A
Anonymous
Guest
Napenda kuwasilisha hoja kuhusu changamoto inayowakabili Wahadhiri wengi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika mchakato wa kupandishwa vyeo.
Kwa sasa, Wahadhiri wengi wamekwama kutokana na sharti la mfumo wa PEPMIS (Performance Evaluation and Project Management Information System), licha ya kuwa wametimiza vigezo vya msingi vya kitaaluma vinavyotambulika na mamlaka husika.
Wahadhiri hawa wamewekeza muda, nguvu na rasilimali nyingi katika kutekeleza majukumu yao makuu ya ufundishaji (teaching), utafiti (research) na ushauri elekezi (consultancy), wamefanikiwa kukusanya alama zinazohitajika kwa mujibu wa miongozo ya TCU na NACTVET.
Kimsingi, maeneo haya matatu; utafiti, ushauri elekezi na ufundishaji ndiyo nguzo kuu zinazotumika kimataifa katika kutathmini maendeleo ya kitaaluma na kustahili kupandishwa vyeo kwa wahadhiri. Hata hivyo, pamoja na wahadhiri wengi kutimiza vigezo hivyo, bado wameendelea kukosa fursa za kupandishwa vyeo kwa sababu ya kutokidhi matakwa ya mfumo wa PEPMIS.
Ni muhimu kutambua kuwa PEPMIS ni mfumo mpya ambao bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiufundi na kiutendaji. Aidha, bado kuna watumishi wengi ambao hawajapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake na namna unavyotumika katika tathmini za utendaji kazi.
Kutokana na hali hiyo, tunashauri Serikali itoe nafuu ya muda kwa kusitisha matumizi ya PEPMIS kama kigezo cha lazima katika mchakato wa kupandisha vyeo hadi pale mfumo huo utakapokuwa umeimarishwa, changamoto zake kutatuliwa, na watumiaji wake kupata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake.
Katika kipindi hiki cha mpito, tunapendekeza tathmini za kupandisha vyeo ziendelee kuzingatia vigezo vya kitaaluma vinavyotambulika kimataifa na kitaifa, ambavyo ni utafiti (research), ushauri elekezi (consultancy), na ufundishaji (teaching/training).
Hatua hii itasaidia kuhakikisha kuwa wahadhiri wanaostahili hawanyimwi haki zao za maendeleo ya kitaaluma kutokana na changamoto za mfumo ambao bado uko katika hatua za awali za utekelezaji.
Tunaamini kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha morali ya watumishi, kuongeza tija katika taasisi za elimu ya juu, na kulinda haki za wahadhiri ambao wamefanya kazi kwa bidii na kukidhi vigezo vya kitaaluma vinavyohitajika.
Pia soma ~ Prof. Shemdoe: Uzembe wa Ma-Afisa Rasilimali Watu katika Mfumo wa PEPMIS umezuia Watumishi kutopanda daraja