Wahhab kundi lenye itikadi kali ndani ya uislamu

Wahhab kundi lenye itikadi kali ndani ya uislamu

Jamaa mbishi ushirikina mkubwa ni kusema Yesu , mtu aliyezaliwa na binadamu na kula na kunya kama wewe kuwa ni Mungu.

hivi wewe jamaa mbishi nikikuita Nguruwe utafurahi ??? na utaona ni sawa??

na ndio maana Mwenyezi mungu akasema kuwa anaweza kukusamehe makosa yote isipokuwa hilo kosa la kumshirikisha na kiumbe anayekunya
Kijana, ukubali usikubali.....uchawi wote upo ndani ya Uislam. Ufugaji majini, albadiri, makafara, n.k.
 
Hakuna dhehebu linaitwa wahabi kwenye uislam acha ujinga
We ndio acha ujinga unawajua wakristo wa ethiopia.dini inakuja na ukabira bado kusoma kote unakuwa kichwa chepesi
 
Umemaliza na wewe kuwa Muislamu unayemfua mtume صل الله عليه وسلم ndo maana wa Suni wanafata Suna au mwendo wa mtume صل الله عليه وسلم
Huwezi kuifuata sunna wewe mwenyewe na hauwezi kuielewa Qur'an wewe mwenyewe.

Ili uwe na uelewa sahihi wa kuelewa dini ni lazima uwafuate wanawazuoni ambao Mtume mwenyewe amesema ni warithi wa Mitume.

Hapa ndipo inapokuja asili ya neno madheheb, linatokana na kitenzi dhahaba, ikiwa na maana ya mwendo au mwelekeo.

Yaani kutoka kwa Mtume, kuja kwa sahaba fulani (hiyo ni hatua), kutoka kwa sahaba kwenda kwa fulani (hiyo ni hàtua). Zikiwa nyingi zinaitwa madheheb yaani mwendo au mwenendo.

Hivyo ndivyo wanawazuoni wanavyofafanua maana ya madheheb.

Hivyo, wewe ikiwa unafuata uelewa wa mwanawazuoni fulani kuhusu ufafanunuzi wake wa Qur'an na Sunna basi huo ndiyo mwendo au mwenendo uliyoshika wewe. Yaani huo ndiyo mwenendo wako. Kiarabu hiyo hali inaitwa madheheb.

Ikiwa kama wewe ukisema hauna madheheb, tafsiri yake ni kwamba ufafanuzi juu ya Qur'an na hadithi ni wa kwako wewe mwenyewe.

Yaani uelewa wako wa dini hauna sanadi ya kufanya marejeo ya uelewa na kupata ufahamu wa kufafanua na kuelewa Qur'an na Sunna kutoka kwa yeyote isipokuwa ni wewe mwenyewe.

Lakini ikiwa kama uelewa wako wa Qur'an na hadithi unategemea wanawazuoni fulani basi huo ndiyo mwenendo wako wa ufahamu wa dini. Hayo ndiyo madheheb yako.

Mtume hana madheheb kwa sababu yeye ndiye chimbuko la elimu na hekima.
 
Enyi waislam msijipe taabu kwani Uislam ni mwepesi na umewekwa clear usitafute details za kukupotezeni
 
Hakuwa na dhehebu.Alikuwa muislamu tu.
Kipindi cha tabiina na tabitabiina wale ambao wasiyokuwa na elimu au waliyokuwa na ufahamu mchache kuhusu dini yao walikuwa wanawategemea maimamu wakubwa wa kwenye miji ambao walikuwa wanawategemea.

Mfano Imam Al Awzai alikuwa anategemewa Sham n.k

Imam sufyan Authawr alikuwa maeneo ya Iraq.

Imam Layth Ibn Saad alikuwa maeneo ya Misri.

Imam Dawud Al Zahir naye alikuwa kufa huko Iraq.

Imam Abou Hanifa...

Imam Malik, Shafii na Hanbal..n.k

Hao wote walikuwa vigogo wa elimu na ndiyo ambao walikuwa wanategemewa kwenye miji yao.

