Wahenga wa kike: Mnakumbuka nguo za redimedi, sare sare, moka bila kisahau fukufuku

Yaan umenikumbusha muhenga mie bila nguo mpya ya sikukuu sitoki mwananyamala kwetu tulikuwa tunaendaga kutembea mwinyijuma kule kuna kila aina ya michezo au disco toto villa kwa manjunju natamani kurudisha miaka nyuma

Kwa Manjunju pale kwenye ule Mbuyu?
 
Hahahahahahah daaaah nimecheeeka hiyo ya kujipitisha,nilikua nawaambia wenzangu,kaeni hapa nikawaoneshe nguo nimeletewa naenda navaa af natoka nasimama mlangoni,watanishika shika kunisfia mpaka ichafuke
 
Mm nilikuwa napenda mwanamke nyongaaa alafu anaweka kikamba kwa chini ya takoo aliounga nikivuta takooo loteee linabebwaa jujuuuuu
Hahaha huo naujua ila sikuwahi kuuvaa,na bkauzi yake inakua na kikamba ukivuta kanabana maziwa,sista angu kavaa sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] halafu usikute bazee la blue
Yaaaani kama ulikuwepo hahaha lilikua la blue bahari,afu hizo nguo mama mpaka leo zake kazitunza,ila zangu uwii nilikua sizipendi nazichukia akazigawa
 
Yaaaani kama ulikuwepo hahaha lilikua la blue bahari,afu hizo nguo mama mpaka leo zake kazitunza,ila zangu uwii nilikua sizipendi nazichukia akazigawa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukinunuliwa gauni mpya hasa nyakati za sikukuu kila wakati kujaribisha..ili mradi tu kuumiza moyo wenzangu
 
Ee ya suruali na blauzi ndefu mpaka kwenye magoti hivi hahaha kama wahindi
Hahahaha! Ilikuwa raha sana.
Ilikuwa inachanganywa, suruali rangi moja halafu blauzi inakuwa ya maua maua, blauzi inakuwa na mipasuo pembeni.
 
Hapo kwenye Mokasi ni za kiume za kike zilikuwa zinaitwa Skuna, sisi wanaume tulikuwa tuna suruali za Tokyo. Yaani ukivaa Tokyo we mkali, zilikuwa zina mikanda yake noma sana aisee, wadudu maarufu enzi hizo, ni panzi, fukufuku, dondora kwenye mipera, na wale wanaopatikana kwenye michongoma wana pembe kama za ngombe walikuwa wanacbezeshwa kwa kujizungusha chini pembe zao, mwisho kabisa walikwepo bruce lee walikuwa wana mapigo ya kibruce maarufu kama vunjajungu, hahahahahahahaaa nimecheka sana kwa kukumbuka enzi za wakati huo wa kucheza majoka style ni kuchezesha mabega, kwenda kibisa, na mazingaombe ya mashuleni hatari sana wakina power mabula.
Niishie hapo.
 
Yaan umenikumbusha muhenga mie bila nguo mpya ya sikukuu sitoki mwananyamala kwetu tulikuwa tunaendaga kutembea mwinyijuma kule kuna kila aina ya michezo au disco toto villa kwa ujiji natamani kurudisha miaka nyuma
kumbe na ww ulichezaga mule villa? [emoji1][emoji3][emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…