Huwa nafanya kitu kinachofanana na chako. Lakini kwa njia tofauti kidogo. Nitaieleza na unaweza kuidesa kama utaona inakufaa au ni bora kuliko yako.
Mimi natumia column moja kwa mwezi. Column hiyo moja ina sehemu kuu nne.
Sehemu ya Kwanza (Mapato/Cash Inflows)
Inaanza na line/row ya kwanza naweka balance ya cash kutoka mwezi iliopita. Then naorodhesha vyanzo mbalimbli vya mapato (cash)....hapa kunaweza kuwa na lines/rows kadhaa kutegemeana na vyanzo vyako (mshahara, mkopo, rent, dividend, etc.). Baada ya hapi naweka line ya jumla (subtotal) ya vyanzo vya mapato kwa huo mwezi (line/row moja tu) na halafu line moja tena ya jumla ya balance ya mwezi uliopita na mapato ya mwezi huo (yaani jumla yote ya cash niliyonayo).
Sehemu ya Pili (Matumizi/Cash Outflows)
Kwa kuwa matumizi ni mengi na yanabadilika hapa nakuwa na lines/rows nyingi zaidi. Na kama kuna matumizi naona ni lazima kuwa na breakdown, basi naweka hiyo breakdown kwenye worksheet nyinginezo. Kwa mfano unaweza kuwa na line ya chakula, lakini ukaona ni muhimu kuwa na list ya hivyo vyakula kwa ajili ya control. Baada ya matumizi then ntakuwa na line ya jumla ya matumizi (cash niliyotoa) yote kwa mwezi huo.
Sehemu ya Tatu (Cash Balance)
Hii line/row moja tu. Hapa nakokotoa tofauti kati ya jumla ya mapato yote (kutoka sehemu ya kwanza, including balance ya mwezi ulopita - #nafikiri hii inajibu swali lako la msingi) na jumla ya matumizi yote (sehemu ya pili). Hii balance (baada ya kurexoncile na Sehemu ya Nne) ndio utai link mwezi unaofuata kama opening balance.
Sehemu ya Nne (Cash Count/Recon)
Hii ni sehemu muhimu sana. Ni lazima ufanye cash count kila mwisho wa mwezi. Ukiweza kuifanya vizuri itakufunilia mambo mengi sana kuhusu mapato na matumizi yako mpaka utafurahi. Hapa naorodhesha cash zote nilizonazo hapo mwishoni mwa mwezi (ukishindwa basi fanya tarehe moja ya mwezi unaofuata kabla hujaanza kufanya matumizi). Yaani jumlisha balance ya hela zote - mpesa/tigopesa etc, pesa iliyopo kwenye wallet yako, pesa iliyopo kwenye safe (kama unayo), pesa iliyopo kwenye kila bank account yako, kwenye gari, kwenye begi etc. Jumla yote ni lazima ifanane na jumla unayoipata Sehemu ya Tatu. Ukiona hazifanani basi ujue kunaweza kuwa na matizo katika rekodi ya matumizi yako, mapato yako au hujahesabu vizuri pesa iliyonayo. Review records zako mpaka zi reconcile. Hii itakupa discipline sana ya record keeping na hata matumizi yako to the last shilling. Utajikuta unalazimika kuweka record kila siku maana ukisibiri mwishoni mwa mwezi kuna uwezekano mkubwa vitu vingi ukasahu.
Kila la heri.