Wahadhiri vilaza huzalisha wasomi vilaza

Hapo penye nyekundu nakubaliana nawe. Kuhusu hiyo paper ya "SUA" naamini nahitaji kujua details za hiyo course na vitu vingine (kama nilivyo changia hapo juu), na pia walengwa wanahitaji knowledge na depth ya Principles of Food Processing and Preservation ya kiasi gani kujua ubora wake. Kwa mfano hii paper ingekuwa ni kwa wanafunzi wa food science na technology huenda tungetegemea maswali ya undani zaidi kuliko ilivyo hapa kwa general agriculture (elective).

Kwa mfano wako wa immunology namba 2 ni kuhusu terminolgy where as number 1 I believe ni a fundamental concept ya jinsi ya immune system inavyokuwa fired na antigen-specificty/heterogeneity na clonal expansion so ni ya undani zaidi. Of course swali ni wewe mwalimu unatafuta nini, objectives za course, stage ya course uliyofikia, na aina ya wanafunzi (utanisamehe kama immunology yangu imekuwa stale early 80's).

Kwa kuwa mleta mada alizungumza na rafiki yake mhadhiri wa SUA ningetegemea mfano aliotoa kuelezea uwapo wa walimu vilaza ungekuwa na nyama zaidi.

Baada ya kusema yote haya kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na walimu "vilaz.a" hata vyuoni hivyo vyuo na TCU viwe macho na system ya external examiners ipewe mkazo stahiki. Elimu ya kufundisha hasa kwa wasiopitia elimu hiyo ambao ni wengi vyuoni nayo tusi ipuuze.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. You are very right and bright, I can say! . Nadhani wewe ni mwalimu wa zamani kama ni wa siku hizi umejitahidi kusoma na kuelewa..... the saying goes : Teacher can teach, students can refuse to learn; and vice versa!

We nimekukubali, kama ni miaka ya 80 bado uko hivyo, uko vizuri. Looks you were good at Immunology kama ni kwenye 80's and you have not been practicing since then. ........ Three cardinal characteristic of an immune system :specificity, memory and self and nonself recognition/discrimination..... landa vimeongezeka vingine with advance of science.
 
Wengine wengi ni GPA za kutumia nguvu za ziada. ..they don't flow naturally. Rarely we encounter those lecturers that you go out with something....the look of Prof Materu who was at the faculty of engineering...Prof. Luhanga kama akiacha makidai yake. ..Prof Mshoro ambaye I salute with ovation because he is the genius etc
 
Great-nami nimejifunza kupitia uzi huu. Nimependa umeifanyia kazi na haki hii topic I wished majadiliano hapa yangekwenda na ku-dig taarifa. Thanks
 

Umeongea kweli mkuu,kuna siku nilikua naongea na mzee mmoja aliesoma na JK. Aliniambia Elimu ya sasa haina nyuma wala mbele,matatizo halisi ya elimu hayatazamwi,bali wanangaika na vimvuli vyao.
Alinieleza jinsi gani elimu ya shule ya msingi ilivyokua inawajenga katika kuongea,kuandika na kujieleza kwa lugha zote mbili. Sasa hivi mwanafunzi wa shule ya msingi hawezi kujielezea mwenyewe,lakini ukimpa mtihani anafaulu. Inaonyesha jinsi gani wanafunzi wanakariri ili wafaulu tu.
Jambo lingine alilonieleza ni kubadilishwa kwa vyuo vya ufundi na vyuo maalum kama IDM (Mzumbe),MUST(Mbeya Technical college) kuwa vyuo vikuu. Vyuo kama IDM,IFM,DIT,ATC,MTC ndio vyuo vilikua vinaongoza kwa kuzalisha watendaji wakubwa wa serikali lakini baadhi ya vyuo hivyo vimebadilishwa na kuanza kufundisha kama vyuo vikuu wakati halikua lengo halisi la hivyo vyuo na kuchangia kupungua kwa wataalam watakaofanya kazi serikalini.
Yako mengi sana tunatakiwa kuyaondoa/kuyaongeza kwenye huu mfumo wa sasa wa elimu hili tupate elimu iliyobora.
 
Kweli kabisa mkuu.

Au hivi: CCM = Chama Cha.........
 
Mkuu hapa naona umetuletea STUDY SKILLS. Maswali yako wapi?
 
Kwahiyo una maana mhadhiri akitunga mtihani mgumu ndio anaonekana kipanga!?
Akitunga mtihani mgumu ndio anakuwa amemsaidia mwanafunzi kujifunza, sio kwa kumkaririsha madude ya kipuuzi ambayo hayana impact ktk maisha ya mwanafunzi.
 
Hata kama alikuwa anapima oil mtihani huu haukubaliki kwa level ya chuo kikuu.
Kwa namna yoyote mtihani (upuuzi huu) haukubaliki kwa level ya Chuo Kikuu, labda kwa hivi vya kipuuzi vya kuchipua kama uyoga
 
Umetoa maada nzuri ila inaelekea muoga.Binafsi napenda mabadiliko ila usiangalie question paper anza kuangalia mtaala unataka kutengeneza watu kwa kiwango gani ndo uangalie mtihana unavyotungwa.
 
Umetoa maada nzuri ila inaelekea muoga.Binafsi napenda mabadiliko ila usiangalie question paper anza kuangalia mtaala unataka kutengeneza watu kwa kiwango gani ndo uangalie mtihana unavyotungwa.
Mkuu kwa hiyo kumbe mtaala unakusudia kutengeneza VILAZA?
 
Sijawahi kuona nchi yenye elimu ya kijinga na kipumbavu kama Tanzania
 
Reactions: qqq
Nchii hii ngumu sana ndugu yangu, matatizo kila kona
 
Tangu serikali ya CCM ilipoanza kuingiza siasa kwenye elimu, ubora umekuwa ukishuka kila siku na ukishuka serikali nayo huingiza mkono wake kwa kuamuru mitihani irahisishwe na isahihishwe kwa juu juu.....hata kama mwanafunzi ameandika jibu la kipuuzi, apewe tiki na makisi kedekede!!! 😳 😳 😳 😳
 
Elimu ya nchi hii inazidi kudidimia kila kukicha.
 
 
Wanafunzi hawa wa shule za kata walioanguka mtihani wa NECTA ni zao la wahadhiri vilaza kama hawa wa SUA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…