Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?
Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ndio tumeamua sasa hivi kila mtu kuwa chawa ili naye aende kula kwa urefu wa kamba yake?
Vijana tuamke kuokoa taifa hili, kwa haya yanayoendelea na nchi itafutika kwa kila mtu kuchota kwa nafasi yake bila kujali maslahi ya nchi.
===
Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi Tanzania umemnunulia Helkopta Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aitumie Helkopta hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakani (2025) atakapokuwa anapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi Julai 20.2024 Msemaji wa umoja huo Mhandisi Yuda Thomas Kemincha amesema sambamba na kununua Helkopta hiyo lakini pia wametoa mafuta ya shilingi milioni 100 za Tanzania, huku akitumia nafasi hiyo kufafanua kuwa hatua hiyo inakuja kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia kuhusiana na yale aliyoyafanya nchini.