GE2025 Wahitimu JKT Wahimizwa kujiepusha na Matumizi mabaya ya Mitandao ya Kijamii hasa wakati wa uchaguzi

GE2025 Wahitimu JKT Wahimizwa kujiepusha na Matumizi mabaya ya Mitandao ya Kijamii hasa wakati wa uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wameona mambo ni mengi sana Mtandaoni wananchi wanakabia juu kwa juu, sasa kazi ni kufanya brain washing kwa vijana wanaotoka kambini na kurejea mtaani

Natumai mmewaambia namna ya kuja kupambana na mafisadi wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yao

---------------

Vijana kote nchini Pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Kijeshi, wametakiwa kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kutumia mitando hiyo kwa manufaa na kujiletea maendeleo hasa wakati huu wa kipindi cha uchaguzi mkuu ili kulinda amani kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla

Hayo yameelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana Oparesheni Nishati Safi, ambao wamepata mafunzo kwa kipindi cha miezi mitatu katika kambi ya kijeshi 824 Kanembwa JKT mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Malassa, ambapo amesisitiza wazazi kuwapa nafasi vijana wao kupata mafunzo ya awali ya kijeshi pamoja na vijana kutakiwa kulinda amani kipindi cha uchaguzi mkuu

Kamanda Kikosi 824 KJ Kanembwa Kanali Mantange Kombe amesema vijana wamepata dozi kamili kwa kipindi cha miezi mitatu wakiwa kikosini, huku wazazi na Vijana wakieleza kupongeza Jeshi kwa kuanda maafunzo hayo kutokana na kusaidia vijana wengi kuwajenga katika uzalendo

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jeneral Jacob Mkunda, aliyewakilishwa na Brigedia Jenerali Maneno Mabakila, amewaagiza vijana kuishi viapo na kufanyia kazi

Soma pia Vijana wa JKT Waonywa Kuhusu Mitandao, Waandaliwa kwa Mapambano ya Taifa

 
Back
Top Bottom