Kwenye taasisi nyingi iwe serikalini au private sector , asilimia kubwa ya watu wa uhasibu na masijala wanasumbua sana, muhasibu kukamilisha malipo hadi umbembeleze kama vile hiyo pesa inatoka mfukoni mwake , visingizio kibao… mara mfumo , mara mtandao hadi malipo yakamilike hata kwa shughuli za kiofisi kijasho kinakuwa kimekutoka . Mapacha wao watu wa masijala ni wataalamu wa kuficha barua na madokezo au anaamua tu hataki kuipeleka eneo husika , hivi barua au dokezo linawezaje kupotea ndani ya ofisi? Au kuna ulazima gani wa mtu kusindikiza document anapoisubmit masijala kuhakikisha inafika mahali sahihi?
Haya mambo yapo africa tu, nimefanya kazi nchi moja ya wenzetu , namna kila mtu anajitahidi kufanya kazi kwa weledi, kurahisisha kazi ya wenzake na kupunguza urasimu usiokuwa na maana .
Namna hii ni nadra kupachukia mahali pa kazi
Badilikeni ndugu zetu , you are not doing anyone a favor when you do what you are paid to do , acheni hizi tabia za hovyo