Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Halafu Khantwe RTD zamani ilikuwa ikifika saa 6 unaskia

Mungu ibariki afrika
Mungu ibariki Tanzania.

Hadi kesho alfajiri [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu Khantwe RTD zamani ilikuwa haikeshi ilikuwa ikifika saa 6 unaskia

Mungu ibariki afrika
Mungu ibariki Tanzania.

Hadi kesho alasiri [emoji23][emoji23][emoji23]
Umenikumbusha nikiwa Mdogo sana siafu waliingia ndan tukatoka nje kuota moto hukunyumewasha radio kila inafika tu SAA sita mitambo ikazimwa watu tuna hasira ya siafu nikaonda ndugu zangu wakubwa wanalalamika so wangeweka mizk tu sasa tutakesha kweli mpaka asubuhi ikabid tuchukue kanda ya kwaya siikumbuk vizur ila ni wale wa arusha nyimbo zao za kubamba sana na hiyo ikawa holaa kumbe betri zimeisha radio ikawa inaimba pole pole ukipunguza saut inaimba vizur na hamsikii [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani kweli siku hazigandi. Nakumbuka enzi hizo hakuna utitiri wa redio stations ukitaka kusikiliza huna option kama kipindi kilichopo hukipendi uzime tu radio.
Hata mfumo wa vipindi ulikuwa tofauti sana na huu wa sasa...enzi hizo vipindi vililenga kutoa elimu zaidi kuliko burudani. Kama kipindi ni cha kutoa elimu kuhusu masuala ya umeme let's say, hakuna porojo ni elimu tu mwanzo mwisho.
Nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini mwishoni hivi, kuna vipindi nilikuwa sipitwi kabisa hata kama nilikuwa kucheza muda huo ntafanya juu chini niwepo

Kulikuwa na vipindi vya watoto kimoja nilikuwa kinaitwa Mama na mwana kilikuwa kinarushwa jumamosi saa nane na nusu. Nilikuwa sipitwi kabisa....kulikuwa na hadithi zilikuwa zinasimuliwa naikumbuka moja tu ya Binti Chura.

Kuna kipindi kingine kilikuwa kinaitwa Twende na wakati ulikuwa mchezo wa kuigiza unarushwa kila jumamosi saa mbili na nusu usiku. Nilikuwa nafuatilia hatua kwa hatua maana ulikuwa haurudiwi ukipitwa ndo tuonane next episode.
Karibu mdau tukumbushane wewe ulikuwa unapenda vipindi gani?


Sent using Jamii Forums mobile app
Tumbuizo Asilia - Michael Katembo , Khalid Ponera baadae Malima Ndelema

Starehe na BP - Julius Nyaisangah

Misakato - Julius Nyaisangah

Ugua pole - Walikuwa wanazunguka hospitali mbalimbali nchini kupitia wawakilishi wa mikoani na wale wa Dar

Nipe Habari - Siwatu Luanda

Mama na Mwana - Deborah Mwenda

Club Raha Leo Show - Julius Nyaisangah, Enock Ngombale na Geofrey Erneo

Kijaruba - Abdallah Mlawa

Mchana Mwema/Pokea Salamu - Christine Chokunegela na wenzake wengi

Chaguo la msikilizaji - Malima Ndelema

Mkoa kwa Mkoa - Michael Katembo, Nadhir Mayoka, Malima Ndelema

Disco Show - Julius Nyaisangah

General tyre na gari lako - Samadu Hassan

Ngano za Muziki - Salama Mfamao, Siwatu Luanda na wengine

Majira ya asubuhi na saa 3 usiku...

Watoto wetu - Watangazaji wa kike..

Mikingano - Salum Seif Nkamba 'SS Nkamba'

Mkulima wa Kisasa - Malima Ndelema

Michezo/Matangazo ya Mpira - Mshindo Mkenyenge, Omary Jongo, Ahmed Jongo 'Father', Dominick Chilambo, Mikidah Mahmoud, Charles Hillary, Juma Nkamia, Salim Mbonde, Abdallah Idrissa Majura na wengine..

Taarifa ya Habari - Julisu Nyaisangah, Charles Hillary, Betty Mkwasa, Sarh Dumba, Halima Kihemba, Jacob Tesha, Sekione Kitojo, Tido Mhando, Mikidad Mahmoud, Christine Chokunegela, Abdallah Mlawa, Abdul Ngalawa, Eddah Sanga, Aboubakary Liongo, Iddi Rashid Mchatta na wengine...

Mazungumzo baada ya Habari - Abdul Ngalawa, Mikidad Mahmoud

Pia walikuwepo wawakilishi wa Kanda/mikoa

Nyanda za Juu Kusini - Idrissa Sadallah, Martha Ngwila

Kanda ya Mashariki - Halima Kihemba , Penzi Nyamungumi, Monica Lyampawe..

Kanda ya Magharibi - Titus Philipo

Kigoma - Chisunga Stephen

Songea - Abisai Stephen

Lindi - Angalieni Mpendu

Ziwa Victoria - Dominick Chilambo, Nathan Rwehabura

Kanda ya Kati - Ben Kiko, Ahmed Kipozi, Sangi Kipozi, Hendrick Michael Libuda, Daniel Msangya, Wilson Malosha, Hellen Masele na wengine

Mtwara - Cassim Mikongoro

Kanda ya Kaskazini - Ahmed Jongo

Zanzibar - Yusuph Omary Chunda na Makame Abdallah

Hawa ni kwa uchache tu....
 
Umenikumbusha nikiwa Mdogo sana siafu waliingia ndan tukatoka nje kuota moto hukunyumewasha radio kila inafika tu SAA sita mitambo ikazimwa watu tuna hasira ya siafu nikaonda ndugu zangu wakubwa wanalalamika so wangeweka mizk tu sasa tutakesha kweli mpaka asubuhi ikabid tuchukue kanda ya kwaya siikumbuk vizur ila ni wale wa arusha nyimbo zao za kubamba sana na hiyo ikawa holaa kumbe betri zimeisha radio ikawa inaimba pole pole ukipunguza saut inaimba vizur na hamsikii [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha, sasa sijui lengo la kuzima lilikuwa wafanyakazi wa kalale?

Mimi hadi leo ninayo kanda ya Jangalason nimetape baadhi ya vipindi.

Na tulishapigana na kaka yangu sababu ya kutape kanda zake hadi nikamchoma Kisu cha mguu.
 
Back
Top Bottom