PostGE2025 Wahadhiri Dini ya Kiislam: Lissu aliposhambuliwa Dodoma, TEC hawakutoa tamko sababu rais alikuwa Mkatoliki; Ushahidi wa Tamko la TEC

PostGE2025 Wahadhiri Dini ya Kiislam: Lissu aliposhambuliwa Dodoma, TEC hawakutoa tamko sababu rais alikuwa Mkatoliki; Ushahidi wa Tamko la TEC

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wanaowatukana hawa mashekh wapo sahii

Ni mashekh wapumbavu sana
Shehe ponda na kuna mashehe wengine walitoa walaka wao wapo sahihi wanajua kudai haki na wasema kweli ni tofauti na mashehe njaa majini ubwabwa wa kule Bakwataccm ambao ni wanafiki sana na wajinga mno
 
Narudia tena, hawa masheikh tuwaachie kutangaza muandamo wa mwezi tu, elimu dunia ni watupu kabisa.

Umeona hiyo confidence aliyonayo hapo, hapo ukimuongezea plate mbili tu za ubwabwa anamkana hadi Mtume.
 
Kuna maoni nilisoma mtu akishauri kuwa, Hawa Masheikh na Wanazuoni wanaojitokeza kushambulia TEC wanazidi kuharibu kwani wanaongea hisia badala ya Logics. Nimemsikiliza huyu Sheikh anasema kuwa Lissu alishambuliwa Dodoma, lakini TEC hawakutoa tamko lolote sababu Rais alikuwa Mkatoliki. Katika kumbukumbu zangu, TEC walitoa tamko kulaani tukio hilo pamoja na mengine ya utekaji wakati wa awamu ya Tano.

Nimalizie kwa kusema, BAKWATA na wanaokuja kukosoa tamko wachimbe vizuri kwanza ili kujiridhisha, vinginevyo wanaendelea kuonesha kuwa wana ajenda zao za siri.


USHAHIDI

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limelaani shambulizi la hivi karibuni lililotekelezwa na watu wasiojulikana dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mbunge huyo aliyejeruhiwa Septemba 7 kwa kupigwa risasi tano mjini Dodoma, hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Nairobi nchini Kenya.

Baraza pia limeungana na Watanzania kulaani kwa nguvu zote matendo yote ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani nchini.

Tamko la baraza hilo lililosainiwa na Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Beatus Kinyaiya limetolewa baada ya kikao cha kawaida cha baraza kilichofanyika kwa siku mbili Septemba 9 na 10 jijini Dar es Salaam.

“Katika Taifa letu sasa tunashuhudia matendo ya mauaji ya watu wasio na hatia kama ilivyokuwa kule Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, utekaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na hivi karibuni shambulio la mbunge Lissu,” limesema baraza katika tamko hilo.

Imeelezwa vurugu na mashambulizi ya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa kwa kuwa matendo hayo ni dhambi, uhalifu na si utamaduni wa Mtanzania, hivyo vyombo vinavyohusika havina budi kuyakomesha mara moja.

Na lete la kuwazui waumini wao kushiriki uchaguzi 2020 pamoja na kuhamasisha maandamano ya kuvuruga uchaguzi, hilo ndilo watu wanasema
 
Bakwataccm ipo uvunguni mwa ccm Unaishi na nyoka
Wanasiasa ndio walivyo kwani hata maaskofu mbona wapo huko ccm wengine washateuliwa katika kamati kikubwa hizi taasisi za kidini zingejitenga na siasa mnyukano ubaki kwa wananchi na vyama vya siasa

Assume leo hii Bakwata au Tec waongelee sheria za mpira na uonevu wa timu ya Simba dhidi ya yanga hata wewe utashangaa

Siasa ni ushabiki ila dini ni Imani, siasa na dini ni vitu viwili tofauti na ndio maana Serikali haina dini
 
CCM banaa naona kila mbinu imeshindikana ya kuwagawa watanzania na sasa wameingia kwenye udini.
Hii ndiyo Gia ya mwisho wanayoitegemea...
Miaka 70 ya CCM kuishi hapa duniani imefika mwisho tunakumbusha kuwa Tanzania ya Leo huwezi kuigawa Kwa misingi ya dini, hawa wacheza sinema wa bakwata waambieni warudi tena kuandaa movie nyingine
Uzuri waislam wa kweli waadilifu wacha mungu wapenda haki wenye weledi mkubwa hawaitaki hawaipendi Bakwata kamwe ndiyo maana propaganda za UDINI za Bakwataccm zimefeli mara zote, kila wakipandikiza udini wanafeli, njaa ya Bakwata ni janga la Taifa
 
Hao watu huwa ni mihemko inawaongoza ila kichwani hamna kitu
 
Hawa wapuuzi na uwezo wao mdogo wa kifikiria wanachokifanya ni kuhalalisha ushetani wa Samia kwa kulinganisha na maovu ya magufuli, halafu wanahubiri amani.. ovyo sana hawa watu
 
Udini na mambo ya hovyo vinatengenezwa na kusambazwa Bakwata ya ccm na Mashehe njaa majini ubwabwa ambao IQ zao ni zero 0.00 hawana Elimu wala kazi mda mwingi ni kushinda vibarazani kubuni upumbavu ili wapate kisingizio cha kwenda kuchukua pesa kwa maccm, maisha yao ni unafika fitna majungu na propaganda mda wote
 
