Wahasibu na wenye uelewa naombeni msaada wenu hapa tafadhali

Mkuu ebu kwanza kabla ya kukusaidia toa huo mshahara kwenye column ya revenue. Mshahara always ni expense siyo sehemu ya mapato.
Mshahara ni expense kivipi mkuu wangu? Embu fafanua kidogo.
 
Samahani kiongozi, acha nikuambie kitu kwa nia njema kabisa. Payments na receipts sio expense au income respectively kama ninavyohisi kwa uelewa wako. Receipts ni hela unayoipata au kuipokea so huenda isiwe kipato chako/income yako. Likewise to payments sio expenses. So nakushauri kabla hujaongea jaribu kufatilia mtiririko mzima wa kile mleta uzi anachokitaka. Receipts and payments sio income na wala expenses.
 
Shukrani sana mkuu!! Tuko pamoja
 
Embu fafanua maana zake kiongozi kwa niaba yetu sisi tusiojua uhasibu.
Ukitaka kuelewa vizuri tofauti zake (siyo maana) angalia hapa: Kama mleta mada kapokea mshahara wake wa January kwenye mwezi wa pili, je kwenye report yake ya january income yake itakuwa ni kiasi gani?
 

Kwa hiyo mleta mada akipata mshahara wake wa mwezi wa January kwenye mwezi wa February, (huku mshahara wake wa December akiwa ameupokea mwezi huo huo wa December) kwenye mwezi wa January mapato yake yatakuwa ni nini as afar as salary is concerned?
 
Kwa hiyo mleta mada akipata mshahara wake wa mwezi wa January kwenye mwezi wa February, (huku mshahara wake wa December akiwa ameupokea mwezi huo huo wa December) kwenye mwezi wa January mapato yake yatakuwa ni nini as afar as salary is concerned?
Mkuu hujui kitu. Samahani lakini.
 
Mshahara ni expense kivipi mkuu wangu? Embu fafanua kidogo.
Sawa mkuu sasa nimelisoma swali lako kwa uzuri nikalielewa. Ni hivi;
Mshahara wako siyo revenue, ni income. Revenue kihasibu ni mapato yanayotokana na uuzaji wa bidhaa au huduma flani.
Kwa hiyo kwa mwezi husika kama umetumia mshahara wako na bado ukabaki na salio, mwezi unaofuata hilo salio lako bado litabaki kuwa income kwa sababu kihasibu huwa kuna mwendelezo wa kila account hadi tunapofunga mwaka.
 
Dah... Nimefurahia huu mtanange wa kuelimishana. Sitii neno, nipo na pop corn hapa!
 
Umeleta "concept" mpya mkuu... Good! Kwa hiyo tunapofunga mwaka au kota ndio tunafanya salio liwe "balance carried forward"?
 
Mkuu konda msafi embu njoo toa wazo lako kwenye hii comment ya Echisute
 
Nashauri kwa sababu unataka kutengeneza kitu kirahisi cha kusaidia kujua mapato na matumizi yako kutokana na mshahara kwa mwezi. Napendekeze utengeneze Fund accountability statements. Kwamba ulichokipata unakitumia na kinachobaki kinakuwa na nafasi yake kama anzio kwa kipindi kingine halafu chini unakuwa na raw nyingine inayoonyesha mshahara wa mwezi husika. Then unajumlisha unapata pesa mwendelezo wa matumizi kwa mwezi husika.
 
Kwa kuwa huyu bwana siyo mhasibu niliona nisimchanganye kwa maneno ya kihasibu. Lakini hii ni kitu rahisi kabisa. Kinachotakiwa ni Receipts and Payments Statement basi. Kama uliwahi kuona kitu kinaitwa "CASH BOOK" utaelewa. Receipts and Payments Statement ni replica ya CASH BOOK. Ndiyo maana nikamwambia pale alipoandika Income aweke Receipts na pale alipoandika Expenses aweke Payments. Sasa Konda Msafi hii unaona ni INNOVATION?
 
Thanks for your input! Niko naitengeneza hiyo excel nikimaliza nitaiweka hapa ili mnipe mawazo yenu!! [emoji120]...
 
Huwa nafanya kitu kinachofanana na chako. Lakini kwa njia tofauti kidogo. Nitaieleza na unaweza kuidesa kama utaona inakufaa au ni bora kuliko yako.

Mimi natumia column moja kwa mwezi. Column hiyo moja ina sehemu kuu nne.

Sehemu ya Kwanza (Mapato/Cash Inflows)
Inaanza na line/row ya kwanza naweka balance ya cash kutoka mwezi iliopita. Then naorodhesha vyanzo mbalimbli vya mapato (cash)....hapa kunaweza kuwa na lines/rows kadhaa kutegemeana na vyanzo vyako (mshahara, mkopo, rent, dividend, etc.). Baada ya hapi naweka line ya jumla (subtotal) ya vyanzo vya mapato kwa huo mwezi (line/row moja tu) na halafu line moja tena ya jumla ya balance ya mwezi uliopita na mapato ya mwezi huo (yaani jumla yote ya cash niliyonayo).

Sehemu ya Pili (Matumizi/Cash Outflows)
Kwa kuwa matumizi ni mengi na yanabadilika hapa nakuwa na lines/rows nyingi zaidi. Na kama kuna matumizi naona ni lazima kuwa na breakdown, basi naweka hiyo breakdown kwenye worksheet nyinginezo. Kwa mfano unaweza kuwa na line ya chakula, lakini ukaona ni muhimu kuwa na list ya hivyo vyakula kwa ajili ya control. Baada ya matumizi then ntakuwa na line ya jumla ya matumizi (cash niliyotoa) yote kwa mwezi huo.

Sehemu ya Tatu (Cash Balance)
Hii line/row moja tu. Hapa nakokotoa tofauti kati ya jumla ya mapato yote (kutoka sehemu ya kwanza, including balance ya mwezi ulopita - #nafikiri hii inajibu swali lako la msingi) na jumla ya matumizi yote (sehemu ya pili). Hii balance (baada ya kureconcile na Sehemu ya Nne) ndio utai link mwezi unaofuata kama opening balance.

Sehemu ya Nne (Cash Count/Recon)
Hii ni sehemu muhimu sana. Ni lazima ufanye cash count kila mwisho wa mwezi. Ukiweza kuifanya vizuri itakufunilia mambo mengi sana kuhusu mapato na matumizi yako mpaka utafurahi. Hapa naorodhesha cash zote nilizonazo hapo mwishoni mwa mwezi (ukishindwa basi fanya tarehe moja ya mwezi unaofuata kabla hujaanza kufanya matumizi). Yaani jumlisha balance ya hela zote - mpesa/tigopesa etc, pesa iliyopo kwenye wallet yako, pesa iliyopo kwenye safe (kama unayo), pesa iliyopo kwenye kila bank account yako, kwenye gari, kwenye begi etc. Jumla yote ni lazima ifanane na jumla unayoipata Sehemu ya Tatu. Ukiona hazifanani basi ujue kunaweza kuwa na matizo katika rekodi ya matumizi yako, mapato yako au hujahesabu vizuri pesa iliyonayo. Review records zako mpaka zi reconcile. Hii itakupa discipline sana ya record keeping na hata matumizi yako to the last shilling. Utajikuta unalazimika kuweka record kila siku maana ukisibiri mwishoni mwa mwezi kuna uwezekano mkubwa vitu vingi ukasahu.

Kila la heri.
 
Umeeleza vizuri sana ndio nami nimemweleza kwa ufupi ikiwezekana Nita attach sample kesho
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…