KERO Wahitimu Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) 2025 hatujapewa vyeti, wanasema “msiwe na haraka"

KERO Wahitimu Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) 2025 hatujapewa vyeti, wanasema “msiwe na haraka"

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa niaba ya wanafunzi tuliohitimu mwaka 2025 katika Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS), tunaomba kupaza sauti kuhusu changamoto kubwa tunayoipata ya kucheleweshewa vyeti vyetu.

Tangu tumalize masomo mwezi Julai mwaka 2025, hadi sasa hatujapewa vyeti. Kila tunapofuatilia chuoni, tunapewa majibu yasiyoeleweka na kuambiwa “msiwe na haraka, subirini,” au “wiki ijayo,” lakini ahadi hizo zimekuwa zikirudiwa kwa miezi mingi bila utekelezaji.

Hali hii imesababisha madhara makubwa kwa wahitimu wengi; baadhi tumekosa fursa za kupandishwa madaraja kazini, wengine tumeshindwa kuendelea na masomo ya juu, na wengine tumekosa ajira kutokana na kukosa vyeti hivyo muhimu.

Aidha, namna tunavyojibiwa wakati wa kufuatilia suala hili si ya kuridhisha, jambo linaloongeza maumivu kwa wahitimu. Tunaomba mamlaka husika ziingilie kati ili chuo hiki kitoe vyeti vyetu kwa haraka, kwani tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu sana bila majibu ya msingi.
 
Back
Top Bottom