Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea. Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry

Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea. Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry

Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea kombe la AFCON .Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry geograpyhy wako zero

Timu inayocheza Leo na Equatorial Guinea ni Guinea Conakry watangaze hivyo sio tu kusema tu Guinea

Hebu wahini kusahihisha hilo
Hiyo Guinea Conakry ni kuuita tu ili kiuitofautisha. Lakini nchi kama nchi inaitwa hivyo hivyo Guinea bila kuongeza neno.

Ni kama Congo Kinshasa na Congo Brazzaville. Hizi zote ni Congo, na hata passport itasoma unatokea Congo ila hizo Kinshasa na Brazzaville ni miji mikuu ya kutofautisha hizo nchi mbili.

Ila Equatorial Guinea ni jina kabisa la nchi, wala sio sababu ya kutofautisha. Hivyo maneno "Conakry" na "Equatorial" hayako katika muktadha mmoja.
 
Mm naangalia Tbc sa hv wamebadilisha Naona somo limewaingia
Safi tumepiga sana kelele humu kuwa tuna reporters sio waandishi wa habari Asante TBC mwandish habari mojawapo ya kazi zake ni kuelimisha jamii kuhusu anachotangaza au kuripoti sio ti kuwa kama kasuku tu ohh Guinea wanacheza Guinea ipi

Hili mada vyuo waandaa waandishi wa habari wachukulie kama study case kumaliza Hilo tatizo la Hivyo vyuo kuzalisha reporters tu badala ya waandishi wa habari wenye analytical skills na kuelimisha jamii pia

Nasuburi na kesho nione magazeti wataandika Nini kwenye ukurasa wa michezo walimu wafundisha waandishi wa habari kesho nunueni magazeti yote muone waandishi wenu mlioandaa upeo Wao wa uelewa
 
TBC hao 🤣🤣🤣
images (43).jpeg
 
Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea kombe la AFCON .Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry geograpyhy wako zero

Timu inayocheza Leo na Equatorial Guinea ni Guinea Conakry watangaze hivyo sio tu kusema tu Guinea

Hebu wahini kusahihisha hilo
Jina Guinea lilitokana na nini kwanini nchi 5 zijikute zina Guinea kwenye majina yao?
 
Hata wewe ni kilaza vile vile
Kuna guinea 3 Africa na moja IPO Asia

Equitorial guinea
Guinea Conakry
Guinea Bissau
Haya yote ni mataifa matatu tofauti na yapo Africa
Nyingine ni new Papua Guinea hiyo IPO Asia na Kuna black people vile vile
Papua new Guinea watu wake hujenga nyumba juu ya maji.
 
Nchi ziko tatu
1. Guinea
2. Guinea-Bissau
3. Equitorial Guinea

Guinea ya kwanza, inatamkwa hivyo hivyo kama Guinea bila kuongeza neno lolote
Halafu kwenye bara lingine kuna Papua New Guinea
 
Hata wewe ni kilaza vile vile
Kuna guinea 3 Africa na moja IPO Asia

Equitorial guinea
Guinea Conakry
Guinea Bissau
Haya yote ni mataifa matatu tofauti na yapo Africa
Nyingine ni new Papua Guinea hiyo IPO Asia na Kuna black people vile vile
Hakuna nchi inaitwa Guinea Conakry
 
Jina Guinea lilitokana na nini kwanini nchi 5 zijikute zina Guinea kwenye majina yao?
Kijiografia Guinea ni eneo la Afrika Magharibi, Ghuba ya Guinea.

Makoloni mengi ya Ulaya katika eneo hilo yalijipa majina kama Guinea ya Ufaransa, Guinea ya Ureno, Guinea ya Uhispania, na Guinea ya Ujerumani.

Nchi hizo zilipopata uhuru wao kila mmoja alibakiza jina la Guinea kwa namna moja au nyingine. Guinea ya Ufaransa ikawa Guinea. Guinea ya Ureno ikawa Guinea-Bissau. Guinea ya Uhispania ikawa Equatorial Guinea.

