Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ndio tumeamua sasa hivi kila mtu kuwa chawa ili naye aende kula kwa urefu wa kamba yake?

Vijana tuamke kuokoa taifa hili, kwa haya yanayoendelea na nchi itafutika kwa kila mtu kuchota kwa nafasi yake bila kujali maslahi ya nchi.

===

Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi Tanzania umemnunulia Helkopta Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aitumie Helkopta hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakani (2025) atakapokuwa anapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi Julai 20.2024 Msemaji wa umoja huo Mhandisi Yuda Thomas Kemincha amesema sambamba na kununua Helkopta hiyo lakini pia wametoa mafuta ya shilingi milioni 100 za Tanzania, huku akitumia nafasi hiyo kufafanua kuwa hatua hiyo inakuja kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia kuhusiana na yale aliyoyafanya nchini.

Tuendelee kuwapa Wachina hizi kandarasi sisi bado ni wa mambo madogo madogo kama haya ya uchawa!!
 
Watu wa twitter wanasema mbona kama mheshikiwa engineer ni chawa mwandamizi hivi eti kwenye umoja wa wahandisi hayupo
 
Attachments

  • Screenshot_20240721-110236.png
    Screenshot_20240721-110236.png
    1.2 MB · Views: 1
1. Kuna uwezekano wanahitaji aendelee kuwepo maana kuna manufaa wananufaika nayo.

2. Hiyo chopa hiyo hiyo chopa hiyo, isije ikawa ni mouse trap, ikapindua meza na kuandika historia nyingine mbaya.

3. Propaganda
 
Wahandisi wenyewe sasa....
IMG_20240722_170027.jpg
IMG_20240722_170024.jpg
 
Attachments

  • IMG_20240722_170024.jpg
    IMG_20240722_170024.jpg
    29.6 KB · Views: 1
Hiyo sio Rushwa kweli?🤔

..hata KIUSALAMA haiko sawasawa.

..Samia kwasababu ni Rais anapaswa kusafiri kwa kutumia vyombo vya umma wakati wote.

..Wakandarasi wasubiri 2030 ambako mgombea wa Ccm atakuwa bado hajawa Rais, na wakati huo watatakiwa waichangie Ccm kununua helikopta.
 
Kwa kweli huu ni ujinga wa hali ya juu. Sikujua kwamba tuna wahandisi wajinga namna hii. Halafu unaweza kuta kuna mtu hata siyekuwa raia halisi ndiye ametoa hili wazo, nia yake ni nani anaijua vizuri? Usalama wa Taifa sitegemei wakubali jambo la kijinga kama hili. Tena jambo hili linadhalilisha Ikulu yetu kwa ujumla. Waelekezwe wakakarabati Mahospitali na shule nyingi hazina hata vyoo, watoto wanajisaidia vichakani au vyoo vya shimo halafu mhandisi unakuja hapa kutuambia unamnunulia Raisi Helicopter?? Ningewaona wana akili timamu kama wangeweka lengo la kuunda hiyo Helicopter wao wenyewe, tujue wanataka kujitanabahisha kuwa ni wasomi wabobevu. Shame on you all!
 
Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ndio tumeamua sasa hivi kila mtu kuwa chawa ili naye aende kula kwa urefu wa kamba yake?

Vijana tuamke kuokoa taifa hili, kwa haya yanayoendelea na nchi itafutika kwa kila mtu kuchota kwa nafasi yake bila kujali maslahi ya nchi.

===

Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi Tanzania umemnunulia Helkopta Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aitumie Helkopta hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakani (2025) atakapokuwa anapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi Julai 20.2024 Msemaji wa umoja huo Mhandisi Yuda Thomas Kemincha amesema sambamba na kununua Helkopta hiyo lakini pia wametoa mafuta ya shilingi milioni 100 za Tanzania, huku akitumia nafasi hiyo kufafanua kuwa hatua hiyo inakuja kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia kuhusiana na yale aliyoyafanya nchini.

Kuna vituko vingi sana....
 
Najiuliza kwanini Samia anaanza kampeni mapema namna hii? ana lengo gani na hii nchi?

Hivi wakati huu ambapo mambo yanajiendea hovyo kila kona, juzi tu amesema anataka kuanza kuchimba madini yaliyogundulika kwenye mbuga ya Serengeti eti kwasababu wanyama hawali madini!

Hii ndio akili inayolazimisha kuendelea kuliongoza hili taifa kwa miaka mitano zaidi? Naamini kuna wajanja wanaofaidi kwa kutumia udhaifu wa hiyo akili na hao ndio wapiga filimbi wakubwa.

Wanajua kabisa huyu kilaza akiondoka madarakani nao channel zao zitafungwa, wanachokifanya sasa ni kuyashawishi makundi mbalimbali kupiga kelele ili kumuaminisha kilaza anakubalika, kumbe mipango yao iko mbali kabisa kututafuna.
 
Back
Top Bottom