The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanikiwa kumpata mtoto mwenye umri wa miezi sita aliyechukuliwa na watu wasiojulikana, baada ya kuvamia nyumba ya Melksedek Mrema na mkewe Joan Gabriel, ambao nao wakati wa tukio hilo walitupwa kwenye mashimo ya choo, kabla ya watuhumiwa kuondoka na mtoto huyo.
Soma pia: Kibaha: Waiba gari, kichanga na kuwatumbukiza wazazi kwenye shimo la choo
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcane amesema majira ya saa 9.00 usiku wa kuamkia leo Januari 24, 2025, katika eneo la Kimalamisale, mtaa wa Serengeti B uliopo Kata ya Dutumi, Kibaha vijijini waliwakamata wanaume watatu na mwanamke mmoja aliyekutwa na mtoto huyo wa kike na gari Toyota IST.
Amesema baada ya kumpata mtoto, walimpeleka katika Hospitali ya Tumbi kwa uchunguzi Zaidi, kisha atakabidhiwa kwa wazazi lakini kwa sasa yupo sehemu salama zaidi.
Watuhumiwa wote wapo kituo cha polisi na uchunguzi unaendelea.