Wahasibu na wenye uelewa naombeni msaada wenu hapa tafadhali

detail zinaonesha hiyo ni baki ya mwezi uliopita siyo income ya mwezi huo,na kutakuwaje na double counting wakati umeishaibalance mwezi ulioisha.hiyo ni just CASH BOOK simple kwa mahitaji yake. naona unamshauri kwa mtazamo wa INCOME STATEMENT kwamba baki iwe inaingia kwenye BALANCE SHEET au?
 
Kwani lengo lake ni nini? Je anaandaa taarifa za mapato na matumizi kwa ajili ya urembo au kujifurahisha tu au anaandaa kwa ajili ya kujua kipato chake kwa mwezi against matumizi? Kama anaandaa kwa kujifurahisha basi format yako uliyoitoa inamfaa. Ila kama anaadaa kujua kipato chake halisia kwa mwezi na matumizi yake halisia kwa mwezi formart yako itakuwa ina m-mislead. Atakuwa anaonekana anatengeneza kipato kikubwa kwa mwezi ilihali mapato mengine ni dublication.
 
CASH BOOK inamfaa.siyo kujifurahisha tuu,hapo anatimiza malengo yake,akitaka kujua kipato halisi kwa mwezi husika,anafanya kutoa hiyo baki ya mwezi uliopita anabakiwa na mapato halisi ya mwezi.hicho unachomwelekeza utamchanganya atahairisha na kutunza mahesabu maana itambidi aingie darasani.
 
Pongezi za dhati kwa mleta uzi, wengi hatuna utaratibu wa kuweka kumbukumbu zetu za mapato na matumizi, hasa tusiokua na biashara.

Pili, kama nimemuelewa vizuri Upepo wa Pesa , hii ni kwa ajili yake na sio kwa mambo ya kulipa kodi au kujua faida na hasara kwenye mwenendo wa biashara. Kwa muktadha huo, iwe unaandika kwenye karatasi au kwenye excel sheet, haijalishi, ilimradi wewe uwe unajua kipi ni kipi, cha muhimu, utatumia calculator kukokotoa endapo unatumia karatasi.

Lakini kwa kesi yako, wewe tayari una computer, nakushauri uzingatie alichopendekeza casanova69 ila ufanye marekebisho kidogo, iwepo sehemu utakayowekea formula itakayokokotoa jumla ya mapato ya mwezi husika kutoa baki iliyoletwa kutoka mwezi uliopita pamoja na matumizi ya mwezi husika kupata net income ya mwezi husika.

Nnachosisitiza ni kwamba, jumla ya matumizi, jumla ya mapato, baki/akiba/salio vyote lazima viwekewe fomula ya kukokotoa ila kuwe na maelezo ya hicho ni kitu gani. Pia huenda maneno tu yanatofautiana ila kimsingi kama haufanyi biashara, tutakua na akiba/salio na sio net income. Maneno huenda yakatofautiana lakini kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawa haina neno ilimradi wewe unajua kipi ni kipi.

Mimi sio mhasibu wala sijasomea uhasibu.
 
Sawa mkuu. Ila mtafutie format nyingine basi ili salio lisionekane upande wa income, maana kwenye hiyo format umeweka column mbili ya income and expense.
 
konda msafi inavyoonekana wewe ni mhasibu professional ndio maana unataka mambo yaende kisomi. Kwa madhumuni ya huyu mwenzetu, anahitaji kitu rahisi sana kuweza kutunza kumbukumbu zake tu za mapato na matumizi.
 
Sawa mkuu. Ila mtafutie format nyingine basi ili salio lisionekane upande wa income, maana kwenye hiyo format umeweka column mbili ya income and expense.
iyo income na expenditure ni sawa na DR na CR tu.nimeassume hiyo baki lazima itaendelea kutumika kama pesa zingine yana atachanganya na mshahara unaofuata,naona ile neno INCOME ndio linakuchanganya/unalifikiria tofauti.
 
konda msafi casanova69 The Monk

Nashukuruni sana kwa mawazo yenu!! Nitayafanyia kazi na nitaweka hapa hiyo format nitayo iandaa...

Ila kwa upande flani nakubaliana na konda msafi anaposema salio la mwezi uliopita nisiliweke kwa "income section" ya mwezi ujao.

Nilichoplan kufannya ni hiki...

Nimeshaandaa excel sheet, na ina income na expense section.

Mapato yote ya mwezi husika (inclide salari, posho na mengine) nitayaweka kwenye income section ya mwezi husika.

Na matumizi yatakua kwenye expenses section.

Kupata kipato kilicho baki nitachukua income minus expenses ili nipate jumla iliyobaki baada ya matumizi!!