Uzuri waislam wa kweli waadilifu wacha mungu wapenda haki wenye weledi mkubwa hawaitaki hawaipendi Bakwata kamwe ndiyo maana propaganda za UDINI za Bakwataccm zimefeli mara zote, kila wakipandikiza udini wanafeli, njaa ya Bakwata ni janga la Taifa
Hao wanaotetea haki si ndio hao baadae mnawaita magaidi hizi manipulation za kidini hazina maana kwa kipindi kama hiki maana unafiki ni mwingi sana

Sheikh ponda kipindi kile cha uamsho alionekana gaidi na mtu anaestahili kifo eti sasahivi ni shujaa yani watu mnajichomeka kila sehemu mnayoungwa mkono ili kusukuma agenda zenu na mtu asiyetumia akili atawafuata bila kuchanganua mambo
 
Kuna mbulula mmoja kobazi anasema tamko la TEC la sasa lina page nyingi kuliko la kipindi cha lisu
Jinga kbs hao, kwa hivyo rais akiwa wa dini yako akifanya upumbavu kama kuua watu wasio na silaha wanakaa kimya kumtetea?

Kwani uislam (dini) ndio ilimtuma kufanya hivyo??.

Bakwata punguzeni kuwa wajinga, mnauaibisha uislam!
 
Bora wabaki hao hao kwenye Bakwata kwa maana BAKWATA ikiwa na masheikh wenye elimu ya dini na extremist ambao kwa kiasi kikubwa pia Wana elimu dunia nchi haitakalika hii amini nakwambia ndio maana ccm haitaki waislamu wanaojielewa kwenye Bakwata jaribu kufuatilia jumuia ya kiislam kabla ya Bakwata ambayo Nyerere kaiua unajua kwanini kaiua?
Hapana sijui.
 
Ukitaka kuwapata mashehe pika ubwabwa nyama na pilau nyama. Ziwepo pilipili za kutosha, kachumbari na ndizi mbivu wapikie uwape bure halafu waambie chochote unachotaka watafanya.
 
CCM banaa naona kila mbinu imeshindikana ya kuwagawa watanzania na sasa wameingia kwenye udini.
Hii ndiyo Gia ya mwisho wanayoitegemea...
Miaka 70 ya CCM kuishi hapa duniani imefika mwisho tunakumbusha kuwa Tanzania ya Leo huwezi kuigawa Kwa misingi ya dini, hawa wacheza sinema wa bakwata waambieni warudi tena kuandaa movie nyingine
Hata huku watashindwa tu. Kwa sababu hata kwenye huo udini siyo Waislam wote wana akili finyu kama za hawa wapuuzi wachache wanaotumiwa na wahuni wa ccm kuleta taharuki na mgawanyiko wa kidini.

Mimi kama mimi ninachojua adui yangu ni ccm! Kwa hiyo hata Rais awe ni malaika, bado nitampinga tu mpaka pale ccm itakapozikwa rasmi kaburini.
 
Kiongozi Mkuu wa Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania Sheikh Rajab Salum amepinga vikali tamko lililotolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu uvunjifu wa amani uliojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema baraza hilo lina ajenda ya siri waliyoificha na kulitaja kama baraza la kueneza ubaguzi kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 19, 2025 Jijini Dar es Salaam, Sheikh Salum amelaani pia lugha iliyotumiwa na baraza hilo katika waraka wake ikiwamo maneno ya 'Taifa kujeruhiwa na kupoteza heshima yake' akisema ikiwa kweli walikuwa na nia njema walipaswa kueleza madhaifu dhahiri waliyoyaona ikiwemo kwa waandamanaji na kushauri namna nzuri ya kuandamana na serikali inavyopaswa kuwajibika kwa waandamanaji.

Akieleza kuwa TEC hawakuwa na msingi wa kweli wa kupigania haki nchini, Sheikh Salum amerejea pia baadhi ya matukio yaliyotokea nchini kwa miaka ya nyuma, akihoji ilipokuwa sauti ya TEC katika kukemea masuala hayo yaliyosababisha adha kubwa kwa wananchi ikiwemo vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.

"Mfano mzuri tu ni katika serikali ya awamu ya tano, kulikuwa na mambo mengi na ya kutisha, watu wakifungwa midomo na uhuru wa habari ukiminywa na zaidi ni shambulio la mwanasiasa mmoja (Tundu Lissu) pale Dodoma. TEC mlikuwa wapi kusema chochote? Haya yote yanatupa ukumbusho mzuri kuwa baraza hili lina ajenda ya siri waliyoificha." Amesema.

Sheikh Salum pia amerejea matukio yaliyotokea katika kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya tatu nchini, ikiwemo mauaji wakati wa maandamano, suala ambalo lilisababisha mamia ya wananchi kukimbilia Kenya, Canada na Mataifa mengine.

Ameeleza pia kuhusu mauaji ya Januari 27, 1995 ikiwemo Masheikh kupigwa risasi na kuuawa wakitoka misikitini sambamba na mauaji ya mwaka 1998 kwenye msikiti wa Mwembechai Magomeni mkoani Dar es Salaam, akisema yote hayo yamedhihirisha namna ambavyo TEC inatumika kueneza ubaguzi nchini.
 
Back
Top Bottom