Kwa hali ya namna hii ndiyo yakazaliwa madheheb, yaani mienendo au mwendo ya kwamba. Yaani; mwendo wangu mimi wa elimu nauchukua wa ufahamu wa Imam fulani.

Baadayw hayo madheheb mengine yote yakapotea, yakabaki manne; yakabaki ya Hanafi, Maliki, Shafii na Hanbali mpaka leo hii 2025.

Hivyo mtu akiulizwa wewe ni madheheb gani? Ana maanisha, mwenendo wako wa ufahamu wako wa dini ni kwa ufahamu wa nani?

Kwa sababu wanawazuoni kwa rehma yake Mungu ndiyo wametutunzia hii dini. Kwa msingi huo ufahamu wako wa dini ni mwenendo upi?
 
Huwezi kuifuata sunna wewe mwenyewe na hauwezi kuielewa Qur'an wewe mwenyewe.

Ili uwe na uelewa sahihi wa kuelewa dini ni lazima uwafuate wanawazuoni ambao Mtume mwenyewe amesema ni warithi wa Mitume.

Hapa ndipo inapokuja asili ya neno madheheb, linatokana na kitenzi dhahaba, ikiwa na maana ya mwendo au mwelekeo.

Yaani kutoka kwa Mtume, kuja kwa sahaba fulani (hiyo ni hatua), kutoka kwa sahaba kwenda kwa fulani (hiyo ni hàtua). Zikiwa nyingi zinaitwa madheheb yaani mwendo au mwenendo.

Hivyo ndivyo wanawazuoni wanavyofafanua maana ya madheheb.

Hivyo, wewe ikiwa unafuata uelewa wa mwanawazuoni fulani kuhusu ufafanunuzi wake wa Qur'an na Sunna basi huo ndiyo mwendo au mwenendo uliyoshika wewe. Yaani huo ndiyo mwenendo wako. Kiarabu hiyo hali inaitwa madheheb.

Ikiwa kama wewe ukisema hauna madheheb, tafsiri yake ni kwamba ufafanuzi juu ya Qur'an na hadithi ni wa kwako wewe mwenyewe.

Yaani uelewa wako wa dini hauna sanadi ya kufanya marejeo ya uelewa na kupata ufahamu wa kufafanua na kuelewa Qur'an na Sunna kutoka kwa yeyote isipokuwa ni wewe mwenyewe.

Lakini ikiwa kama uelewa wako wa Qur'an na hadithi unategemea wanawazuoni fulani basi huo ndiyo mwenendo wako wa ufahamu wa dini. Hayo ndiyo madheheb yako.

Mtume hana madheheb kwa sababu yeye ndiye chimbuko la elimu na hekima.
Ndo maana Kila wakati nilikuwa nakukwepa sababu nilijua unapoelekea, nimemalizana na wewe endelea na usufi wako, eti huwezi elewa Qur,aan na Sunnah mpaka .........
 
Ndo maana Kila wakati nilikuwa nakukwepa sababu nilijua unapoelekea, nimemalizana na wewe endelea na usufi wako, eti huwezi elewa Qur,aan na Sunnah mpaka .........
Suala si kunikwepa! Suala badala ya kuwa na elimu una itikadi, hili ni jambo lisilofaa.

Baada ya Qur'an zinafuata hadithi za mtume, nayo ni sahih al Bukhari. Huyu ambaye wewe unayejiita mwana sunna unafuata hadithi zake. Bukhari ana madheheb, na madheheb yake ni Shafii.

Imam Abul Husayn Muslim ibn al Hajjaj, maarufu Imam Muslim, ambaye tunafuata kitabu chake cha hadithi, naye ana madheheb na madheheb yake ni Shafii.

Ikiwa wewe ni mtu mwenye kutafakari jiulize: Hawa ambao waliyomuelewa Mtume, na kusoma hadithi zake, na kufahamu maana yake na kufahamu sanadi yake mpaka kwa Mtume Muhammad s.a.w, ambao ulimwengu wa kiislamu unategemea vitabu vyao baada ya Qur'an al Kareem wana madheheb. Swala yao hawaifanyii mpaka waangalie Shafii kasemaje!

Wewe unasema hakuna madheheb. Taffakari kwa kina. Kabla hujashiba itikadi, Shiba kwanza elimu.

