Wahenga semeni ukweli, kuna mengi hamsemi

Wahenga semeni ukweli, kuna mengi hamsemi

Sijaoa ila nmekaa na mwanamke mwaka mmoja ndani. Shida t
Mimi nilikaa nae miezi sita tu na swali kubwa nililokuwa nikijiuliza alafu nalipotezea ni hili ambalo umeuliza wewe leo.
 
Pata mtu sahihi yaan yule mnaoendane,mnachukuliana ,mnaheshimiana na kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzie aisee mtakaa sana ...mm na miaka 23 sasa ya ndoa ila mke wangu ndo furaha yangu ndo roho yangu.Kijana ukija pata mtu sahihi aisee ndoa ni tamu sana
 
Hivi mliwezaje kukaa na mwanamke mmoja tu miaka 35+?

Katika jambo wahenga mlizingua ni hili

Sijawaelewa
Watu wanakaa bila mwanamke kama watawa bila hata ya kuwa watawa, nini huyo mmoja.

Jishikilie kijana.
 
Sijui kwa nini ila nimejikuta naiwaza hivyo unavyosema mmekaza na wao wamekaza.

Sema hii mkutane wenye mioyo ya kusamehe.
Oooh yes! Point yangu ndo ilikuwa inahusu kusamehe. Siku hizi watu wana mioyo mepesi na hawana msamaha.
 
Hivi mliwezaje kukaa na mwanamke mmoja tu miaka 35+?

Katika jambo wahenga mlizingua ni hili

Sijawaelewa
Nipo na wife mwaka wa 24 huu.

Ukitaka kuishi nao vizuri inabidi kwanza utimize majukumu yako vizuri na pia usimbane mwache ajiachie lakini mfanye ajue mistari gani asivuke katika huo uhuru.
 
Hii sio sheria/kanuni kushindwa kwako sio kila mmoja atashindwa hata hao wahenga sii wote waliweza kuna ambao walidumu na wengine hawakudumu.
Sawa mkuu ila nataka waliodumu watwambie waliwezaje
 
Kwa kweli mwanzo ni ngumu lakini jinsi siku zinavyoenda mnasomana tabia na kuvumiliana

Nina miaka mingi sana kwenye ndoa,
Mungu aniongoze mpaka naondoka duniani
 
Wahenga wanazingua hawasemi ukweli
Wengine wanasema walipokuwa wakikaribia nyumbani walikuwa wanafikia sehemu na kutuma watoto watangulie nyumbani kusema kuwa "Mzee amerudi yupo sehemu fulani baada ya nusu saa au lisaa atakuwa hapa". Kwa maoni yao wanasema hii iliwezesha pale nyumbani kurudisha mazingira ya kawaida na kutengeneza mazingira ya kumkaribisha mwenye mji kwa amani kabisa😀
 
Kwasababu wanawake wa enzi hizo hawakua na tabia za hovyo kama hawa wanawake wa sasa,full heshima,full utii,Mume aliheshimiwa kama mfalme wa Nyumba.
 
Back
Top Bottom