Mkuu kumaliza zamani kwa sehemu kubwa kunahusishwa na uzoefu/experience. Huwezi sema ww dereva wa mwaka 2011 uwezo wako uwe sawa na dereva aliyemaliza masomo yake mwezi march.2022. ikiwa wakati wote ulikuwa ukiifanyia kazi taaluma yako.
Ajira za ualimu na afya zilikuwa ni ajira za moja kwa moja kutokana na idadi kubwa ya mahitaji huduma zao kwa taifa. Huu mfumo tokea uwe disturbed miaka ya hivi karibuni serikali haijawahi kutoa tamko la moja kwa moja kuwa serikali haitakuwa na ajira za moja kwa moja kwa hao waalimu na watumishi wa afya wataajiriwa interview kwa kufuata vigezo vya uzoefu,gpa,n.k kama ilivyo kwa kada nyingine.
Kitendo cha serikali kutokutoa kauli yoyote juu ya kusitisha ajira za moja kwa moja serikalini na kitendo cha watumishi wa elimu na afya kupangiwa hata kwenye vituo vya kazi tofauti na vile ambavyo waliviomba kuna ashiria kuwa zile ajira za moja kwa moja bado zipo na lile tangazo la kuwataka waombe ajira kwa barua ni kutafuta uthibitisho tu ili kujua ni Nani yupo teyari kuitumikia serikali lakin kujua idadi ya wahitaji ajira.
Ajira za ualimu na afya zinasemamiwa na WIZARA moja kwa moja tofauti na ajira nyingi za kule ajira portal ambazo unakuta zinasimamiwa na taasisi husika mfano ajira za mashirika,halmashauri,n.k