Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?
Ndio tumeamua sasa hivi kila mtu kuwa chawa ili naye aende kula kwa urefu wa kamba yake?
Vijana tuamke kuokoa taifa hili, kwa haya yanayoendelea na nchi itafutika kwa kila mtu kuchota kwa nafasi yake bila kujali maslahi ya nchi.
===
Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi Tanzania umemnunulia Helkopta Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aitumie Helkopta hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakani (2025) atakapokuwa anapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi Julai 20.2024 Msemaji wa umoja huo Mhandisi Yuda Thomas Kemincha amesema sambamba na kununua Helkopta hiyo lakini pia wametoa mafuta ya shilingi milioni 100 za Tanzania, huku akitumia nafasi hiyo kufafanua kuwa hatua hiyo inakuja kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia kuhusiana na yale aliyoyafanya nchini.
Pesa za kuuza maliasili zetu kwa wageni ndizo zinatumika kwa mlango wa nyuma.
Ajabu, wale makandarasi wanaolalamika kila siku hawalipwi pesa zao kwa wakati, leo wanatoa wapi pesa za kununua helkopta? na milioni 100 za mafuta?
- Wajinga wa awamu hii hawana hata akili na uwezo wa kutudanganya.
Hii awamu ya Samia niseme ndio ya hovyo kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya hili taifa, pesa za umma zinaibwa hovyo bila hatua kuchukuliwa, na kutumika hovyo kwenye mambo ya kijinga yasiyo na maana.
Mfano; mabango ya Samia nchi nzima nini maana yake? Samia anajigeuza Pepsi au Fanta anaanza kujitangaza kila mahali! simply wajanja wanapiga dili zao hapo nae amelala tu anajiita chura kiziwi.
Hata Sabodo alishawahi wapa CHADEMA mamilioni ambayo yaliishiwa kuliwa na Mbowe na genge lake. Hao jamaa wamefanya vyema ila namshauri Mama Samia asipande hiyo helikopta. Anaweza hata kumpa mgombea wa CHADEMA aitumie.
Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?
Usidanganyike. Hao hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Wanatumiwa tu kama njia ya kupitishia pesa toka kwa wafadhili; kama waarabu kuziingiza hapa kutununulia serikali mwakani.