Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Yaah kweli khante....akawa anajibadili anakuwa binadamu ila watoto wa karne ile walikuwa maboya wanadanganywa kirahisirahisi watoto wa sasa digitali mnoo

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23] sema tulikuwa maboya...walikuwa akina nani? Hata siku hizi wanadanganywa tu sema uongo wa sasa upo kidigitali pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me kwa kweli nakumbuka sana vinyimbo na matangazo zaidi

Tangazo la Kiwi la asubuhi saa 12....nikilisikia ulikuwa kero tupu maana liliashiria dalili zote za kuchelewa namba shuleni

Naanzaje kusahau wimbo/tangazo la Tanesco "Peleleza bwana Umeme?"

Au naanzaje kusahau tangazo la ile shule ya kiingereza "anaongea kiingereza kigumu?

Au tangazo la sabuni kama sikosei ni protex ya jamaa anajikuna balaa " Omari ngwarara ngwarara"
 
miaka ile ukisikia kipindi cha mashairi saa saba mchana basi ujue mda wa shule umefika kwa darasa la kwanza na pili! Nilikichukia sana kipindi hiki kwani kilimkumbusha maza muda na kunikomalia kwenda shule, wakati mchez ndo umenoga!!
 
Kipindi mahoka kinarushwa yaonekana ulikuwa aidha hujazaliwa au bado mdogo maana hivyo ni vipindi vya zamani zaidi kwako, je umewahi sikia PWAGU MA PWAGUZI au CLUB RAHA LEO SHOW!

Sent using Jamii Forums mobile app
Club raha Leo show nilikuwa nakisikia japo sikuwa nakisikiliza. Kwamba nilikuwa sijazaliwa hapana labda tulikuwa hatujamiliki redio bado[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom