Ndo maana Kila wakati nilikuwa nakukwepa sababu nilijua unapoelekea, nimemalizana na wewe endelea na usufi wako, eti huwezi elewa Qur,aan na Sunnah mpaka .........
Suala si kunikwepa! Suala badala ya kuwa na elimu una itikadi, hili ni jambo lisilofaa.
Baada ya Qur'an zinafuata hadithi za mtume, nayo ni sahih al Bukhari. Huyu ambaye wewe unayejiita mwana sunna unafuata hadithi zake. Bukhari ana madheheb, na madheheb yake ni Shafii.
Imam Abul Husayn Muslim ibn al Hajjaj, maarufu Imam Muslim, ambaye tunafuata kitabu chake cha hadithi, naye ana madheheb na madheheb yake ni Shafii.
Ikiwa wewe ni mtu mwenye kutafakari jiulize: Hawa ambao waliyomuelewa Mtume, na kusoma hadithi zake, na kufahamu maana yake na kufahamu sanadi yake mpaka kwa Mtume Muhammad s.a.w, ambao ulimwengu wa kiislamu unategemea vitabu vyao baada ya Qur'an al Kareem wana madheheb. Swala yao hawaifanyii mpaka waangalie Shafii kasemaje!
Wewe unasema hakuna madheheb. Taffakari kwa kina. Kabla hujashiba itikadi, Shiba kwanza elimu.
Kuhusu usufi, mfano babu yangu akiomba dua atasema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِاسْمِكَ الْأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيتَ بِهِ أَجَبْتَ، وَإِذَا سُئِلْتَ بِهِ أَعْطَيْتَ، وَبِأَسْمَائِكَ الْحُسْنَى كُلِّهَا، وَبِأَسْمَائِكَ الَّتِي أَنْزَلْتَهَا فِي كِتَابِكَ، وَبِأَسْمَائِكَ الَّتِي اسْتَأْثَرْتَ بِهَا فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ
Ee Mwenyezi Mungu! Nakuomba kwa Jina lako Tukufu ambalo ukiliitwa kwalo unaitika, na ukiombwa kwalo unatoa, na kwa Majina yako yote mazuri, na kwa Majina yako uliyoyateremsha katika Kitabu chako, na kwa Majina yako uliyoyahifadhi katika elimu yako ya ghaibu.
Akimaliza hapo atamalizia:
Wa as aluka bihaqqi Muhammad swallallahu alayhi wasalllam:
"Na nakuomba (Mwenyezi Mungu) kwa baraka na heshima ya Mtume Muhammad, kisha atamalizia haja zake.
Nikahoji, kwa nini unasema na kwa baraka na heshima ya Muhammad?
Kitabu cha Imam Abdallah Sirajuddiin, kiitwacho "Shahadatu laa ilaha illa llah Muhammad rasuulullah"
Kitabu kikizungumzia maana ya shahada, madhumuni ya shahada, masharti ya shahada na faida za shahada.
Ukurasa wa 18, Imam Sirajuddin ameweka hadithi sahihi akinukuu hadithi isemayo:
"Lammaqtarafa Adamal khatwia (Pindi adamu alipokula tunda),
Qal: (Akasema)
Yaa Rabbi as aluka bi haqqi Muhammad swallallahu alayhi wasalllam illa maa Ghafar talii: Mola wangu nakuomba kwa haki (heshima na baraka) ya Muhammad s.a.w unisamehe madhambi yangu.
Nakuwekea kurasa ya hiyo kitabu kama ushahidi, na Allah kwa sababu ya toba ya namna hiyo alimsamehe baba yetu Adam.
Babu yangu akifanya hivi wewe
Jaboja unamtuhumu ni mshirikina, ya kuwa anamshirikisha Mungu, hali ya kuwa si mshirikina, bali amefuata hadithi sahihi ya Mtume jinsi Allah alivyomsamehe baba yetu Àdam madhambi yake.
Na ndiyo maana nikakuuliza tena, nini maana ya usufi? Kwa sababu dua za namna hiyo wanazifanya sana masufi. Kabla ya kumtuhumu babu yangu na sunni wengineo wanaofuata usufi, tuambie kwanza ni nini maana ya usufi?
Kama umezungumza suala ambalo huna ufahamu nalo omba radhi ili kuwanusuru wale ambao wamebeba kauli yako. Na hii si kwa maslahi yangu, bali ni kwa maslahi yako mwenyewe.
Ushahidi wa hicho kitabu ni huu: