PostGE2025 Wahadhiri wa Kiislamu: Waislamu msijihusishe na Maandamano ya Disemba 9

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Jumuiya ya Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania imewataka Waislamu wote nchini pamoja na Watanzania kwa ujumla kujitenga na hamasa na ushiriki wa maandamano yanayohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii nchini ya Disemba 09, 2025 yakidaiwa kuratibiwa na Watanzania wasioishi nchini.

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania Sheikh Rajab Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2025, akiyataja maandamano hayo kuwa batili na jambo lisilokubalika nchini.

Sheikh Salum pia akitaja ajabu ya maandamano hayo kuwa yanaratibiwa na watu wasioshiriki na wanaoishi nje ya Tanzania, amewataka wale wote wanaohamasisha maandamano hayo kurejea nchini ikiwa wana nia njema ili kuja kujumuika na Watanzania.

"Kuna maandamano yanadaiwa kuratibiwa Tarehe 09 Disemba. Ajabu ya maandamano haya ni kuwa wanayoyaratibu wako nje ya nchi, kuna dada mmoja yupo Marekani na mwingine akiwa nchini Kenya, niombe na nitoe angalizo kwa Waislamu kwamba msijihusishe kabisa na haya mambo na niwaombe hawa wanaohamasisha warejee nchini tuje tushiriki wote." Amesema Sheikh Salum.

Jumuiya hiyo ya wahadhiri inaungana na Jumuiya nyingine za Kiislamu ikiwemo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) pamoja na madhehebu mengi ya Kikristo nchini kulaani uvunjifu wa amani, uharibifu na wizi wa siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakiwataka waumini wao kujitenga na vurugu na hamasa hizo na kuunga mkono hatua za maridhiano zilizoanza kuchukuliwa na serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 
"Kuna maandamano yanadaiwa kuratibiwa Tarehe 09 Disemba. Ajabu ya maandamano haya ni kuwa wanayoyaratibu wako nje ya nchi, kuna dada mmoja yupo Marekani na mwingine akiwa nchini Kenya, niombe na nitoe angalizo kwa Waislamu kwamba msijihusishe kabisa na haya mambo na niwaombe hawa wanaohamasisha warejee nchini tuje tushiriki wote." Amesema Sheikh Salum.

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania Sheikh Rajab Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2025, akiyataja maandamano hayo kuwa batili na jambo lisilokubalika nchini.

Tuwekee CV ya huyo Sheikh Salum.
 
Mimi ni muislamu ila ni bora niimsikilize mlevi au mtoto mdogo wa chekechea kuliko kusikiliza hao
Vichaa wanafiki wazee wa ubwabwa wanaojali vyakula vyao kuliko hata damu za watu

Na nitoe angalizo sio Kila anaevaa kanzu na kofia anatuwakilisha sisi waislam hao waende wakawasemee CCM sio sisi waislam hatuwataki hatuwapendi wanafiki hao
 
Ni mhadhiri wa chuo au msikiti?
Hizo akili zake ni za ubwabwa yaani maandamano hayakubaliki ila mauaji ni sawa?
 
Mimi si Mwislam ila sheikh Salum Rajabu umetoa neno la hekma.
Upewe maua Yako sheikh na jumuia yenu kwa ujumla.

Nchi ipo katika taharuki ya kuingia katika machafuko na Kuna Nchi Mafisi zinasubiri kwa hamu kinuke ili Zifaidike na mgogoro.
 
"Kuna maandamano yanadaiwa kuratibiwa Tarehe 09 Disemba. Ajabu ya maandamano haya ni kuwa wanayoyaratibu wako nje ya nchi, kuna dada mmoja yupo Marekani na mwingine akiwa nchini Kenya, niombe na nitoe angalizo kwa Waislamu kwamba msijihusishe kabisa na haya mambo na niwaombe hawa wanaohamasisha warejee nchini tuje tushiriki wote." Amesema Sheikh Salum.

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania Sheikh Rajab Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2025, akiyataja maandamano hayo kuwa batili na jambo lisilokubalika nchini.
Kina Sheikh Takadir walipambana na mkoloni aliyekuwa akionea wananchi lakini masheikh wa siku hizi wakishapewa bahasha za khaki wanatema upupu tu.
 
Hawa mashekhe ubwawa walio tuletea wanazidi kuchochea moto na kupromo maandamano zaidi wanazima moto kwa kuongeza mafuta wataungua.
 
"Kuna maandamano yanadaiwa kuratibiwa Tarehe 09 Disemba. Ajabu ya maandamano haya ni kuwa wanayoyaratibu wako nje ya nchi, kuna dada mmoja yupo Marekani na mwingine akiwa nchini Kenya, niombe na nitoe angalizo kwa Waislamu kwamba msijihusishe kabisa na haya mambo na niwaombe hawa wanaohamasisha warejee nchini tuje tushiriki wote." Amesema Sheikh Salum.

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa Wahadhiri wa Kiislamu nchini Tanzania Sheikh Rajab Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2025, akiyataja maandamano hayo kuwa batili na jambo lisilokubalika nchini.

Huyu shekhe ubwabwaanawadharau sana waislam! Anawaona waislam hawana uwezo wa kutafakari na kuamua ni nini kilicho sahihi kwao, mpaka waambiwe na shekhe wa mchongo!
 
Masheikh mnakosea msiwazuie hao nyumbu kufanya hayo machafuko, nchi yetu inatakiwa ifanye operation maalumu ya kuwatanguliza akhera hao nyumbu, na hamna njia nyingine inayotoa justification ya kuwaua zaidi ya wao kufanya hizo vurugu, tunaomba waachwe watoke waharibu na kuiba mali za watu ili serekali ipata sababu halali ya kuwaua.
 
Wanataka kuifanya hii ni vita ya kidini but one thing I know for sure the foundation of GOD is justice.Misingi ya Mungu ni haki.Tumeshashinda.
 
Kwa kua mimi na uislam wangu silipi kodi?kwa kua mimi na uislam wangu naishi maisha mazuri nnayostahili kulingana na rasilimali zilizokuwepo?au uislam ndio unafurahia mauaji?dhulma na laghai za viongozi?
Yaani hawa watu si bora wakae kimya kuliko kuropokwa ropokwa hovyoo
 
Back
Top Bottom