Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,415
- 119,473
Jamani kweli siku hazigandi. Nakumbuka enzi hizo hakuna utitiri wa redio stations ukitaka kusikiliza huna option kama kipindi kilichopo hukipendi uzime tu radio.
Hata mfumo wa vipindi ulikuwa tofauti sana na huu wa sasa...enzi hizo vipindi vililenga kutoa elimu zaidi kuliko burudani. Kama kipindi ni cha kutoa elimu kuhusu masuala ya umeme let's say, hakuna porojo ni elimu tu mwanzo mwisho.
Nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini mwishoni hivi, kuna vipindi nilikuwa sipitwi kabisa hata kama nilikuwa kucheza muda huo ntafanya juu chini niwepo
Kulikuwa na vipindi vya watoto kimoja nilikuwa kinaitwa Mama na mwana kilikuwa kinarushwa jumamosi saa nane na nusu. Nilikuwa sipitwi kabisa....kulikuwa na hadithi zilikuwa zinasimuliwa naikumbuka moja tu ya Binti Chura.
Kuna kipindi kingine kilikuwa kinaitwa Twende na wakati ulikuwa mchezo wa kuigiza unarushwa kila jumamosi saa mbili na nusu usiku. Nilikuwa nafuatilia hatua kwa hatua maana ulikuwa haurudiwi ukipitwa ndo tuonane next episode.
Karibu mdau tukumbushane wewe ulikuwa unapenda vipindi gani?
Sent using Jamii Forums mobile app