Kihistoria inasemekana neno Guinea linatokana na neno la Kireno Guiné ambalo liliibuka katikati ya karne ya 15 kurejelea nchi zinazokaliwa na Guineus. Pia, Wareno walitumia neno na msemo wa watu kutoka Afrika Kaskazini (Berber) "aginaw" na "Akal n-Iguinawen" wakimaanisha "mweusi" na "ardhi ya watu weusi". Msemo huu waliutumia kuwatambua watu wa Guinea. Kuna maneno mengine ya kibaguzi kama "Ghinawen" wakimaanisha "watu walioungua" walitumia neno hili kutokana na ngozi nyeusi waliyokuwa nayo watu wa Guinea.

Wareno walifika Guinea katika karne ya 15, ndiyo ukawa mwanzo wa kufanya biashara na Ulaya kwenye pwani ya Guinea. Dhahabu, pembe za ndovu na watumwa walibadilishana kwa bunduki na bidhaa nyingine za Ulaya.

Lakini pia, Guinea lilikuwa ni jina la sarafu ya Uingereza. Ni sarafu ambayo ilitengenezwa kati ya 1663 na 1813. Dhahabu iliyotumika kutengenezea guineas za kwanza ilichimbwa katika eneo la Guinea.

Ajabu ni Papua New Guinea. Kisiwa hicho kiliitwa Papua mwanzoni, baada ya jina lake la asili. Wamagharibi wa kwanza kufika huko walianza kukiita kisiwa hicho "Guinea Mpya" kwa sababu walidhani wenyeji wa huko walitokea Guinea kwakuwa walikuwa wakifanana na Waafrika weusi.

Nahodha na mwanajiografia wa Ureno António Galvão aliandika kwamba: "Watu wa visiwa hivi vyote ni weusi, na wana nywele zilizojikunja, ambao watu wa Maluco huwaita Papuas." Maluco (Maluku Islands) ni visiwa vilivyopo huko Indonesia.

Papuwah (Papua) ni neno kutoka lugha ya Malay likiwa na maana "nywele zilizojikunja" (curly hair) na ndiyo lilitumika kuwatambua watu wa Papua ila baada ya Wamagharibi kufika huko wakawafananisha na watu weusi wa Guinea, ndiyo likapatikana jina New Guinea.

"Guinea Mpya" lilikuwa jina lililoundwa na Mhispania Yñigo Ortiz de Retez. Mnamo 1545, alibainisha kufanana kwa watu hao na wale aliokuwa amewaona hapo awali kwenye pwani ya Guinea ya Afrika.

Kwa maana hiyo majina yote Papua na New Guinea yanatumika kuitambulisha nchi ya Papua New Guinea.
 
Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea kombe la AFCON .Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry geograpyhy wako zero

Timu inayocheza Leo na Equatorial Guinea ni Guinea Conakry watangaze hivyo sio tu kusema tu Guinea

Hebu wahini kusahihisha hilo
Kama hili nalo linakupa tabu basi hata Congo Brazavile na Congo Kinshasa zitakupa tabu.

Huku kuna Extra Musica na huku kuna Wenge Musica.
 
Hata wewe ni kilaza vile vile
Kuna guinea 3 Africa na moja IPO Asia

Equitorial guinea
Guinea Conakry
Guinea Bissau
Haya yote ni mataifa matatu tofauti na yapo Africa
Nyingine ni new Papua Guinea hiyo IPO Asia na Kuna black people vile vile
Ya Asia sio wanaiita Papua New Guinea?
 
Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea kombe la AFCON .Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry geograpyhy wako zero

Timu inayocheza Leo na Equatorial Guinea ni Guinea Conakry watangaze hivyo sio tu kusema tu Guinea

Hebu wahini kusahihisha hilo

Ujuaji mwingi, wewe mwenyewe mweupe, Afrika kuna nchi hizi...

1. Guinea - Conakry ni capital city
2. Guinea Bissau - Bissau ni capital city
3. Equatorial Guinea - Malabo ni capital city
 
Watangazaji wapo sahihi. Wakisema Guinea wapo na mpira maana yako wanamaanisha Guinea Conakry.
 
Back
Top Bottom