Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
✍️Mara nyingi tunapozungumzia taharuki au vurugu wengi hufikiria ni suala la kisiasa pekee .
Lakini ukweli ni kwamba nyuma ya matukio hayo huwa kuna kundi la wahalifu wanaosubiri mazingira ya sintofahamu ili kutekeleza uhalifu wao.
Hawa hawana ajenda ya kujenga Taifa wala kutetea maslahi ya wananchi lengo lao ni kutumia fursa hiyo kuiba mali za watu kupora biashara na kusababisha hasara kwa wananchi wasio na hatia.
Ni muhimu tukatambua kwamba anayepoteza mali katika mazingira kama haya mara nyingi ni mwananchi wa kawaida.
Ni mfanyabiashara aliyekopa mtaji benki mama lishe anayehangaika kulisha familia yake bodaboda anayepambana kutafuta riziki au kijana anayejitafutia kipato kwa njia halali.
Mali hizo hazikupatikana kwa urahisi zimepatikana kwa jasho muda na kujinyima kwa muda mrefu.
Kwa hiyo tuwe makini tusitoe nafasi kwa wahalifu kujificha ndani ya umati au kutumia taharuki yoyote kama mwanya wa kutenda uhalifu.
Uzalendo wa kweli haupimwi kwa maneno pekee bali pia kwa namna tunavyolinda usalama wa watu mali zao na utulivu wa Taifa.
Tuwe macho tutoe taarifa kwa mamlaka husika pale tunapoona viashiria vya uhalifu na tuwahimize wenzetu kutanguliza amani busara na kuheshimu sheria.