Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,442
Jamaa anahitaji receipt and payments basi sidhani kama anahitaji statement nyinginezo. Na kama atapeleka pesa bank itatoka kama matumizi ya kawaida lakini mwisho ataonyesha balance aliyonayo cash pamoja na bank. Kuna moja niliweka hapa
Mziba umeeleza vizuri. Unajua ukiwa mhasibu usifikiri kila mtu anajua uhasibu, Unatakiwa kumuelezea kwa njia rahisi bila hata kutumia maneno ya kiuhasibu. Kwa mtu aliyewahi kucheza na cash book au hata petty cash book ni rahisi kuelewa haya mambo. Mtu akisha sema "akipata mshahara wake" lazima ujue kwamba mapato yake siyo ya biashara na matumizi yake vivyo hivyo. Kama anatoa pesa kutoka kwenye mshahara wake kuwekeza kwenye biashara yake hilo ni swala lingine kabisa na kwenye matumizi yake binafsi inatakiwa kuonyeshwa kama "uwekezaji kwenye biashara fulani...."
Kwa ufupi mshahara uarecord to pale ambapo umeupata (yaani Receipts) ukitumia ndiyo unaonyesha matumizi (yaani Payments). Mwisho wa siku unaonyesha Receipts and Payments Account kwa mwezi. Balance ya mwezi ule unaichukua kama receipts ya mwezi mpya. Hakuna reserves account inayohusika pale.