Wahenga, mnauzungumziaje wali enzi zake?

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Naomba niende moja kwa moja kwenye point, nikikumbuka enzi hizo siku unapikwa wali, mtu ulikuwa huchezi mbali, utajizungusha na kufanya kazi ya kila aina ili kuusukuma muda ili muda wa kula wali maharagwe ufike. Utafanya maandalizi ya kila aina kununua ndizi au kutengeneza kachumbali pori.

Kwa upande wako ilikuwaje?
 
Nilikuwa nafagilia sana nyama ya kuku hasa tetea anaetaga mafuta mafuta yale nikitoweza kajitonge ka ugali swadakta sana
 
Ubweche cheka na watoto punga ukipikwa watoto hawachezi mbali na wali wa zamani ulikiwa unanukia kweli kweli.

Ukipikwa hadi mtaa wa saba kwa kina Sky utaunusa.

Mimi bhana vyakula vilikuwa sio kipaumbele changu. Baiskeli manati na mishale ya kununua kwa wauzaji.

Nilishawahi kumgonga mzee na baiki akaichukua akaipeleka mahakamani. Nilishawahi kupiga dogo mmoja mshale wa mguu mtaani hivyo vimishale vikapigwa marufuku kuuzwa.
 
Unakula kwa mkono halafu unaenda kwa watoto jirani zako unawanusisha halafu Unamwambia umesikia harufu ya nn? Akikosea bonge la cheko
Kuna ile kama ni ubweche nyama unachukua nyama yako unaishika kwa mkono wa kushoto kwanza.

Unapiga umbweche ukikaribia kumaliza unabakisha kadogo ka kumezea na nyama. Basi utakombolezea sahani akitokea mtu akaivuta utamchukia maisha yako yote ya utoto.
 
Yaani maisha ya zamani bwana raha tupu
 
Nisipokula wali muda mrefu najifanya naumwa unaweza hisi nmerogwa nakuwa sana mbishi likija swala LA kuoga mtoto wa uswaz sijui midoli wala toy
 
Siku hiyo hata mama haiti mara mbili utasikia Bhokeeeee shauri yako
 
"Omuchele" kwetu bhana wali (omuchele) unatanguliwa na ugali kwanza. Ubwabwa pekee hatushibi!!!!!
 
Wali ndondo nilikua sitoki nyumbani ukipikwa utotoni mpaka leo na uzee wangu naupenda kitu cha naziiii wali nazi ndondo nazi jikoni mwenyewe shunie
 
Nakumbuka siku ya wali nilikuwa busy sana na vijishughuli vidogo vidogo, yaan sitakaa mbali na jikoni. Kwanza nitaoga mapema tena kwa umakini wa hali ya juu, nitakuwa busy na dada jikoni kuagizwa vitu viwili vitatu kusuuza vyombo vya hapa na pale hiyo yote nilikuwa nalinda chakula kikiiva mama alikuwa na utaratibu wa kutoa ule utando wa juu (ukoko) basi nitawekewa kwenye kisosi nanyunyuziwa na mchuzi kidogo daah yale maisha yalikuwa poa sana. Nikimaliza nasubiria paper two sebuleni nile ubwabwa wenyewe sasa. Utoto raha mno.
 
wengine tumezaliwa kwa wauza mchele, so wali ni kila siku asubuhi, mchana na jioni na sikuwa nauchoka...
 
Nilikuwa mvivu sana wa kula lakini mama alibaki hoi alipoambiwa na jirani ninapiga wali maharage na ugali bamia vizuri sana nikiwa kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…