Sasa kuhusu salio, nita treat kama balance caried forward. Litaonekana kwenye mwezi ujao ila sinto lijumisha kwenye "income section"...litakua kivyake!!

Nitaandaa formula ya kutafuta commulative balance ya kila mwezi na mwisho wa sheet nitajua nina jumla balance kiasi gani na kwenye mwezi husika nimeingiza kiasi gani na kubakiwa na shilingi ngapi!! Nitafanya hivi kwa kila mwezi na kila kota!

Pia kila kipato na matumizi nitaviwekea percentage... Yaani kwa mwezi husika nijue matumizi gani yalikua makubwa na mapato gani yalikua makubwa...in terms of %!

Nikimaliza kuandaa nitaweka hapa kama sample... Mnishauri zaidi!!

Thank y'all!!
 
Upepo wa Pesa hufanyi saving wewe? huna long term plans? ila utafika mbali boss utafika mbali sana, nlishawahi kutumia mfumo huo na nimeanza tena ila mimi tumizi la kwanza kwangu nikaweka saving yes fanya saving kabla ya matumizi na hata baada ya matumizi kinachobaki tupia huko kusave mimi natupiaga vicoba au saccoss, bank kwangu si rafiki mda wowote nachomoa.
Hongera Boss
 
Savings nafanya japo nyingi naacha bank! Mpaka niwe na economic issue ya kufanya..

Yaani nimejikuta napitia madesa ya wahasibu bila kupenda[emoji23]...niko naanda excel sheet hapa... Nataka ni track every coin inayoingia na kutoka...

Na nijue nna salio shi ngapi!! Kabla mshahara haujatoka nitahakikisha nna bamk statement ili nikompee na excel yangu!!

Hii sheet nitaigawa kwa mwezi na kwa kota (kota ina miezi mitatu)... Baada ya hapo nitaigawa tena kwa mwaka!!

Ngoja niifanyie kazi maana haya maisha ukizubaa utakuta jioni imefika alafu droo haina pesa... [emoji23]
 
Hongera mkuu. Good job.
 
Niliwaza hivo but nafikiri huyu bwana atakuwa na maana ya kwamba yeye ni muajiriwa na kwamba anataka tu kuweka kumbukumbu zake za Personal Income and Expenditure which means kwamba Balance yake itafungua mwezi unaofuata na itakuwa cummulative
 


Mkuu lengo ni kujua hasa mapato na matumizi yake na kuweka kumbukumbu zake sawa, si unajua mali bila daftrai inapotea au hauwezi kupangilia kitu usichokifuatilia kwa ukaribu?

Formula yangu haitampotosha kwa sababu itaonekana mwanzoni mwa kila mwezi, kama salio la mwezi uliopita. Na mwisho atakuwa na sehem inayoonesha salio/baki/akiba ya mwezi husika lakini itakua na formula itakayozingatia kutoa ile akiba iliyotoka mwezi uliopita.

Unaweza kufanya jambo lolote na excel ilimradi tu ujue unataka kufikia lengo gani.
 


Huu ni mwanzo mzuri sana mkuu, wengi utaratibu huu haupo. Kuna kitabu kinaitwa The Richest Man in Babylon kitafute kitakusaidia sana.

Kwa ufupi, kimejikita kwenye msingi wa kutengeneza au kujenga nidhamu ya pesa (wengi hatuna hiyo) ukishakua na nidhamu ya pesa, mafanikio mengine yatafuatia tu. Hata uwe na biashara ya kukuingizia pesa kiasi gani, kama hauna nidhamu ya pesa hauwezi kufika popote.

Yeye anashauri kwenye kila unachokipata, jambo la kwanza jilipe kwanza wewe kwa kuweka akiba sio chini ya asilimia kumi ya kile ulichokipata.
 

Attachments

Mkuu ebu kwanza kabla ya kukusaidia toa huo mshahara kwenye column ya revenue. Mshahara always ni expense siyo sehemu ya mapato.
 
Mmmhhhh. Nimesoma mawazo ya wengi humu hata wenye CPA nikasikitika kabisa. Nikakumbuka posting moja iliyomuhusu Mufuruki humu na jinsi watu walivyoichangia. Mimi nitamsaidia Upepo wa Pesa hivi: Kinachotakiwa ni kitu kinaitwa Receipts and Payments aStatement baaaaaassssiiiiiiiiiiii. Hakuna cha Income/Revenue au Expenditure/Expenses. Kwenye hiyo spreadsheet yako pale ulipoandika Income badilisha iwe Receipts na ulipoandika Expenses badilisha uandike Payments. Umemaliza. Ukiwa na shida rudi hapa uwanjani nakusubiri. CPA zetu ni shidaaaaaa.
 
dah ayo ni maneno tu kiongozi,mbona amna tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…