Kuhusu usufi, mfano babu yangu akiomba dua atasema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِاسْمِكَ الْأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيتَ بِهِ أَجَبْتَ، وَإِذَا سُئِلْتَ بِهِ أَعْطَيْتَ، وَبِأَسْمَائِكَ الْحُسْنَى كُلِّهَا، وَبِأَسْمَائِكَ الَّتِي أَنْزَلْتَهَا فِي كِتَابِكَ، وَبِأَسْمَائِكَ الَّتِي اسْتَأْثَرْتَ بِهَا فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ

Ee Mwenyezi Mungu! Nakuomba kwa Jina lako Tukufu ambalo ukiliitwa kwalo unaitika, na ukiombwa kwalo unatoa, na kwa Majina yako yote mazuri, na kwa Majina yako uliyoyateremsha katika Kitabu chako, na kwa Majina yako uliyoyahifadhi katika elimu yako ya ghaibu.

Akimaliza hapo atamalizia:

Wa as aluka bihaqqi Muhammad swallallahu alayhi wasalllam:

"Na nakuomba (Mwenyezi Mungu) kwa baraka na heshima ya Mtume Muhammad, kisha atamalizia haja zake.

Nikahoji, kwa nini unasema na kwa baraka na heshima ya Muhammad?

Kitabu cha Imam Abdallah Sirajuddiin, kiitwacho "Shahadatu laa ilaha illa llah Muhammad rasuulullah"

Kitabu kikizungumzia maana ya shahada, madhumuni ya shahada, masharti ya shahada na faida za shahada.

Ukurasa wa 18, Imam Sirajuddin ameweka hadithi sahihi akinukuu hadithi isemayo:

"Lammaqtarafa Adamal khatwia (Pindi adamu alipokula tunda),

Qal: (Akasema)

Yaa Rabbi as aluka bi haqqi Muhammad swallallahu alayhi wasalllam illa maa Ghafar talii: Mola wangu nakuomba kwa haki (heshima na baraka) ya Muhammad s.a.w unisamehe madhambi yangu.

Nakuwekea kurasa ya hiyo kitabu kama ushahidi, na Allah kwa sababu ya toba ya namna hiyo alimsamehe baba yetu Adam.

Babu yangu akifanya hivi wewe Jaboja unamtuhumu ni mshirikina, ya kuwa anamshirikisha Mungu, hali ya kuwa si mshirikina, bali amefuata hadithi sahihi ya Mtume jinsi Allah alivyomsamehe baba yetu Àdam madhambi yake.

Na ndiyo maana nikakuuliza tena, nini maana ya usufi? Kwa sababu dua za namna hiyo wanazifanya sana masufi. Kabla ya kumtuhumu babu yangu na sunni wengineo wanaofuata usufi, tuambie kwanza ni nini maana ya usufi?

Kama umezungumza suala ambalo huna ufahamu nalo omba radhi ili kuwanusuru wale ambao wamebeba kauli yako. Na hii si kwa maslahi yangu, bali ni kwa maslahi yako mwenyewe.

Ushahidi wa hicho kitabu ni huu:
Screenshot_20250314_165959_Samsung Notes.jpg

Screenshot_20250314_164938_Samsung Notes.jpg
 
Waislamu bila kujali ni Wasunn,Wahabi,Washia,Wahamadia ni walewale! Wote wanatumia Quran ile ile na Sunna za mtume yule yule.
Ni hatari kwa ulimwengu huu.
Sasa wakina nani ndy sio hatari kwa ulimwengu huu?
 
Sijui umekopy katika kitabu na mashia kipi but ukisikia wahabi ujue kua hilo jina wamepewa na mashia na masufi but hamna mtu wa sunnah anajiita wahabi but ukiwa na msimamo wa kufuata sunna na kukemea uzushi mashia na sufi wanakuita wahabi so hiyo kitu umetoa wapi huko kuandika miaka ni mbwembwe tu
Mnajiita Answar na cheo kikipanda mnajiita salafi... Yaani HAMCHEKI NA WOWOTE😁😁😁
 
Back
Top Bottom