoa wa Mara na wana Kanda ya Ziwa. Na leo mtanikoma humu kama nilivyowanyoosha jana Watani zangu wengine ' Wahaya ' kwa Kosa la mwenzao Ruge Mutahaba kulilia na kuipengea Kamasi ' Mbunye '.
Ekaye mutama, niko tuli. Wala ntiwotuyobhola.
 
Nikikumbuka miaka ya 90' waha walikuwa wanaposafiri ndani ya Treni lazima wanakuwa wamejitwisha mzigo kichwani ss sijui ulikuwa ushamba
 
Hahahahahah nilikuwa na Imagine yani inavyokuwa pale first class akiteta na economy class huku akizingatia miiba ya samaki.
 
bora kwenye ndege hawa waha kwenye treni wanakunyaga kabisa

Mkuu umeharibu kabisa ' mbavu ' zangu kwa Kunichekesha na hakyanani ' Waha ' wenyewe wakija na wakiona hii post yako hawatakuacha salama hivyo anza kujiandaa Kisaikolojia kwani umewapiga ' dongo ' kali na la mwaka. Nimecheka mno Mkuu.
 
Wanapitishia wapi hicho chakula hadi waingie nacho
 
Mkuu umeharibu kabisa ' mbavu ' zangu kwa Kunichekesha na hakyanani ' Waha ' wenyewe wakija na wakiona hii post yako hawatakuacha salama hivyo anza kujiandaa Kisaikolojia kwani umewapiga ' dongo ' kali na la mwaka. Nimecheka mno Mkuu.
[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom